Kwanini uraia wa Tanzania unatolewa kama njugu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini uraia wa Tanzania unatolewa kama njugu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Mar 1, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]TUMELAZIMIKA leo kuzungumzia suala la utoaji holela wa uraia wa Tanzania kutokana na mambo mawili makubwa. Kwanza, ni utamaduni wa Serikali ambao unaendelea kushika kasi hadi hivi sasa wa kuwapa wageni uraia wa Tanzania kama vile nchi yetu haina mwenyewe. Tanzania ni nchi pekee duniani ambayo viongozi wake hawajui thamani ya uraia, pengine kutokana na historia ya nchi kuwa kisima cha amani ambako wakimbizi kutoka sehemu nyingi duniani walikimbilia kutafuta hifadhi.

  Pili, ni kuwapo kwa sera tatanishi kuhusu dhana ya uraia na uhamiaji, kiasi kwamba wakati fulani Serikali iliamuru wakimbizi waitwe wageni kwa maelezo kwamba kuwaita wakimbizi ni kuwadhalilisha. Kwa upande mwingine, tafsiri ya ukimbizi na uhamiaji ilipotoshwa na dhana ya ukombozi wa Bara la Afrika ambayo wanasiasa wengi waliichukulia kumaanisha kwamba Afrika ni moja, hivyo mipaka ndani ya bara hilo ilikuwa bandia kwa sababu iliwekwa na wakoloni ili kuwagawa Waafrika kwa lengo la kuwatawala na kuwanyonya.

  Ndiyo maana Serikali haikutilia maanani umuhimu wa kuwa na sera ya uhamiaji kwa maana ya utoaji wa uraia kwa wageni ambayo ni endelevu na ya uwazi. Pasipo kutathmini madhara ya kisiasa na kiuchumi ya kufungua mipaka holela kwa lengo la kuwakaribisha wahamiaji na wakimbizi, Tanzania iliyokuwa makao makuu ya Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) wakati huo, ililewa sifa ilizokuwa ikimwagiwa na jumuiya ya kimataifa kwa jinsi ilivyokuwa ikitoa hifadhi kwa wakimbizi na kuwahudumia pengine kuliko ilivyokuwa ikifanya kwa raia wake. Serikali ilitumia fedha na rasilimali nyingi siyo tu kuwahifadhi, bali pia kuhakikisha wanaangusha tawala za kikoloni kijeshi katika nchi zao na kusimika uongozi wa kizalendo.

  Tunaposema hivyo hatuna maana kwamba kuhifadhi na kusaidia wakimbizi halikuwa jambo la kheri. Tunachosema ni kwamba yalikuwa makosa makubwa kwa Serikali kutobadilika kwa kutunga sheria na sera endelevu za uhamihaji na utoaji uraia kwa wageni baada ya nchi zilizokuwa chini ya ukoloni, zikiwamo Zimbabwe, Afrika Kusini, Namibia, Msumbiji na Angola, kupata uhuru na wakimbizi kurudi makwao.

  Inasikitisha kuona kwamba Serikali haikubadilisha mwelekeo ili sera zake ziweke vipaumbele vya kuinua uchumi, kuleta maendeleo na ustawi wa jamii kwa kuhakikisha kwamba rasilimali zake zinanufaisha raia na uraia unatolewa kwa uangalifu mkubwa, kwa uwazi na kwa kutumia vigezo ambavyo havitiliwi shaka.

  Badala yake tumeendeleza sera dhaifu za uhamiaji na utoaji wa uraia kwa wageni na ndiyo maana kila kukicha tunashuhudia mamia ya wazamiaji wakiingia nchini na kuigeuza nchi yetu shamba la bibi. Ni Tanzania pekee ambapo Serikali inatoa uraia kirahisi kwa wageni kwa kutoa tangazo moja katika gazeti ikisema fulani anaomba uraia, hivyo kama kuna mtu anapinga mgeni huyo kupewa uraia amwandikie Mkurugenzi wa Uhamiaji. Baada ya tangazo hilo wananchi huachwa gizani pasipo kuambiwa matokeo ya ombi hilo.

  Hiyo ndiyo hali halisi, kwani wananchi hawaambiwi fulani wa nchi fulani, mwenye umri na jinsi fulani, kapewa uraia kwa vigezo fulani. Pia hawaambiwi uraia umetolewa kwa watu wangapi, watu gani, katika kipindi gani na kwa mchakato gani. Kwa maneno mengine, utoaji uraia ni siri nzito iliyo mioyoni mwa watawala.

  Katika nchi nyingine, serikali hazitoi uraia bila kuangalia faida itakayopatikana. Serikali huangalia mambo mengi, yakiwamo uwezo wa kifedha wa mwombaji, ustaa wake wa kiwango cha juu (mwimbaji, msanii, mcheza tenisi na kadhalika) na kiwango cha juu cha ubingwa na weledi wake katika taaluma mbalimbali kama udaktari na uinjinia. Hapa nyumbani uraia wanapewa watu tegemezi, tena wenye umri mkubwa na mzigo kwa uchumi wetu.

  Ni kwa sababu hiyo tunaitaka Serikali iangalie upya sera yake ya uhamiaji na utoaji uraia kwa wageni, kwani wananchi wamechoka kuona nchi yao ikiendelea kugeuzwa shamba la bibi.

  Chanzo.
  Kwa nini uraia wa Tanzania unatolewa kama njugu?
   
 2. Straddler

  Straddler JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Biashara hiyo, kaka...:A S-coffee:.
  Nilishawahi kumuuliza swali hilo Ofisa mmoja wa idara ya Uhamiaji. Akanijibu "...tukale wapi?"
   
 3. J

  Jonas justin Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndo serikali yetu hiyo inayoongozwa na magamba...
   
 4. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Hiyo kama haitoshi vile, tunataka pia kupitisha sheria ya uraia wa nchi mbili!
   
 5. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Xenophobia,mhhh
   
 6. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  ukitaka kujua uraia hautolewi kama njugu,just go against the system..if you don't believe me ask ulimwengu,..
   
 7. Gwandalized

  Gwandalized JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Acha ubaguzi wewe,ardhi kibao
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kupata uraia wa Tanzania imekuwa kitu rahisi kuliko uraia wa nchi yoyote dunia.Ningependa katiba mpya utaratibu wa kupata uraia wa Tanzania ubadilishwe mara moja.Vigezo vya kupewa uraia wa Tanzania viangaliwe upya kugawa uraia kama njugu,usiri na urahisi lazima viondolewe.

  Vigezo kama elimu,uwezo wa fedha,umahiri na ubora katika fani mbali mbali,utii wa sheria za nchi na faida itakayopatikana iwapo uraia wa Tanzania utatolewa kwa mtu ujulikane na wananchi wote wa Tanzania.
   
Loading...