Kabende Msakila
JF-Expert Member
- Oct 7, 2020
- 1,383
- 1,248
WanaJF, Salaam!
Nimefuatilia kwa takriban miaka sita (6) hivi humu kwenye jamvi huru la siasa. Ukijitokeza kusifia, kuunga mkono jitihada za Serikali inapofanya jambo zuri i.e Ujenzi wa vivuko Busisi - Sengerema, ujenzi wa barabara za lami, ujenzi wa vituo vya afya, uteuzi wa wapinzani, maridhiano ya kitaifa Zanzibar nk nk.
Kwa hayo na mengine mengi ukitokea hadharani na kuyasifia ukweli ni kwamba hawa jamaa wa CDM wanaudhika kweli - wanajaa gesi na hapo unashushiwa dhihaka kibao kama:
(i). Lumumba buku saba - sasa Je, wao wanaposifia Tundu Lissu au Mbowe huwa mmepewa Ufipa kiloba?
(ii). Weka namba ya simu chini ili uteuliwe (as if Serikali ina nafasi ya kuteua kila mtanzania mwenye hisia na mawazo chanya) - Je, ninyi mnaposifia CHADEMA huwa mnafanya hivyo ili chama cha Mbowe kiwateue?
(iii). Wauaji, watekaji na wakandamizaji wa haki za binadamu - hivi huwa mnasahau kwamba ukandamizaji mmeuasisi huko CHADEMA - CCM tumebadili wenyeviti wa taifa mara kadhaa, CHADEMA mmebadili mara ngapi? Mmeshajiuliza kwa nini Silinde, Waitara, Katambi, Dkt Kaburou, Zitto, Dkt. Slaa, Dkt Mashinji, Lijualikali na wengine wengi waliamua kuwaacha?
Nihitimishe kwa kusema kwamba si kwamba Paskali Mayyala, Msakila Kabende nk kuunga mkono jitihada za Serikali ni kutaka teuzi "NO". Things are always clear kwamba Serikali ya JPM iko makini sehemu zote na imeweza kujibu maswali mengi ya upinzani kama dhana ya ufisadi, uwajibikaji, matumizi ya fedha za umma nk
Asubuhi njema wanachadema, ACT-Wazalendo, CUF, NLD, UDP, NCCR nk.
Msakila M Kabende
Kigoma
Tanzania