Kwanini unatakiwa kuacha ulevi wa pombe? Hizi ni baadhi ya faida

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,726
10,020
1) Utakusaidia sana uhifadhi wa pesa kwa matumizi mengine
Umewahi kujiuliza ni kiasi gani cha fedha unatumia kwa unywaji pombe pekee? Sasa jumlisha kiasi chote kwa miezi yote ambayo ungetumia kunywea ungekuwa na kiasi gani. Muda mwingine hata kama kuna kiasi maalum uliweza unaweza jikuta umetumia zaidi ya malengo kwa sababu zisizo za msingi kabisa yote ni kutokana na kuendeshwa na pembe kwa wakati huo.

2) Utakuwa na nguvu zaidi
Kumbuka huwa unajisikiaje asubuhi unapoamka baada ya unywaji mzito uliofanyika usiku wake? Hatuongelei bado kuhusu madhara hangover (bado) lakini vipi utaweza kuimudu siku ukifananisha na wakati ambako hukulewa?. Kama utaweza kuamka kwa wakati na kujikontrol mwili wako, utagundua kuwa mwili utakuwa mzito sana mwanzoni na nguvu zitaanza kurudi kadri utakavyozidi kuuhangaisha.

3) Hutapata hangover tena kutokana na ulevi!
Tuwe wakweli hakuna mtu anaependa hangover, huku kichwa chako kikipata dhoruba ya kichwa kuuma na kizunguzungu kutokana na vyupa ulivyopata kabla. Hebu fikiria utakuwa unajisikia poa namna gani pindi unapoona umeondokana na adha hii? Unaamka ukiwa safi, tayari kwa uzalishaji mali kwa siku hiyo na si kuanza tena kutafuta wapi nitapata painkillers.

4) Hakuna tena kujihisi mkosefu mudawote
Pale marafik na wanafamilia wanapokushauri kila mara na kukusema juu ya ulevi wako na kwa maana hiyo kila utakapo jaribu kunywa nafsi yako lazima itakuwa inakusuta kila unapochukua fundo.

5) Hautakuwa tena mtu wa kuomba msamaha kila baada ya usiku unapolewa!​

Fikiria vitu vyote vya aibu ulivyokuwa unafanya baada ya kulewa; kupigana hovyo, matusi na kelele za kila namna, kuitaita majina ya wqtu hovyo bila hata sababu na vitendo vingine vya aibu visivyofaa kwa jamii. Hutakiwi kuwa hivyo na acha visingizio.

6) Kujiamini kutaongezeka karadufu
Pale utakapoona umeweza kuacha ulevi na uwezo wa kuendelea kuwa hivyo upo unaweza kujiona wewe mwingine kabisa na tofauti na yule uliyezoea kuwa hata mbele ya watu huwezi simama ukaongea vya maana na watu kukutilia umakini.

Utajihisi paka kawa simba
Kwa sababu kuacha pombe si lelemama.

7) Utakuwa mtu wa malengo na baadae angavu
Hii inaleta kujiamini zaidi, furaha na raha ya kuishi maisha yasiyokufanya upoteze dira na malengo ya maisha tangu utakapoacha mizigo yote ya ulevi wa

8) Ini lako litakushukuru sana kwa hatua hiyo
Pombe inaleta shida sana kwenye ini, mbaya zaidi unywaji uliopindukia unafanya ini lielemewe na kazi na kujisababishia matatizo kadhaa ya kiafya.

9) Ngozi itang'aa
Ulevi wa pombe unasababisha upotevu wa maji mwilini nikimaanisha pamoja na unyevu katika ngozi na kufanya ngozi ifubae na hata kujikunja tofauti kabisa na uhalisia wa umri wa mlevi. Pitia pia hapa......positive changes in your skin and face.

10) Ubongo utapona kutokana na madhara
Unywaji pombe uliozidi kiasi , sio tu utaifanyisha ini kazi kupita kiasi bali mwili mzima. Ubongo wako unawajibika kwa kila kitendo kutokana na sababu wajibu wake kiutendaji wa kuwajibisha mwili nini cha kufanya na kwa wakati gani.

Ulevi uliokithiri unaumiza eneo katika ubongo na ndio maana hujikuta umefanya kitu ambacho hukutegemea kufanya kabisa. Kuachana na ulevi wa pombe kunaupa wakati mzuri ubongo kujirudi taratibu katika utendaji wake unaostahili na afya.
 
afadhari umeongelea ulevi! nimeshtuka mwanzon nikidhan unaongelea kunywa pombe. eti niulize tu, hivi ambao hawanywi pombe huwa mbadala wao ni nini
 
Michongo mingi ya hela tunaipata tukiwa na wadau tukipata kilaji, sasa Unasemaje tuache pombe bwashee
 
kinachochangia ulevi sana ni kampani..
kampani hunichochea sana niwe mlevi na kampani ambayo haikwepeki ya staff na boss mwenyewe.kila dili unaalikwa bar dmmmnn

Acha tu sio wewe tu. Watu wanadhani hatupendi kuacha tatzo vipato vya wengi viko connected kwenye bar / pombe. Mimi kazi na ma deal mengi ndio nayapatia huko.

Hata kiwanja changu goba nliwahi pata kwenye bar / pombe na sikulipa hela yeyote ya dalali. Mmiliki nlikua niko nae tunapiga vyombo.
 
Acha tu sio wewe tu. Watu wanadhani hatupendi kuacha tatzo vipato vya wengi viko connected kwenye bar / pombe. Mimi kazi na ma deal mengi ndio nayapatia huko.

Hata kiwanja changu goba nliwahi pata kwenye bar / pombe na sikulipa hela yeyote ya dalali. Mmiliki nlikua niko nae tunapiga vyombo.
noma sana
 
Back
Top Bottom