Kwanini utendaji kazi wa Raisi unapimwa kwa kipimo cha siku 100 na sivinginevyo?

WINGER_TEREZA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
242
450
Habari wanajukwaa. Imekuwa ni kawaida kwa Kiongozi Mkuu wa nchi hasa nchi zinzotumia title ya Raisi, kama hii ya kwetu, kutumia kigezo cha siku 100 za kwanza za Raisi kuwa Ikulu kufanyiwa tathimi ya utendaji kazi wake.

Wachambuzi wa mambo ya siasa, wasomi, wanazuoni na Wananchi wa kawaida hutumia siku 100 kupima muelekeo wa Raisi husika katika harakati zake za kutekeleza majukumu yake kwa kutumia hizo siku 100 na mwishoe hufanya tathimi na hata kuja na conclusion.

Kuna wengine wanaamini Raisi akiharibu katika siku 100 za kwanzo Ikulu basi usitarajie kama atafanya vizuri katika kipindi chote kilichobakia hata kama ni miaka 4 na ushee ndiyo imebaki!. Swali langu ni je, kwanini siku 100 ndiyo hutumiwa kama kigezo cha kupima ufanisi wa Raisi?.. Kwanini isiwe siku 60 au miezi 6 au hata mwaka?. Na ni nani yaliyetoa siku 100 kama "SI - unit" ya kumpima Raisi?.

Asanteni, nataka kufamishwa hilo tu maana hiko kipimo hutumiwa dunia kote.
 
Hicho kipimo hua ni cha huko mambele,huku bongo kipimo hua ni miaka 10,afu anaweletea jiwe ili muone umuhimu wake na mafanikio ya mstaafu huyo kipindi akiwa madarakani

Nasema uongo ndg zanguuuuuuuuuu?
 
Hicho kipimo hua ni cha huko mambele,huku bongo kipimo hua ni miaka 10,afu anaweletea jiwe ili muone umuhimu wake na mafanikio ya mstaafu huyo kipindi akiwa madarakani

Nasema uongo ndg zanguuuuuuuuuu?
Hahahaha, hapo unasema uongo ndugu yangu. Mbona hata Jiwe alipoingia Magogoni katika awamu yake ya kwanza baada ya siku 100 alifanya tathimi ya Uongozi wake kwa kuongea na vyombo vya habari. Tena nadhan ndio ilikuwa mara yake ya kwanza na ya mwisho kufanya hivyo maana aliulizwa swali kuntu na Pascal Mayala na badala ya kujibu swali akamdhihaki Pascal kwa kusema Mayala kwao sijui ni Mafunza (kama sijakosea, hahahaha - Jiwe bhana)
 
Back
Top Bottom