Kwanini USA ilishindwa Vietnam lakini imefanikiwa Vita za Mashariki ya Kati kama Iraq, Syria, Afghanistan na Saudia?

jiwekuu770

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
2,247
1,634
Kama kichwa Cha habari

Je, kwanini USA imefanikiwa kivita na kiushawishi na kuingilia mifumo ya nchi za mashariki ya kati na lakini ilishindwa na VIETNAM?

Kuna watakao sema backup ya China. Kumbukeni kuwa Mashariki ya kati Kuna backup ya Russia!

NAWASILISHA

Jiwekuu
 
Una uhakika imefanikiwa Afghanistan na Iraq? Hizo nchi zingine sijui kama Marekani imo vitani (rasmi) huko.

Back up ya China? Kwa maana kwamba China ilikuwa inaisaidia Vietnam ama? Russia inapinga maslahi ya Marekani Mashariki ya Kati sasa back up yake itakuwa imesaidiaje Wamarekani kushinda kama unavyodai.

Mada yako haieleweki mkuu na naamini huna uelewa sawa sawa wa haya mambo au umeandika kwa haraka sana. Tulia uwasilishe hoja yako vizuri.
 
Una uhakika imefanikiwa Afghanistan na Iraq? Hizo nchi zingine sijui kama Marekani imo vitani (rasmi) huko.

Back up ya China? Kwa maana kwamba China ilikuwa inaisaidia Vietnam ama? Russia inapinga maslahi ya Marekani Mashariki ya Kati sasa back up yake itakuwa imesaidiaje Wamarekani kushinda kama unavyodai.

Mada yako haieleweki mkuu na naamini huna uelewa sawa sawa wa haya mambo au umeandika kwa haraka sana. Tulia uwasilishe hoja yako vizuri.
Ningekua cna uelewa ningejuaje Kama USA ilipgana Vita na Vietnam na wakasalenda!!?
Ningejuaje kua aliangusha utawala wa sadam Iraq, mhusika wa Vita ya Syria

Amepgana Sana na makundi ya kigaidi Afghanistan...ameweza kusiteka kiuchumi na kisiasa nchi Kama S.Arabia,U.A.E,Qatar,Kuwait,Oman,Iraq n.k

Mkuu ungesema napelea info lakini cyo cna uelewa ..au kwako mtu ambae Hana uelewa n mwenye anasema USA haijawai pgana na Iraq?
 
Tofauti ni kwamba Vietnam wamarekani walipigana kama wao wakashindwa lakini mashariki ya kati kama ulivyotaja wametegemea majeshi ya nchi washirika mfano ile vita ya kuikomboa Kuwait Marekani ilisaidiwa na mataifa 28. kuna mwaka fulani nchi ya Marekani ilituma majeshi somalia kichapo walichokipata huko ni siri yao.
 
Ningekua cna uelewa ningejuaje Kama USA ilipgana Vita na Vietnam na wakasalenda!!?
Ningejuaje kua aliangusha utawala wa sadam Iraq, mhusika wa Vita ya Syria..
Basi umeandika kwa haraka sana kiasi kwamba ni vigumu kidogo kuupata muhimili hasa wa hoja yako hasa katika siasa tata na changamano za Mashariki ya Kati. Nilikuwa sijui kama Marekani wako vitani na Saudia, Iran na Syria. Hata Afghanistan na Iraq huwezi kusema moja kwa moja kuwa wameshinda bila kuelezea unamaanisha ushindi upi.

Afghanistan Mataliban bado wapo tena wana nguvu kweli kweli na Wamarekani wanaendelea kuuwawa. Iraq nako walikokwenda kwa mbwembwe wakidhani kuwa watapokelewa kama wakombozi kisha wajichotee mafuta ya bure huku wakipandikiza demokrasia yao ya Kimagharibi bado hawajafikia lengo lao kuu mbali na kumuua Saddam na kuiacha nchi ikiwa imegawanyika vipande vipande.

