Kwanini ujiunge na CHADEMA na kuachana na CCM... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini ujiunge na CHADEMA na kuachana na CCM...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chris Lukosi, Aug 31, 2012.

 1. Chris Lukosi

  Chris Lukosi Tanzanite Member

  #1
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 4,587
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Ndugu zanguni,
  Kama mjuavyo vuguvugu la mageuzi limepamba moto nyumbani na kila kukicha chama chetu kinazidi kujizolea umaarufu kwa sababu ni chama pekee kinachopambana na mafisadi bila ya woga.Kila kukicha Viongozi wetu wa taifa wanazunguka nchi nzima kueneza demokrasia ya kweli na huru. Hivyo basi ni wajibu wetu kuwaunga mkono kwa kuendeleza harakati hizi. Zile enzi za kuogopa au kufikiri kuwa uongozi wa nchi ni kwa ajili ya familia fulani au majina fulani ya vigogo zimepitwa na wakati. Mkumbuke sababu ya uprising ya egypt ilitokana na waarabu kuchoshwa na utawala wa familia moja kwa muda mrefu. Haya pia tumeyaona Libywa, na Tunisia. Watu hawa walisema tumechoka. Haiwezekani baba amuachie mwana na mwana endeleze utwawala kwa wajukuu, utaratibu huu hautakiwi tena duniani kote. Sisi hapa tumshukuru mwenyezi Mungu katujalia tuko kwenye nchi inayoongozwa kwa demokrasia ya kweli na huru tunaona matunda ya demokrasia hivyo ningependa mafanikio na faida tunazoziona hapa basi na ndugu zetu kule nyumbani waweze kuishi kama sisi. Bila woga wala hofu.

  Nadhani wote mnakumbuka chama cha UNIP cha Keneth Kaunda wa Zambia. Chama hiki kilitawala Zambia kwa miaka mingi lakini vyama vingi vilipoingia Zambia Unip ilipotea kabisa kwenye Ramani ya zambia na uchaguzi uliopita UNIP walipata asilimia 0.38% ambayo ni chini ya asilimia moja. Hii ina maana waliopiga kura ni watoto wajomba na mashangazi. Kila mtu alichoka.
  Tanzania ni kama gari , Chama kinachotawala ni kama engine na Kiongozi wa nchi ndio dereva.

  CCM ni kama engine iliyochoka sana kwa kukosa matunzo mazuri kiasi kwamba hata leo hii ukibadilisha dereva au spare mpya engine hii haiwezi kulipandisha gari letu kwenye mlima mkali wa maendeleo. Engine hii iitwayo CCM haijawahi kufanyiwa overhaul au main service lakini badala yake wao humwaga oil chafu tu bila hata ya kubadilisha oil filter. Na tukifanya mchezo gari litaanza kuporomoka kurudi nyuma.

  Ni wakati umefika kwa watanzania kubadilisha engine kwenye gari letu tanzania. Tunatakiwa tufunge engine mpya kabisa iitwayo Chadema.

  Chadema Chini ya madereva wetu Dr Slaa na Mheshimiwa Mbowe tutaweza kupanda mlima huu mkali bila wasi wasi kwa kutumia rasilimali tulizonazo ambazo kila mtu anajua kuwa sisi ni matajiri wa rasilimali tatizo ni CCM, hawana maarifa wala plan ya jinsi ya kuzitumia rasilimali hizi walizozikalia kwa miaka 50 sasa.. Chama chetu kitawapa nafasi wasomi na watu wote wenye vipaji, walete maarifa yao kwenye sekta ya viwanda , madini na mariasili kitu ambacho
  CCM imeshindwa kuwatumia. Badala yake utwasikia tu mara kilimo kwanza mara kilimo ni uti wa mgongo au kilimo cha kufa na kupona . Hatuwezi kuendelea kwa kutegemea kilimo peke yake. Kama ni maboga kila mtu analima.

  Mimi binafsi ninaamini utajiri wa nchi hutokana na viwanda pamoja na maliasili kama gesi, mafuta, madini mbalimbali nk.
  Nchi haiwezi kuwa tajiri kwa kutegemea kilimo, kilimo huchangia asilimia ndogo sana ya uchumi wa nchi.

