Kwanini UKAWA wanazuiwa na polisi kufanya mikutano yao?

SOCIOLOGISTTZ

JF-Expert Member
Jun 16, 2013
2,606
1,225
Nimesikiliza taarifa ya habari kupitia kituo cha ITV leo saa mbili, kuwa jeshi la polisi limezuia mikutano ya UKAWA ndani ya mkoa wa Kigoma kwa muda wa siku tatu sasa. Anayejua nini kilichopo nyuma ya pazia atujuze tafadhali.
 
Mhabarishaji

JF-Expert Member
Oct 5, 2010
1,005
2,000
NCCR ina sauti kubwa sana Mkoa wa Kigoma, ina wabunge Kigoma, Kasulu, na Kibondo. Manispaa ya Kigoma-Ujiji, nayo Meya wake ni wa CHADEMA. CUF nayo si haba. Combination ya vyama hivi ni sauti yenye nguvu kubwa sana kwa wakazi wa Mkoa wa Kigoma, ambao wanapokea haraka ajenda za Upinzani kuliko za CCM. Nguvu ya sauti hiyo imeitisha sana CCM, kiasi kwamba wameona kete pekee ya kupambana na UKAWA, ni kutumia tawi lao la POLICCM.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
NCCR ina sauti kubwa sana Mkoa wa Kigoma, ina wabunge Kigoma, Kasulu, na Kibondo. Manispaa ya Kigoma-Ujiji, nayo Meya wake ni wa CHADEMA. CUF nayo si haba. Combination ya vyama hivi ni sauti yenye nguvu kubwa sana kwa wakazi wa Mkoa wa Kigoma, ambao wanapokea haraka ajenda za Upinzani kuliko za CCM. Nguvu ya sauti hiyo imeitisha sana CCM, kiasi kwamba wameona kete pekee ya kupambana na UKAWA, ni kutumia tawi lao la POLICCM.

Jamani huu ndiyo ukweli wenyewe. Nashauri mkutano huo ufanyike hata kama ni baada ya wiki, na upewe publicity ya kutosha ikihusisha media zote, mpaka TBC! ili wakati wao wanaposhindwa kutenda haki, wapate tu fursa ya kujionea jinsi wanachi wanavyosapoti mabadiliko, huku wao wakiwa kwenye kundi la wasaliti wa wananchi hao!
 
ihs

Member
Jul 24, 2012
93
0
Nimesikiliza taarifa ya habari kupitia kituo cha ITV leo saa mbili, kuwa jeshi la polisi limezuia mikutano ya UKAWA ndani ya mkoa wa Kigoma kwa muda wa siku tatu sasa. Anayejua nini kilichopo nyuma ya pazia atujuze tafadhali.

Hapa hatuhitaji kujiuliza ni kitu gani ambacho kimetokea, utawala ulioko madarakani umejisahau sana kiasi cha kuingiza vyombo vya ulinzi katika siasa zao na maslahi yao. Hili halina kificho kwa watu ambao wameona mwanga kidogo, liko wazi sana. Ni jambo baya sana kukandamiza nguvu ya umma, freedom of speech ambayo imeelezwa na kutolewa provision kwenye katiba kwa maslahi ya wa tu wachache.

Ila inabidi chama tawala kiweke angalizo tu, what goes around comes around!! Chama kingine kikija kuchukua dola kitaweza kufanya hivo hivo, na chama cha upinzani ambacho kwasasa ni chama tawala kitabidi kikae kimyaaa bila kua na authority ya kujitetea kwa sababu wameshindwa kufanya sasa!!

Lazima ifikie muda tukubali changes, changes will be there! Our resistance to change wont help anything but will make things harder the longer we wait for the changes!!
 
RockSpider

JF-Expert Member
Feb 16, 2014
6,865
1,500
Nimesikiliza taarifa ya habari kupitia kituo cha ITV leo saa mbili, kuwa jeshi la polisi limezuia mikutano ya UKAWA ndani ya mkoa wa Kigoma kwa muda wa siku tatu sasa. Anayejua nini kilichopo nyuma ya pazia atujuze tafadhali.

Watabana wataachia tu! wanajua kuwa hawawezi kugeuza usiku kuwa mchana ...
 
Mutakyamirwa

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
4,945
1,500
Kama Zanzibar walizuia na baadae wakarihusu hata Kigoma itakuwa hivyo, tena haraka iwezekanavyo!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom