Kwanini uogope Kuulizwa Dini, Kabila na Jinsia yako, Je wewe sio Raia wa Tanzania?

Kwa hiyo siku hizi wanafunzi wakifanya application UDSM wanaangalia huyu ni kabila gani ili wamcjague? Hata kama ana sifa lakini kwa kuwa idadi ya kabila lake imeshatimia hachaguliwi? Nina wasiwasi na utafiti wako. Kwa maoni yangu watu wanachaguliwa kwa merit na sio kabila, mtu anaajiriwa kwa merit sio kabila pamoja na lwamba tunajivunia makabila yetu kama wewe Mkinga.
Hana akili huyo
 
Yuko sahihi na siyo kwa udsm tu, ni kwa vyuo vyote ni muongozo wanapewa na serikali na kutekeleza.
 
Hebu nipe mfano labda tume fanya interview halafu wote tume pita na qualification ziko sawa ila labda kuna wakristo wengi kwenye hiyo taasisi uta fanyaje?
Hamuwezi kulingana kila kitu,ndio maana hata kwenye ligi ya mpira,mkilingana points wanaenda kuangalia goal difference,mkilingana wanaangalia nani Wana magoli mengi ya kufunga,kama Bado mmelingana,wanakuja hadi red cards nani anazo nyingi,yellow cards,fouls NK!Mpaka mshindi atapatikana!Mkilingana kila kitu zamani Hadi shilingi Ilikuwa inarushwa!
So kumchagua dini A na kumuacha dini B kisa tayari una watu wa dini B wengi,sio sawa!
Hapo mnaweza kuwapa mtihani mwingine hata wa uelewa wa mambo mengine ya kijamii!Lazima more competent atapatikana!
 
Nani aliandika ,au kuuliza kabila au dini ya mtu ,hugo ni muasi rebel. Muasisi na Baba Mwl. J K.Nyerere alionya. Tabia za kuligawa taifa.kulizana idini na kabila. Vipi sio wakilisto au au waislamu.vipi tusiona na kabila kiswahili.
.
 
Watu Tata
 
Mleta mada unataka kutuaminisha kuwa ulichaguliwa kujiunga UDSM kwa sababu wewe ni Mkinga? Wagogo, wamakonge, wanyiha, wahehe, wadigo n.k. hawakuwepo chuoni hapo kwa sababu ya kabila zao? Ilitokea lini hiyo ili nasi tujiridhishe kuwa tuhuma zako ni za kweli?
Unaju kila jamii inavipa vitu fulani umuhimu zaid wako wanaona ng,ombe ni kila kitu, wengine wanafikiri kuozesha hata vitoto vodogo, wengine wanaipa elimu umuhimu nk. Sasa anafikiri kuoa na kuolewa umpe nini zaidi kumhamasisha ajue maana ya elimu. Na hufanyi hivyo kwa kumwondolea haki mwenye uhijitaji na uwezo wa kusoma.
 
Uko vizuri sana mkuu Ni nchi kama Tanganiza tu ndio kuna watu wana mawazo kama yale ya mchongameno kuhusu suala la dini na kabila, fomu nyingi tunajaza Online hilo suala lipo nchi kibao zinataka kujua taarifa za dini ya muombaji, Na utashangaa wanaohoji kutokuwepo kwa suala hili ni Wakiristo tu
Kwa hiyo afisa utumishi akijua dini yako anafanya nini nayo au anakupangia ratiba ya ibada.
Chukua mfano afisaelimu atataka kujua mwalimu wake ana elimu gani, masoma gani hata umri wake hivi vitamsaidia kumpangia mwalimu kazi.
Jiulze akijua dini yake itamsaidia nini au tu ajue kama anakula kitimoto au la kwa kuwa anawanunulia nyama walimu wake. Hilo swali ni hopless na ndiyo maana utakuta watu wanalalamika oh sijui dini fulani inapendelewa. Sasa kama yutafuata misingi hiyo si ndio malalamiko yatazidi hata dini zitaanza kuhesaniana madhehebu, mbona wasabato hawapo, wasunni wachache nk. This is nonsense, period!
 
Suala la Marital status nimeoa/umeolewa pia linaulizwa je lina umuhimu gani kwenye utumishi? mbona hukujenga hoja yako hapa?
Ni jambo la kawaida tu kujuwa una sifa za mtumishi au mtu yoyote hasa ukija kwenye mahitajio yao ya kila siku. Acheni woga wenu
 
Mimi ni Mkinga na siogopi watu wakinitania pale Kariakoo au kwenye ofisi za chama chetu cha CCM

Mamlaka inataka kujua kanzi data za dini, Kabila na Jinsia ili iweze kufanya usawa wa mgawanyo wa keki ya Taifa, Kila mtu ashirikishwe Katika ugawaji wa rasilimali za Taifa

Tutajuaje tunatakiwa kujenga vyoo vya kiume vingapi maofisini bila kuwa na idadi kamili

Tutajuaje mwezi Desemba wachaga wanavyoenda Kilimanjaro kwa kiasi gani kazi za serikali zinasimama au kupwaya

Wale wazee waliosoma Udsm enzi hizo watakumbuka chuo kilijaa watu wa Bukoba, Mbeya na Kilimanjaro.

Darasa zima pale Udsm unakaa na wanyakyusa na wahaya tu,Je makabila mengine yalikuwa na shida gani? Kwanini idadi yao kujiunga na chuo ilikuwa ndogo

Leo hii ukifika Udsm kimekuwa chuo kidogo chenye kubeba usawa wa watoto nchi nzima

Tatizo hilo sasa limeisha baada ya Serikali ya Jakaya Kikwete kuanzia mwaka 2006 kuja na mapendekezo maalumu ya Big Results Now yaliyoimarisha shule za kata na kuajiri walimu wa kutosha kila mwaka kupelekwa kwenye mikoa iliyo nyuma kielimu

kuanzia mtu wa kwanza kwenye list jina linaanza na Mwa......., Mwakitafuna, Mwakalele, Mwakifuna, Mwanjabala, Mimi Gussie wakati nimeenda kufanya utafiti pale Udsm na kusoma soma majarida yao nikajiuliza hivi huko Undergraduate kupo vipi? Maana nilikuwa Mkinga peke yangu tu na Jamaa mmoja toka Tabora wote waliobaki ni wachaga, wanyakyusa na wahaya

Walimu asilimia 50% walikuwa wahaya hasa wale maprofesa

Tatizo la dini bado halijapatiwa ufumbuzi bado hasa Katika baadhi ya mikoa ya Pwani kama lindi, Mtwara na Pwani, Kwanini bado wana muamko mdogo sana wa elimu na ushirikishwaji wao ni mdogo sana

Ni dhahiri shahiri kuna baadhi ya makabila yalipiga hatua kutokana na mkoloni aliyetutawala na rasilimali alizozipata toka mikoa hiyo

Ni muda muafaka kupata takwimu hizi za mgawanyo wa wafanyakazi serikalini

Kama wewe ni mtanzania unaogopa kwanini Kabila lako au Dini yako

Haya mambo mnapewa nafasi hamtaki mwisho wa siku mtaanza kusema ccm na serikali ina upendeleo kumbe ni baadhi ya watu kuficha takwimu zao

Mimi ni Mkinga na sijazaliwa ukingani lakini siogopi mbele za watu wakinitania Mkinga, Wewe unaogopa kitu gani kutaja Jinsia yako, Dini yako na Kabila lako?
Utakuwa na stress kali sana sio bure.yaani Tanzania ya sasa ndio ya kuulizana makabila akitaka hizo information si wangezipata utumishi.Aibu kwa Taifa.
 
Suala la Marital status nimeoa/umeolewa pia linaulizwa je lina umuhimu gani kwenye utumishi? mbona hukujenga hoja yako hapa?
Ni jambo la kawaida tu kujuwa una sifa za mtumishi au mtu yoyote hasa ukija kwenye mahitajio yao ya kila siku. Acheni woga wenu
Marital status ina umhimu sana katika kupanga kazi mfano kumhamisha mtumishi. Mtu aliye na familia ni tofauti na single katika kutelkeleza majukumu.
 
Suala la Marital status nimeoa/umeolewa pia linaulizwa je lina umuhimu gani kwenye utumishi? mbona hukujenga hoja yako hapa?
Ni jambo la kawaida tu kujuwa una sifa za mtumishi au mtu yoyote hasa ukija kwenye mahitajio yao ya kila siku. Acheni woga wenu
Umri, hali ya ndoa, makazi, nyumba nk vina umuhimu kitakwimu.
Sema tu dini na kabila vina umuhimu katika kazi. Kitu gani mwajiri atanugaika nacho kuhusiana na dini ya mtu au kabila lake sema tutakuelewa.
 
Suala la Marital status nimeoa/umeolewa pia linaulizwa je lina umuhimu gani kwenye utumishi? mbona hukujenga hoja yako hapa?
Ni jambo la kawaida tu kujuwa una sifa za mtumishi au mtu yoyote hasa ukija kwenye mahitajio yao ya kila siku. Acheni woga wenu
Ujue mtumishi mwenye ndoa akilipwa mafao ya uhamisho ni pamoja na mwenza na watoto wanne.
 