  SIRI YA MAFANIKIO YA TAIFA BORA NI MAARIFA
  MAARIFA HUTOKA KWA WASOMI PAMOJA NA WATU MBALI MBALI WENYE UJUZI
  SERIKALI YETU IMESHINDWA KUWATUMIA WASOMI WETU BADALA YAKE IMEWATELEKEZA NA KUWAACHA WAKIBEBA BOKSI ULAYA NA MAREKANI.

  Wachina walikuwa masikini sana miaka ya nyuma, na viwanda vingi vya wamarekani na nchi nyingine tajiri vilijengwa china kwa sababu ya cheap labour.
  Wachina waliamua kutumia wasomi wao na watu wenye ujuzi kujifunza maarifa wanayotumia wamarekani na mataifa tajiri. Badaad ya hawa watu kuyapata maarifa waliamua kuanza kujenga viwanda vyao wenyewe nma kutengeneza malighafi kama zile za wamarekani kwa bei nafuu, hii iliwasaidia kumaliza masoko yote nchi za africa na asia.
  Uchumi wa china umekua kwa maarifa, sasa kwa nini na sisi uchumi wetu usikue kwa maarifa.

  Unasema kilimo kwanza halafu unanunua jembe la disc plough ulaya wakati hili jembe linaweza kutengenezwa pale ZZK au UFI? Disc plough inaweza kutengenezwa na fundi welder wa kawaida kabisa kama akipewa mafunzo madogo tu.

  Unasema kilimo kwanza wakati pamba inayolimwa mwanza inapelekwa China kutengeneza nguo halafu hizo nguo zinarudishwa tanzania kuuzwa. kwa nini usiwachukue wasomi wakasomee mambo ya viwanda vya nguo China warudi nyumbani wakatengeneze hizo nguo pale Mwatex?

  Viwanda tunavyo
  Wasomi tunao
  Malighafi tunazo
  Mengine mtamalizia wenyewe

  CCM kama UNIP ya Zambia ifikapo 2015 kura zao zitatoka kwa watoto wa vigogo, wajomba na close relatives
  On 23 September, Chief Justice Ernest Sakala announced Sata the winner of the election with 1,150,045 votes, or 43%, with 95.3% of votes counted. Banda received 961,796 votes, or 36.1%, and other minor parties trailed in the poll.[SUP][5][/SUP][SUP][11][/SUP] Sata was sworn into office later that day
  [TABLE]
  [TR="bgcolor: #E9E9E9"]
  [TH="colspan: 5"]Zambian presidential election, 2011

  [/TH]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #EEEEEE"]
  [TH="colspan: 2"]Party[/TH]
  [TH]Candidate[/TH]
  [TH]Votes[/TH]
  [TH]Percentage[/TH]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [TD]Patriotic Front[/TD]
  [TD]Michael Sata[/TD]
  [TD="align: right"]1,170,966[/TD]
  [TD="align: right"]41.98%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #3BADF3"][/TD]
  [TD]Movement for Multi-Party Democracy[/TD]
  [TD]Rupiah Banda[/TD]
  [TD="align: right"]987,866[/TD]
  [TD="align: right"]35.42%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #FFF500"][/TD]
  [TD]United Party for National Development[/TD]
  [TD]Hakainde Hichilema[/TD]
  [TD="align: right"]506,763[/TD]
  [TD="align: right"]18.17%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TH="bgcolor: #EEEEEE"][/TH]
  [TD]Alliance for Democracy and Development[/TD]
  [TD]Charles Milupi[/TD]
  [TD="align: right"]26,270[/TD]
  [TD="align: right"]0.94%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TH="bgcolor: orange"][/TH]
  [TD]National Restoration Party[/TD]
  [TD]Elias Chipimo Jnr[/TD]
  [TD="align: right"]10,672[/TD]
  [TD="align: right"]0.38%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #C94E47"][/TD]
  [TD]United National Independence Party[/TD]
  [TD]Tilyenji Kaunda[/TD]
  [TD="align: right"]9,950[/TD]
  [TD="align: right"]0.36%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #165D25"][/TD]
  [TD]Forum for Democracy and Development[/TD]
  [TD]Edith Nawakwi[/TD]
  [TD="align: right"]6,833[/TD]
  [TD="align: right"]0.24%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TH="bgcolor: #EEEEEE"][/TH]
  [TD]National Movement for Progress[/TD]
  [TD]N'gandu Peter Magande[/TD]
  [TD="align: right"]6,344[/TD]
  [TD="align: right"]0.23%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TH="bgcolor: #FDE910"][/TH]
  [TD]Heritage[/TD]
  [TD]Godfrey Miyanda[/TD]
  [TD="align: right"]4,730[/TD]
  [TD="align: right"]0.17%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TH="bgcolor: #EEEEEE"][/TH]
  [TD]Zambians for Empowerment and Development[/TD]
  [TD]Frederick Mutesa[/TD]
  [TD="align: right"]2,268[/TD]
  [TD="align: right"]0.08%[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #EEEEEE"]
  [TD="colspan: 3, align: right"]Valid votes[/TD]
  [TD="align: right"]2,732,662[/TD]
  [TD="align: right"]97.93%[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #EEEEEE"]
  [TD="colspan: 3, align: right"]Invalid or blank votes[/TD]
  [TD="align: right"]56,678[/TD]
  [TD="align: right"]2.03%[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #EEEEEE"]
  [TD="colspan: 3, align: right"]Total votes[/TD]
  [TD="align: right"]2,789,340[/TD]
  [TD="align: right"]100.00%[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #EEEEEE"]
  [TD="colspan: 3, align: right"]Voter turnout[/TD]
  [TD="colspan: 2, align: right"]53.98%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 5"]Source: Electoral Commission of Zambia[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  SISI SOTE NI NDUGU TATIZO NI CCM

  PIPOOOOZ!
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,848
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Maelezo yako yanatia hamasa sana.inji ya ahadi tunaikaribia
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Tuko pamoja sana kamanda....
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Nimeyapenda maneno yako, lakini zaidi Nimependa maneno haya "sisi sote ni ndugu tatizo ni ccm"
   
 5. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. U

  Udaa JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 727
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja,sisi sote ni ndugu tatizo jakaya na timu yake.
   
 7. c

  chama JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Lukosi acha kuwapiga watu magirini, kilichokuingiza Chadema ni ulaji tu kuna dili unazichungulia;hasa baada ya kunyimwa tenda ya ukaguzi wa magari yanayoingizwa Tanzania, hiyo Zambia imebadilika kitu gani baada ya Kaunda kuondoka madarakani? Nitajie maraisi walioingia madarakani baada ya Kaunda ukiachia marehemu Mwanawasa nani ambaye hakukutwa na kashfa kubwa ya ubadhirifu na wizi? Kina Chiluba walitumia mbinu kama hizi wanazotumia Chadema kuwahadaa wazambia matokeo ni haya Zambia ipo masikini na hakuna walichobadili zaidi ya kujitarisha wao na familia zao. Mzee Kaunda anaendelea kuheshimika sana na wazambia kwani wameujuea ukweli na wengi wao wanajutia maamuzi ya yaliyowaingiza kina Chiluba madarakani. waeleze wanachadema wenzako kilichokuingiza Chadema acha hizi blaah blaah na uwongo mwingi.

  Chama
  Gongo la mboto
   
 8. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Naunga mkono mabadiliko lakini yafanyike kwa mpangilio na kila mtu apate maumivu. Haiwezekani wengine wanalala nyumbani na wake zao halafu wengine wanaungua jua barabarani na kupigwa risasi. Cha kushangaza hawa wanaolala ndiyo wanakuwa wa kwanza kujifanya kuchochea wenzao eti wawe mstari wa mbele kuadvocate mabadiliko. Hili halikubaliki hata kidogo.
   
 9. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #9
  Aug 31, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,418
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 180
  Watasema sana ila ccm 2015 tunangoa matairi ,injini na tutaiweka juu ya mawe ! Kataa bisha habari ndio hiyo
   
 10. t

  tenende JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Gamba liko kazini kutetea mafisadi waendelee kuteketeza raslimali zetu!.. ni ulaji gani uko CHADEMA? ... Kungekuwa na ulaji wewe mwenye tamaa ya kufisidi mali za watanzania ungeendelea kukibeba chama cha mafisadi?. .... Zambia unaisikia au unasimuliwa?... mtu mzima una mawazo ya mwaka 47.
   
