Kwanini unamuumiza mtu unaempenda (mpenzi) au yeyote yule mwenye kushare hisia na wewe?

Umewahi kuumiza/ kuumizwa katika mahusiano yako?

  • Ndio

  • Hapana

  • Sijawahi kuwa kwenye mahusiano


Results are only viewable after voting.

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,726
10,019
Kwa nini unamuumiza mtu unaempenda?
images.jpeg


Ni kawaida kujisikia vibaya unapo muumiza mtu mnayependana hasa kama alikuamini sana.

Kuna sababu mbalimbali nyuma ya maumivu kwenye mahusiano yako. Lakini matendo yako pia yanaweza kumhathiri mtu unaempenda kwa kiasi kikubwa.

-Kuna muda, kumlinda mtu kupita kiasi kuna weza kumuumiza iwe mpenzi wako au mtu yeyote yule wa karibu nawe. Unaweza kujikuta umemuumiza kihisia mtu kwa kumuwekea ulinzi sana au vikwazo vingi kwa kufikiri kwa control uliyoweka juu ya mpenzi wako anaweza kuwa salama kwako na kwake au naweza sema 'suluhu ya matatizo yenu'. Lakini ngoja niseme MAPENZI yana mipaka.

-Kama huwezi kuheshimu mipaka ya mpenzi wako kuna nafasi kubwa sana ya kumuumiza kihisia.
Tabia zako zinaweza kusababisha maumivu kwa mwenzi wako. Kama tabia yako sababishwa na huzuni, wasiwasi, hofu, kutomwamini mtu, na huzuni nakwambia bila kujizuia hali hiyo inaweza kusababisha maumivu kwa mtu umpendaye.

Kila mahusiano yana kupanda na kushuka. Unapitia katika wakati mgumu kwenye mahusiano yako, badala ya kuamua kuachana, unaweza kujaribu kwa kuangalia njia gani zinaweza kutengeneza upya mahali palipo bomoka ndani ya penzi lenu.


OMBA MSAMAHA KWA MPENZI WAKO KWA KUMUUMIZA

Kuomba msamaha baada ya kumuumiza mtu umpendaye ni ngumu sana muda mwingine. Hata hivyo unatamani mahusiano yenu yarudi kwenye afya yake kama mwanzo. Basi unaweza kujaribu njia hizi kuomba msamaha kwa mpenzi wako.

1. MSAMAHA KWA KUONANA MUBASHARA: Hii ni njia bora kabisa ya kuombana msamaha kwa wapenzi. Pamoja na kwamba ni ngumu, lakini inadaidia sana kuweka sawa mambo kwa haraka. Ni njia inayokuwezesha kujuta na kukubali makosa kwamba ulichofanya hakikuwa kizuri, useme samahani na uahidi kuanzisha jani jipya la penzi. Na omba kumfanyia mpenzi wako kitu ambacho huwa kinamfurahisha mara kwa mara.
images (2).jpeg


2. MSAMAHA KWA MAANDISHI: Unaweza pia kuomba msamaha kwa mpenzi uliyemuumiza kwa kumwandikia meseji, email au hata barua kuomba yale yaliyotokea yaishe na kuanza upya.
images (4).jpeg


3. MSAMAHA KWA NJIA YA LUGHA VITENDO: Unapogundua umemuumiza mpenzi wako au yeyote umpendaye, njia nyingine maalum ya kumwomba akusamehe unaweza mnunulia zawadi/ zawadi ndogo kama maua, snacks anazopendelea, au unaweza mtoa out na kumpeleka mahali huku ukihakikisha anarudisha furaha juu yako. Unapofanya hayo hakikisha unamuachia angalau hata ki-note chenye maneno mazuri na matamu ukiambatanisha maombi ya akusamehe ndani yake. Pia unaweza kufanya vitu vingine kama kumsaidia hata kuandaa chakula (ONYO: hii nikwa wanaojua kupika tu!)
images (3).jpeg


Kuwa katika mahusiano ya kimapenzi ni lazima kuumizwa?

Mpaka tena siku nyingine.
 
Swala la wasiwasi na hofu naona linaponza zaidi kwa mwenye wasiwasi maana unakua hukai kwa amani bure tu kwa vitu usivyoweza kuvizuia

Tena mwingine ukiwa na wasiwasi nae anaamua kufanya kweli kabisa ani ili isiwe lawama za bure tu
 
Back
Top Bottom