Midimay
JF-Expert Member
- Apr 12, 2015
- 2,907
- 4,770
Habari za mchana wakuu.
Kama swali lilivyouliza; Tetesi na pengine uhakika ni kwamba UTUMISHI wameendelea kuwa na tabia ya kukubali lobying kwa watumishi wanaogopa kustaafu, kuwaongezea mikataba baada kufikisha umri wa kustaafu kwa lazima(kwa mujibu wa sheria na kanuni mbali mbali) yaani miaka 60.
Sote tunajua kwamba Taifa linapitia katika kipindi kigumu sana ya vijana wake wanaohitimu ngazi mbali mbali za elimu kukosa ajira.
Na njia mojawapo ya kutengeneza ajira kwa vijana wake ni walihudumu kwa muda hadi kufikisha miaka 60 ya umri, kustaafu utumishi wao na kwenda nyumbani.
Sasa tabia hii ya kuongeza mikataba imeshakuwa kawaida sana ndani ya UTUMISHI wa umma.
Na hali ni mbaya zaidi ndani ya Taasisi za umma, mashirika ya umma na mamlaka za serikali za uthibiti.
Kama dola ilikuwa haijui hili, basi naomba walitupie jicho.
Tabia hiyo ni hujuma kubwa sana kwa Taifa.
Tunawaongezea wazee ambao nguvu yao ya kuhudumu imeisha. Wakapumzike nyumbani ili nafasi ziwepo kwa ajili ya vijana wenye nguvu.
Tunakubalije lobying za tamaa zao? Kama kwa miaka 30 ya kuhudumu , ataweza kwa miaka mitano au 10?
Sio kuwazibia vijana nafasi ya kupata ajira ndani ya Utumishi wa Umma?
Operation ya kuwaondoa wastaafu wanaoongezewa mikataba ifanyike.
Waende nyumbani ili vijana wapate ajira.