Kwanini upo hai mpaka leo?

Uswiss

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
842
2,159
Maswali fikirishi.
1. Kwanini unaishi
2. Kwanini upo hai mpaka leo?
3. Umezaliwa ili iweje?

Maswali haya ni magumu sana kwa mtu asiyejua kusudi la maisha yake. Kila mtu ana kitu ambacho mungu amemdhamiria kuwa na kukiishi hapa duniani kabla ya siku zake kutimia.

Kulitumikia kusudi la maisha yako sio kazi kubwa kama kugundua nini kusudi la maisha yako. Ni kawaida ya mungu kwamba mwanadamu anapomaliza kusudi la kuishi kwake hapa duniani basi anamchukua. Katika safari ya kulitafuta kusudi kuna mambo mengi yanaweza kutukwamisha kuelekea katika kulitimiza kusudi la maisha. Mf. Hofu, dhambi, kukataliwa, umasikini, nk. lakini pia inawezekana mpaka leo mtu hajajua kusudi halisi la yeye kuishi hapa duniani. Kuna mtu ambaye anaishi ili kuwafanya wengine wafurahi, kusaidia watu, kuwaongoza .nk. Lakini kuna wengine wanaishi ili kutangaza njia ya uzima na kweli ya mungu. Kila mtu ana makusudi yake ya kuishi.

Kusudi la maisha utalijua kwa kugundu ni nini unaona/unapenda kuwa ndani yako.(mithari 23:7)

MUNGU AWABARIKI.
 
Haya maswali haya wanakuwaga nayo motivational speakers wenye kuanza ufugaji na unyoya mmoja sasa hivi Wana kuku 500,000.
Ila tunawacheka kwa jicho fulani tu....hahaa...mbona watu wanafanikiwa na wameanzia chini? Wale tunawaitaje....
Kuna mtu mmoja namjua ameanziaga chini leo ana ukwasi wankutosha au naye ameingia freemason?😀😀!
 
Tupo hai mpaka leo kwasababu hatujakutana na kitu cha kutuua (ajali, ugonjwa mkubwa nk). Tungekua tumekutana nacho tusingekua hai.
 
Ila tunawacheka kwa jicho fulani tu....hahaa...mbona watu wanafanikiwa na wameanzia chini? Wale tunawaitaje....
Kuna mtu mmoja namjua ameanziaga chini leo ana ukwasi wankutosha au naye ameingia freemason?😀😀!

Sometimes it's very real. Ila kuna wengine fiksi wanatuandalia mazingira ya kutupiga.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom