Kwanini usuluhishi wa Rais JPM kwa Paul Makonda na Ruge Mutahaba umebuma kiuhalisia?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,464
108,619
Siyo Siri tena na nadhani sasa kuna ' Fukuto ' kubwa kabisa linalozidisha ' bifu ' kali kati ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Bwana Ruge Mutahaba na Watu walio karibu na wawili hawa wanasema kwamba Kitendo kile cha Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli kuwakutanisha pale Mkoani Tanga kama sijakosea ndiyo Kwanza kimezidisha ' bifu ' lao.

Leo nilitaka tujikite kabisa kwamba ni kwanini pamoja na juhudi zote zile za Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli kuwakutanisha huku akiwataka wamalize tofauti zao lakini walionyesha tu ukaribu wao pale pale na ndani ya siku tatu hadi wiki moja na baadae ' bifu ' lao likaendelea hadi hivi leo?

Je wawili hawa kwa Kitendo chao cha kuliendeleza ' bifu ' lao kunatuma ujumbe gani / upi hasa kwa Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli ambaye alijitahidi kuwapatanisha huku akidhani ameshamaliza tatizo lao lakini leo hii lipo pale pale tena sasa likiwa limechua sura mpya?

Je kulikuwa na umuhimu wowote labda kwa Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli awaite na kuwapatanisha wote mubashara ( live ) pale pale katika ule Mkutano wake Mkoani Tanga au ilimbidi awaite tu kimya kimya Ikulu Kwake ili aweze kusikiliza malalamiko yao mmoja mmoja kisha Yeye kama Baba na Kiongozi awasuluhishe tu huko huko bila Wananchi ( Sisi ) kujua?

Nimalizie tu kwa kuwaambia akina Makonda na Mutahaba kwamba wakae wakijua huu muendelezo wao wa ' mabifu ' wakati walishasuluhishwa tena na Kiongozi Mkuu kabisa wa nchi unamdhalilisha sana Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli na si jambo la Kiungwana hata kidogo na nijuavyo hasa katika Mila zetu za Kiafrika Mtu mzima akiwapatanisha Vijana basi mnatakiwa siku hiyo hiyo mumalize tofauti zenu na amani, upendo na utulivu vitamalaki.

Paul Makonda na Ruge Mutahaba mmemuangusha sana Mheshimiwa Rais wa JMT Dr. Magufuli. Badilikeni!

Nawasilisha.
 
Siyo Siri tena na nadhani sasa kuna ' Fukuto ' kubwa kabisa linalozidisha ' bifu ' kali kati ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Bwana Ruge Mutahaba
Rais Dr. Magufuli kuwakutanisha huku akiwataka wamalize tofauti zao
Je wawili hawa kwa Kitendo chao cha kuliendeleza ' bifu ' lao kunatuma ujumbe gani / upi hasa kwa Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli
Je kulikuwa na umuhimu wowote labda kwa Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli awaite na kuwapatanisha wote mubashara ( live )
Nimalizie tu kwa kuwaambia akina Makonda na Mutahaba kwamba wakae wakijua huu muendelezo wao wa ' mabifu ' wakati walishasuluhishwa tena na Kiongozi Mkuu kabisa wa nchi unamdhalilisha sana Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli
Kweli kabisa...yawezekana mtoto wa mjini RUGE bado anakihasira na MKUU WA MKOA, labda anaona alimsaidia mwenzake kuujuwa mji VIZURI, MKUU naye anaona kama isingekuwa RUGE labda mwingine angefanya haya mambo, ila ukweli ni kwamba huu MJI una wenyewe, walizaliwa hapa, kona kona wanazijuwa na nini, bila kusahau uzoefu na umri, tusubiri tuone mwisho wake, ila twajuwa mshindi mwishoni ni nani...
 
Wewe ndio unafikiria hivyo na kutaka iwe hivyo!!!
Hayo ungeandika yametoka katika fikra zako haswa kwa kumtaja Raisi wetu kwa sanaaaaa.

Kupatanishwa ni ulisikia kwamba waishi tangu siku hiyo wameshikana mikono 24/7!!!

Kiukweli auonyeshi nini haswa umeandikia huu uzi zaidi ya kutaka kumtaja Raisi kimakusudi.. au elezea kwanini haswaaaaaa umemuandika kwa sana.
 
Huyo unayemuita msuluhishi ndio muhusika mkuu wa jambo hili, Makonda ni MalyaMungu tu.
Wale Makhirikhiri aliotinga nao Clouds Makonda hana authority ya kuwatumia na wala Makonda hana hadhi ya kulindwa na Makhirikhiri.