Kuna mambo mengi mno ya kieneo (Geopolitics)na kihistoria na post yako imekaa kijumla jumla na kirahisi rahisi mno.
 
Sidhani kama kuna mafanikio yoyote ya Marekani katika Mashariki ya kati. Hawa ni kivuruge, kama ilivyokuwa Vietnam na kwengine kote ni kuleta vurugu na mauaji. Labda wamefanikiwa kuuza silaha kwa nguvu, kupora mafuta n.k. vita waliyotegemea kuipiga kwa mwezi, sasa inadumu miaka 15 na hakuna kinachoeleweka, ni mafanikio hayo?
 
Uzalendo.. wale jamaa wako ma mapenzi ya dhati na taifa sio kama kwetu bongo leo inaweza ikatokea vita na kuna watu watakuwa wako kinyume na taifa lao na usikute ni watu wenye ushawsh mkubwa kwa jamii kama wanasiasa ama viongozi wa dini
 
Kwenye vita ya vietnam,lengo lilikuwa moja,kuzuia wacomunist wa soviet,Urusi ya zamani,wasikite mizizi ndani ya hiyo nchi,

Wacomunist walifurushwa afghanstan,mapinduzi yote ya serikali za latin america,yalifanyika,ili kuzuia Ucomunist usitie mizizi.

Vietnam USA, ilifanikiwa sana,ila kwa gharama kubwa, USA, ilishindwa CUBA tu.
 
Kwenye vita ya vietnam,lengo lilikuwa moja,kuzuia wacomunist wa soviet,Urusi ya zamani,wasikite mizizi ndani ya hiyo nchi,
Wacomunist walifurushwa afghanstan,mapinduzi yote ya serikali za latin america,yalifanyika,ili kuzuia Ucomunist usitie mizizi.

Vietnam USA,ilifanikiwa sana,ila kwa gharama kubwa,USA,ilishindwa CUBA tu.
Hizo taarifa umezitoa wapi ndugu ?.mbona kama vile za kwenye vijiwe vya bangi.

Vietnam ni wazi kabisa wala hakuna ubishi kuwa Marekani alinyosha mikono juu, na sababu sio kuzuia wakomunist wasitie miguu bali alitaka kuweka utawala wake pale Vietnam.

Baada ya kupokea kichapo na kuchimba Wasovieti waliweka naval base, sasa hao wakomunist gani waliozuiwa ndugu?.

Afghanistan mpaka muda huu kashaferi bado tu kutangaza moja kwa moja maana wanaogopa aibu.Taliban kila kukicha wanazidi kuchukua tu maeneo huku nguvu ya Marekani ikizidi kupungua kila kukicha.wamepanga kutoa wanajeshi wao wote nchini Afghanistan.

Tukija Iraq na Syria ndo tusiseme maana ni zaidi ya kuferi.ni wazi kwa sasa Marekani kwenye mambo ya kijeshi hana ushawishi, siraha moja aliyobakiza ni ya vikwazo
 
Hii ndo Afghanistan
15july_Afghanistan.jpeg
 
Kama kichwa Cha habari

Je, kwanini USA imefanikiwa kivita na kiushawishi na kuingilia mifumo ya nchi za mashariki ya kati na lakini ilishindwa na VIETNAM??

Kuna watakao sema backup ya China. Kumbukeni kuwa Mashariki ya kati Kuna backup ya Russia!!

