Kwanini ukerwe na kaulimbiu za chama kinacho kuzidi kete?

BUBERWA D.

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
2,293
1,170
Kauli mbiu (slogan) ni tungo fupi zenye falsafa ndani yakeambazo hutumiwa kuwasilisha au kujuza kwa urahisi na ufasaha falsafa inayotoamsukumo wa mtu au kikundi cha watu kufanya jambo fulani aidha la muda mfupi aumuda mrefu kwa manufaa ya wahusika na wafuasi wao.Bila kuwachosha,tujiulize kwanini watu wanakerwa na kaulimbiuza watu wengi wanapokuwa wanaendesha shughuli zao za siasa katika vyama vyasiasa. Kimsingi ni kunyima haki ya msingi ya watu kufanya shughuli zao.Kuna kaulimbiu mbili nitapenda kuzitumia…"KUJIVUA GAMBA naVUA GAMBA VAA GWANDA".

CCM kilikuja na "KUVUA GAMBA" ambayo kutokana na hotubaya muasisi wa kaulimbiu hiyo ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho February 2011akiwa Dodoma ilikuwa inatokana na kukiri kwamba wanachama wake wametopea kwenyewizi, rushwa, ufisadi na kila aina ya kutokuwa na maadili na hivyo wanahitajikujisahihisha. Lilikuwa lengo zuri japo kuna malengo yasiyotekelezeka hasatatizo linapokuwa limefikia "a point of no return".

Na hili tumelishuhudiamaana mwaka huohuo November wakiwa hapohapo Dodoma waliweweseka walipotakiwa kuitetea kauli mbiu hiyo na hivyo kuonekana kuwa walikurupuka na hivyowasingeweza kuisimamia falsafa yake katika mazingira ambayo yanaonyeshawalioiasisi pengine nao walitakiwa wavue au ndiyo magamba yenyewe.
Wapinzani wao sasa wanaonekana wamekuja na VUA GAMBA VAAGWANDA.

Hii ni falsafa kubwa. Inatuonyesha kuwa huwezi kujisafisha tope zilizokuenea mwilini ukiwa ndani ya tope hilohilo. Unatakiwa uondoke ndani ya topehilo ili ujisafishe au wengine wakusaidie kukusafisha. Hii slogani kwa chama inasaidiakuwashawishi walio nje ya chama wajiunge na chama hicho na waliondani waone na kujivunia kuwa wakosehemusalama na safi. Hii inasaidia kuwapiku vyama vingine kwa ajili yakujiimarisha. Sasa unachukia nini watu wanapoimarisha chama chao? Chamachochote kinachotaka kukua lazima kiwe na mikakati ya kupata wafuasi ambao ndiomtaji wa chama.

Hata "KUJIVUA GAMBA"lengo lilikuwa hilohilo ila wameshindwa.Sasa yako yakikushinda vipi umchukie anayefanya mambo yake vizuri?
Kuna hoja kwamba hao wanaoklimbilia kuvaa gwanda eti si waovuwalewale? Hii inatumiwa na wale walioshindwa kuwavutia watu aidha wabaki auwajiunge na chama chao. Ninachojua ni kwamba hakuna mtu anaezaliwa akiwa muadilifuau muovu katika maswala ya kuiongoza na kuisimamia jamii yake, isipokuwa mfumowa kijamii ndio unaoumba au kubomoa misingi bora ya kujiongoza na kujileteamafanikio ya nyanja zote katika jamii.Watu leo tunaowaona kuwa si waadilifu, enzi za MwalimuNyerere walionekana kuwa waadilifu kutoka na mfumo ulioelekeza bila mzaha,mfumowenye miiko thabiti na usimamizi thabiti.

Baada ya kuondoa na kutupilia mbali maadiliwale walioonekana kuwa waadilifu leo ndio wanaotumaliza. Huwezi amini kingungewa miaka ya sitini mpaka themanini akikutana na kingunge wa leo hawawezikutambuana maana ni watu wawili tofauti kabisa.
Hatuwezi fanya uwenda wazimu huu, kwamba kwakuwa mabehewa yareli ya kati yamezoea kutiririka mpaka kigoma, basi hata tukiondo reli mabehewahayo yatakwenda kigoma.

Huo ni wendawazimu mabehewa hayo yatagongana hapohapostesheni na mambo yote yatakwama.Na hayo ndio yanayotokea CCM halafuwananung'unika wakati wenyewe ndiyo waliong'oa reli hiyo miaka ya tisini katikakile walichoita "Zanzibar Resolution". Sasa watanzaniawamegutuka wanaona wakipitia huko wataishia kugongana na kusambaratika kamailivyo sasa ndiyo maana wanavaa gwanda kujaribu njia nyingine. Hapa mabehewa niviongozi na jamii nzima ilihali reli ni miiko, maadili sheria, kanuni nataratibu zetu.
Kwa hiyo mtu anaweza toka kwenye magamba akiwa mchafu nakuvaa gwanda akawa msafi. Kwakuwa yeye ni behewa.

Sasa itategemea amekuta religani. Reli imara au reli legelege iliyong'olewang'olewa? Wazee wa gwanda nimatumaini yangu kuwa reli yenu ni imara mabehewa yatakwenda tu. Na muwe makinikuzidi kujiimarisha.aliye shindwa akianza kulalamika na majungu wewe unaongezamwendo. Kunapokuwa na tatizo tutumie taratibu zetu kulitatua tusikaribishedhambi ileile inayowatafuna magamba. Na tujue kuwa gwanda si gumu kama gambatunahitaji kulilinda na kulienzi kwa umakini mkubwa.
Nakaribisha tafakuri…………
 
Back
Top Bottom