 11. c

  chama JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nimeishi Lusaka maeneo ya Kabulonga miaka 4 na bado nina marafiki wengi tu Zambia hebu mwambie Lukosi aeleze maendeleo y Zambia baada ya Kaunda.

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 12. c

  chama JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nimeishi Lusaka maeneo ya Kabulonga miaka 4 na bado nina marafiki wengi tu Zambia hebu mwambie Lukosi aeleze maendeleo y Zambia baada ya Kaunda. Naijua Zambia wakati wa utawala Kaunda na baada ya Kaunda

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 13. Chris Lukosi

  Chris Lukosi Tanzanite Member

  #13
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 4,587
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Uchumi wa zambia ulianguka sana kwa sababu ulikuwa unategemea shaba peke yake na ndio maana walianguka.
  Zambia walikuwa na njaa sana kiasi kwamba wale dagaa waliooza walikuwa wanauzwa zambia kutoka tanzania, lakini sasa zambia wanajitegemea na uchumi wao umeanza kurudi taratibu.
  Zambia walibadili serikali kwa amani na kila mtu anaishi kwa furaha.
   
 14. c

  chama JF-Expert Member

  #14
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Lukosi nilikuuliza baada ya Kaunda kuondoka madarakani ukiachia marehemu Mwanawasa ni nani ambaye hakukutwa na kashfa ya wizi na ubadhirifu? Kumbuka waliingia madarakani kwa mbinu hizi za movement kwa madai watabadilisha maisha ya mzambia; wazambia wengi hawana furaha ya maisha ni dhiki imewatawala hivi umewahi kufika Zambia au unaisoma kwenye magazeti?

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 15. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #15
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,779
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Ila wewe Chama una moyo!... Mwenzako Nape haonekani humu siku hizi. Ila inawezekana kakukabidhi mkoba wa uenezi humu JF.
  Kiukweli tumechoka kuendeshwa kama mkokoteni.
   
 16. c

  chama JF-Expert Member

  #16
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mimi ni Chama simjui wala simfahamu Nape na wala sina shida ya kumjua; ila wote tunasimamia na kutetea kitu kimoja ni wanaccm; tupo kujibu hoja,uwongo, unafiki, na majungu ya wanachadema ndani JF. Vipi Isevya hawajambo?

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 17. Chris Lukosi

  Chris Lukosi Tanzanite Member

  #17
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 4,587
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Chama,
  Unajua sasa Zambia inauza mahindi Tanzania?
  Wakati wa kaunda zambia walikuwa wanakula mawashwasha kutoka mbozi mbeya na vikanda/mizizi
  Kuna dagaa kutoka lake tanganyika zilizoharibika zinaitwa nyamnunga hizi ulikuwa ukipeleka mpulungu zambia ni dili sana wakati bongo ilikuwa ni chakula ya mifugo lakini leo wazambia hawali tena madudu bali wanauza chakula nje.
  Niliandika Zambia kama mfano tu kuna mifano mingi sana chama.
  Angola wamepigana vita miaka ishirini lakini leo wanatuzidi utajiri sisi tumeukalia chini ya uongozi wa CCM
  Chama kinachotawala Kenya sasa sio KANU tena na umeona jinsi uchumi wao ulivyokua chini ya chama kipya
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Aug 31, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kama wazambia wamekizika chama cha UNIP na kukisahau halafu wewe unakuja na talalila hapa kwamba wanajuta basi wewe una matatizo ya uelewa.
  Hata mimi ninakwenda zambia mara kadhaa kila mwaka kwa shughuli zangu binafsi lakini sijawahi kusikia wazambia wakilalamika. Tena kipindi hiki walichomchagua King Cobra ndipo wamefurahi zaidi na hali yao ya uchumi sasahivi inakua vizuri sana baada ya King Cobra kuwadhibiti viwavi jeshi wote waliokuwemo serikalini.
   
 19. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #19
  Aug 31, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Naunga Mkono hoja ni wakati wamabadiliko na kuunga mkono mabadiliko ili kuiondoa ccmwabepande!
   
 20. c

  chama JF-Expert Member

  #20
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Lukosi,
  Tusichanganye mada nipe majibu ya swali langu, baadaye tutaingia kwenye uchumi; Angola iweke pembeni kidogo kwasababu MPLA bado kinaongoza nchi.

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
Loading...