Rwanda wamefuta kabisa ukabila na Dini kuonekana popote kwenye fomu yoyote ya serikali huku sisi ndio kwanza tunauanza

Rwanda nchi ndogo imetupita kwa hili
 
Nimesoma bandiko mwanzo mwisho, sijaona sehemu umesema umuhimu wa dini na kabila zaidi ya kujitapa ww mkinga na huogopi kusema kabila lako (sisi tunataka utwambia umuhimu wa dini na kabila )
 
Mimi ni Mkinga na siogopi watu wakinitania pale Kariakoo au kwenye ofisi za chama chetu cha CCM

Mamlaka inataka kujua kanzi data za dini, Kabila na Jinsia ili iweze kufanya usawa wa mgawanyo wa keki ya Taifa, Kila mtu ashirikishwe Katika ugawaji wa rasilimali za Taifa

Tutajuaje tunatakiwa kujenga vyoo vya kiume vingapi maofisini bila kuwa na idadi kamili

Tutajuaje mwezi Desemba wachaga wanavyoenda Kilimanjaro kwa kiasi gani kazi za serikali zinasimama au kupwaya

Wale wazee waliosoma Udsm enzi hizo watakumbuka chuo kilijaa watu wa Bukoba, Mbeya na Kilimanjaro.

Darasa zima pale Udsm unakaa na wanyakyusa na wahaya tu,Je makabila mengine yalikuwa na shida gani? Kwanini idadi yao kujiunga na chuo ilikuwa ndogo

Leo hii ukifika Udsm kimekuwa chuo kidogo chenye kubeba usawa wa watoto nchi nzima

Tatizo hilo sasa limeisha baada ya Serikali ya Jakaya Kikwete kuanzia mwaka 2006 kuja na mapendekezo maalumu ya Big Results Now yaliyoimarisha shule za kata na kuajiri walimu wa kutosha kila mwaka kupelekwa kwenye mikoa iliyo nyuma kielimu

kuanzia mtu wa kwanza kwenye list jina linaanza na Mwa......., Mwakitafuna, Mwakalele, Mwakifuna, Mwanjabala, Mimi Gussie wakati nimeenda kufanya utafiti pale Udsm na kusoma soma majarida yao nikajiuliza hivi huko Undergraduate kupo vipi? Maana nilikuwa Mkinga peke yangu tu na Jamaa mmoja toka Tabora wote waliobaki ni wachaga, wanyakyusa na wahaya

Walimu asilimia 50% walikuwa wahaya hasa wale maprofesa

Tatizo la dini bado halijapatiwa ufumbuzi bado hasa Katika baadhi ya mikoa ya Pwani kama lindi, Mtwara na Pwani, Kwanini bado wana muamko mdogo sana wa elimu na ushirikishwaji wao ni mdogo sana

Ni dhahiri shahiri kuna baadhi ya makabila yalipiga hatua kutokana na mkoloni aliyetutawala na rasilimali alizozipata toka mikoa hiyo

Ni muda muafaka kupata takwimu hizi za mgawanyo wa wafanyakazi serikalini

Kama wewe ni mtanzania unaogopa kwanini Kabila lako au Dini yako

Haya mambo mnapewa nafasi hamtaki mwisho wa siku mtaanza kusema ccm na serikali ina upendeleo kumbe ni baadhi ya watu kuficha takwimu zao

Mimi ni Mkinga na sijazaliwa ukingani lakini siogopi mbele za watu wakinitania Mkinga, Wewe unaogopa kitu gani kutaja Jinsia yako, Dini yako na Kabila lako?
Tangu Tanzania ipate uhuru - viongozi wamejitahidi kuiepusha nchi katika demokrasia kwa misingi ya dini. Dini fulani inaweza kumkataa mgombea wa dini nyingine kwa kutumia takwimu za uwingi wao. ,Hii ni hatari kwa amani na utulivu tulionao.
 
Dini na Kabila havina msaada ktk dunia ya leo.
Serikali haina dini wala kabila..
 
Rwanda wamefuta kabisa ukabila na Dini kuonekana popote kwenye fomu yoyote ya serikali huku sisi ndio kwanza tunauanza

Rwanda nchi ndogo imetupita kwa hili
Rwanda wamejifunza kutokana na makosa yao. 1994 ktk vita vya kimbari vitambulisho vilitumika kujua nani mhutu nani mtusi, kikionesha ww ni mtusi unakula panga.
Nway inaonekana hatupendi kujifunza kutokana na makosa ya wenzetu tunataka tujifunze kwa makosa yetu wenyewe.
 
Suala la Marital status nimeoa/umeolewa pia linaulizwa je lina umuhimu gani kwenye utumishi? mbona hukujenga hoja yako hapa?
Ni jambo la kawaida tu kujuwa una sifa za mtumishi au mtu yoyote hasa ukija kwenye mahitajio yao ya kila siku. Acheni woga wenu
Marital status ktk ajira inatumika ktk bima ya afya(huwezi kujaza single ktk form then ukapewa kadi ya bima kwa ajili ya mke),
2nd inatumika kutambua kua una mrithi wako incase uki rest in peace.
 
Back
Top Bottom