NAWASILISHA

#Jiwekuu

Mkuu Marekani alishindwa Vietnam kutokana na uungwaji mkono mkubwa wa Urusi kwa wakomunisti wa Vietnam. Tukumbuke miaka hiyo Urusi ikiitwa Jamhuri ya nchi za Kisovieti ilimwaga misaada katika namna ya Fedha, Mafunzo na ushauri wa kijeshi na kiitikadi kwa wakomunisti wa Vietnam,vilevile Warusi walijiona Kama wakombozi wa watu hivyo walifanya kila namna kuhakikisha itikadi ya kijamaa inatapakaa ulimwenguni kote na Vietnam waliiona Kama fursa.
Pia Marekani alishindwa kutokana na kutokuwa na ufahamu mzuri wa Jiografia ya Vietnam vitu kama milima,misitu minene na mito ilitumiwa vyema na wenyeji wa kikomunisti katika mashambulio yao na kusababisha hasara kubwa kwa vifo vya Askari na uharibifu wa silaha za jeshi la Marekani. Jambo ambalo Marekani na wenyeji wao waliowaunga mkono walishindwa kutumia vizuri.
Hasara kubwa waliyopata Marekani kulipelekea wananchi Wao nyumbani kutoa wito kwa serikali yao kurudisha nyumbani askari wake kwani familia zilipoteza wapendwa wao huku wengine wakipata ulemavu wa kudumu.

Marekani imefanikiwa hasa katika kuvuruga amani na utaratibu mzima wa maisha huko Mashariki ya Kati katika nchi za Iraq,Libya na naitaja Afghanistan japo Mambo hivi Sasa yanageuka katika maeneo haya.
Huko Iraq nchi ya Iran inajiongezea ushawishi mkubwa kila Leo mathalani hivi karibuni kulishuhudiwa maandamano ya watu wakiitaka serikali ya Iraq kuondoa Askari wa kimarekani nchini humo na wengine walivamia ubalozi wa Marekani nchini humo kushinikiza kuondolewa kwa majeshi ya Marekani.
Kule Afghanistan watu wanaowaita wanamgambo wa Taaliban wanawapa tabu mpaka Sasa huku kila Leo wakitwaa maeneo na moja ya ushahidi wa hili ni mchakato wa makubaliano ya Amani yanayopangwa na Mmarekani mwenyewe yanayolenga kuundwa kwa ushirika baina ya viongozi wa Taaliban na serikali ya Afghanistan, wakati huohuo Marekani inajiandaa Kuondoka kabisa nchini humo.
Libya walifanikiwa kumuondoa hasimu wao Gadafi ila hivi Sasa Mambo hayaeleweki nchi za kigeni zimevamia kila mmoja akizingatia maslahi yake.
Syria mpaka hii Leo Marekani imeshindwa kumng'oa Rais Assad wa nchi Hiyo na sababu kuu ni uungwaji mkono anaoupata bwana Assad kutoka kwa Urusi na Iran ambao kwa pamoja NI mahasimu wa Marekani.

Ama tukija kwenye sababu za wao kushinda mashariki ya Kati naweza kueleza kuwa; Marekani ina washirika wengi Mashariki ya Kati Kama Saudia, UAE na Israel Hawa wote wanamsaidia kwa namna Moja ama nyingine katika Oparesheni zake za kijeshi katika nchi hasimu. Uwepo wa kambi za kijeshi katika nchi Kama Israel na Saudia ambazo ni majirani wa nchi anazoshambulia kumekuwa na msaada mkubwa Sana kwa majeshi ya Marekani hasa katika kurahisisha umbali wa mashambulizi, yaani badala ya Marekani kuwapiga Taaliban kutokea Ulaya au Washington wanawapiga kutokea Pakistan au Iraq na kutoka katika nchi hizi Askari wake wanapata Supply zao muhimu na kwa wakati hivyo kuongezea ufanisi katika Oparesheni.
Pia, Kukua kwa teknolojia ya kijeshi ni sababu tosha kuelezea mafanikio yao ya kijeshi katika ukanda huo. Matumizi ya ndege zisizo na rubani zimewasaidia Sana katika kukusanya taarifa za kijiografia na utambuzi wa asili ya maeneo hivyo imefanya iwe rahisi kwao wao kutambua uwepo wa adui na kutambua uelekeo wa adui.

Naamini umepata majibu.
 
Back
Top Bottom