Kwanini umzuie mke wako kuwa na simu ya mkononi wakati wewe unayo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini umzuie mke wako kuwa na simu ya mkononi wakati wewe unayo?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by GM7, Aug 9, 2009.

 1. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Waheshimiwa sana wanaJF,
  Nawauliza hasa wanaume, kwanini usimruhusu mke wako au mpenzi wako wa kike kuwa na simu ya mkononi wakati wewe unayo?

  Katika tembeatembea nilikumkuta dada mmoja ambaye tunafahamiana, ana mtoto wake mmoja na ana mume. Katika maongezi mbalimbali nikamwambia siku hizi karibu mtu ana simu ya mkononi sasa kwa nini wewe huna simu kwa ajili ya mawasiliano wakati simu nyingine zinauzwa mpaka sh.10,000 tu? Akasema "ninue simu baba J atanielewa? Si atafikiri nawasiliana na wanaume wengine?"

  Siku nyingine akaja mama mmoja kununua vocha kwangu. Katika maongezi naye akasema "mume wangu hajui kama nina simu ya mkononi, maana akijui tu nyumbani patakuwa hapatoshi. Yaani hapendi kabisa niwe na simu ya mkononi ila yeye tu awe anayo"

  Swali kwa wanaume: Kwanini wanaume hawapendi wake zao kuwa na simu? Kuna tatizo gani mke wako kuwa na simu wakati wewe unayo?

  Swali kwa wanawake:Kwa nini waume zenu hawawaamini mkiwa na simu? Mna matatizo gani yanayosababisha msiaminiwe kuhusu hili suala?

  Karibu tuendelee kuchangia mada.
   
 2. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hayo yapoa sana, au anakwambia utatumia ya kwangu kutuma msg na kupitga,
  Haoa ni wanaume wasiojiamini wala kuamini wake zao na wana wivu kupita kiasi.
  Halafu wana mambo yao wanafanya nje, kwa hiyo anaogopa ukiwa na simu unaweza ukapata hata mtu wa kukutumia msg kukuambia mume wako yuko na fulani siku hizi au muda huu yuko mahali fulani,
  wanaume wengi wanaonyima wake zao wasiwe na simu ni ambao utulivu 0 siyo waaminifu
   
 3. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Egoism!
   
 4. M

  Msindima JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Namshukru sana alieleta post hii maana jumamosi nilikutana dada mmoja nikamwuliza bado hujanunua simu akaniambia naogopa nikiwa na simu baba fulani hatutaelewana,nikamwuliza kwa nini msielewane yaani simu tu jamani akaniambia ndo hivyo,nikajaribu kufikiri kwa nini hataki kumnunulia mke wake simu?kuna kitu gani kinaendelea? kwa kweli sikupata majibu,labda hapa nitapata majibu,nakushukuru ulieanzisha hii mada.
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Wivu tu ..hivi..nani ana wivu zaidi?? Mwanamme an mwanamke??
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  Hao wanawake wote waliofanyiwa hivyo wana tabia mbaya

  sana .

  Mabwana zao washastukia hilo ndo maana wamewapiga stop

  kununua simu!

  Hata mimi ningekuwa na mke wa hivyo ningemmeza

  nikimwona na simu!

  Sasa ona huyo mwingine, amekatazwa na bwanaake, bado

  ametafuta ingine kwa siri na anaitumia pasipo bwanake

  kujua! kweli hiyo inaswihi?

  Hakuna wivu wala nini, ni wanawake hao ni wahuni too

  much!

  We unataka kuwasiliana na nani na huo usiri wako? Ni kwa

  tija ya familia au ni kuwabania pua akina Fidel180?

  Sh*iiit!
   
 7. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Wanawake wasio na simu wakati waume zao wanazo nafikiri wana mtindio wa ubongo, wewe inakuwaje huaminiki kwa mumeo? Au wewe mwanaume inakuwaje humwamini mkeo? Hayo maisha na mbagumu sana watu inaibidi kukemea tabia fulani kabla haijaota mizizi, ukiona mkeo anaenda kusiko piga kelele aache. Hata asipokuwa na simu kuna vibanda ataenda atapiga wakati hupo atafanya yote anayotaka then wewe unaonekana mjinga.

  heheheheh
   
 8. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
   
 9. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hii naona ni mojawapo ya sababu.
   
 10. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  mmmm hii kali nilkuwa sijasikia wala kufikiria kuna mijiume ya ain hii... simu hata wewe mwnenyewe ukitaka kuwasiliana na mkeo jamani itakuwaje hapo? kama kuna dharura je? utaanza kupiga simu kwa jirani? wanaume wakware ndio wenye hii tabia wasije wakshikwa. mmm nayo teknology ndio mwisho mama anapata simu na anaiweka permanently on silent mode utajuaje?????
   
 11. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #11
  Aug 18, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Halafu wengine waliobahatika kuwa na simu basi kila siku mume/mke anakagua simu ya mwenzake kuona nani kapiga simu au kutuma meseji. Halafu tena kuna wanaume wengine ukiangalia phonebook yake utakuta majina ya wanaume tu ili mkewe akiangalia asiwe na wasiwasi.
  Kwa mfano mtu anaitwa Juliana lakini kwenye simu anaandika Julius. Kweli siku hizi uaminifu haupo.
   
 12. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #12
  Aug 18, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 642
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  KWa staili hiyo hata maendeleo yako nyumbani yatakuwa Magumu. Je ingekuwa vipi kama ungelipata kazi zambia mshahara milioni nne , kwa mwezi na huendi na mkeo ,kurudi nyumbani kila baada ya miezi mitatu contract duration ,2 years?
  Wivu kupita kiasi ni hatari kwa maisha yako na kwa maendeleo ya familia pia .
  THANKS JF MEMBERS FOR EDUCATING THE COMMUNITY
   
Loading...