Wakati Benard Membe akiwa waziri wa mambo yanchi za nje nilikuwa nakwenda nyumbani kwake mara kwa mara pale Oysterbay lakini getini walinzi ni private security company, ila nilikuwa nikienda nyumbani kwa Katibu mkuu Kiongozi Luhanjo ndio nakuta getini mlinzi ni kutoka Tiss lakini na mavazi ya kawaida.

Makonda kama ni ulinzi angepewa FFU wamlinde lakini siyo Makhirikhiri, msingi wa kukupa dibaji hii ni kwamba ujuwe wazi kiburi cha Makonda si cha bure kinatoka kwa yule aliye juu, na mpaka sasa hakuna ajuwaye hawa watu wana siri gani inayowapa bond kiasi hiki kiasi kwamba Makonda anajiamini kuliko kiongozi yoyote yule wa kuteuliwa kwenye hii serikali

Siku zote muda ni mwalimu mzuri sana swala la muhimu ni kuomba uhai tu muda utatueleza yaliyojificha, lakini kiukweli kwahili namtetea Ruge shida iko magogoni.

Kosa la Clouds ni kukataa kutumika kwenye ugomvi binafsi wa Makonda na baba yake vs Bishop Gwajima kwa kurekodi video fake kumdhalilisha Gwajima.

Zingine zote porojo issue ni hiyo, na Makonda alishamuweka baba yake standby ikulu kwamba asubiri kipindi kitarushwa na Shilawadu mzee akasubiri bila mafanikio.

Kwahiyo tusiipotoshe jamii, msuruhishi ni sehemu ya tatizo, ule ulikuwa ni usanii tu.
 
Ukionaga jina la bashite tu kiharage kinawasha
 
Wewe ndio unafikiria hivyo na kutaka iwe hivyo!!!
Hayo ungeandika yametoka katika fikra zako haswa kwa kumtaja Raisi wetu kwa sanaaaaa.

Kupatanishwa ni ulisikia kwamba waishi tangu siku hiyo wameshikana mikono 24/7!!!

Kiukweli auonyeshi nini haswa umeandikia huu uzi zaidi ya kutaka kumtaja Raisi kimakusudi.. au elezea kwanini haswaaaaaa umemuandika kwa sana.
Mpinga ukweli Daima. Hakuna kitakachoandikwa kuhusu Bwanako ukaacha kupinga. Hata kama wamesema nyie ni mwili mmoja ndo upinge kila kinachomhusu?
 
Huyo unayemuita msuluhishi ndio muhusika mkuu wa jambo hili, Makonda ni MalyaMungu tu.
Wale Makhirikhiri aliotinga nao Clouds Makonda hana authority ya kuwatumia na wala Makonda hana hadhi ya kulindwa na Makhirikhiri.

Wakati Benard Membe akiwa waziri wa mambo yanchi za nje nilikuwa nakwenda nyumbani kwake mara kwa mara pale Oysterbay lakini getini walinzi ni private security company, ila nilikuwa nikienda nyumbani kwa Katibu mkuu Kiongozi Luhanjo ndio nakuta getini mlinzi ni kutoka Tiss lakini na mavazi ya kawaida.

Makonda kama ni ulinzi angepewa FFU wamlinde lakini siyo Makhirikhiri, msingi wa kukupa dibaji hii ni kwamba ujuwe wazi kiburi cha Makonda si cha bure kinatoka kwa yule aliye juu, na mpaka sasa hakuna ajuwaye hawa watu wana siri gani inayowapa bond kiasi hiki kiasi kwamba Makonda anajiamini kuliko kiongozi yoyote yule wa kuteuliwa kwenye hii serikali

Siku zote muda ni mwalimu mzuri sana swala la muhimu ni kuomba uhai tu muda utatueleza yaliyojificha, lakini kiukweli kwahili namtetea Ruge shida iko magogoni.

Kosa la Clouds ni kukataa kutumika kwenye ugomvi binafsi wa Makonda na baba yake vs Bishop Gwajima kwa kurekodi video fake kumdhalilisha Gwajima.

Zingine zote porojo issue ni hiyo, na Makonda alishamuweka baba yake standby ikulu kwamba asubiri kipindi kitarushwa na Shilawadu mzee akasubiri bila mafanikio.

Kwahiyo tusiipotoshe jamii, msuruhishi ni sehemu ya tatizo, ule ulikuwa ni usanii tu.
:D
 
Back
Top Bottom