Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 6,860
- 12,291
Habari zenu wana JF wenzangu. Ama baada ya salamu, ningependa nijielekeze kwenye mada husika. Ndugu zangu watanzania, baba yetu wa Taifa mwl Julius K Nyerere aliiongoza nchi yetu kwa muda wa miaka 25. Kwa muda wote huo wa uongozi wake, nchi yetu ilikumbwa na misuko suko mingi ambayo haikuja kutokea katika tawala zingine. Mfano wakati wa utawala wa Nyerere tuliona majaribio mawili ya mapinduzi yalioshindwa, hali iliyopelekea mzee wetu aamue kung'atuka mwenyewe kabla haja ng'atuliwa, maana kwa hali ya nchi ilivyokuwa kipindi kile bila shaka mwenyewe aliona kwamba asingeweza kumaliza miaka mingine mitano akiwa madarakani.
Lakini pia ukiachana na hayo ya mapinduzi pia kulikuwa na misuko suko mingine, mfano yale mauaji yaliosababisha waziri wa mambo ya ndani wa wakati ule mzee wetu mh Ally H Mwinyi kujiuzulu uwaziri. Pia kulikuwa na misuko suko mingine iliyopelekea kina mzee Kawawa, bibi Tito Mohammed na wengineo kufungwa jela. Lakini kama hiyo haitoshi, wapo waliamua kukimbia hata nchi na kwenda kuishi ughaibuni, mfano mzee wetu hayati Oscar Kambona na wengineo.
Hapo sijagusia ukosefu wa vitu muhimu nchini kama vile chakula, mafuta ya kupikia na ya taa, ukosefu wa madawa hospitalini, usafiri kuwa washida mpaka yakaletwa yale magari yalioitwa chai maharage, mzunguko wa pesa mtaani ukawa wa mdondo. Nguo, viatu, soksi, mafuta ya kupaka, sabuni navyo vikawa havipatikani.
Cha kushangaza alipoondoka mwl Nyerere na kuingia Mwinyi, hali ilibadilika kwa kiasi kikubwa. Hakuna aliethubutu kuwaza tena mapinduzi, bidhaa zote muhimu zilipatikana kwa urahisi mitaani. Mzunguko wa pesa ukawa mkubwa, mitumba ya nguo, viatu, soksi kila kona, madawa yakawa mengi hospitalini mpaka watu wakaamua kufungua na zahanati zao. Pia hakuna aliewaza tena kukimbia nchi, isipokuwa tuliishuhudia wale waliokimbia utawala wa kwanza wanaaza kurejea katika utawala huu wa pili nk.
Hali hii aliyoanza nayo Mwinyi, naona imeendelea hadi leo. Je, ni kwanini misuko suko ilikuwa zaidi wakati wa awamu ya kwanza na sio awamu zingine? Je mwl Nyerere alihujumiwa au sera zake mwenyewe ndio zili muhujumu? Inamaana mzee Mwinyi kwa kutumia uwezo wake na cheo chake aliweza kulisuka vizuri jeshi letu na kurejesha utiifu wao kwa serikali yao na raisi wao? Je inamanaa Mwinyi hakuwa na maadui wa kuitingisha serikali yake, hadi kupelekea wengine kukimbia kama walivyokimbia awamu ya kwanza? Mwenye kujua zaidi sababu zilizopelekea mwl Nyerere kushindwa kuituliza hali, hadi kuamua kung'atuka anakaribishwa kutujuza. Asanteni sana kwa kunisoma?