Kwanini Uislamu umerahisisha sana taratibu za mazishi na ndoa.

IKIRIRI

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
2,734
3,017
Amani iwe kwenu waja wa mwenyezi Mungu,

Moja ya vitu ambavyo uislamu unataka vifanyike kwa haraka wakati ukifika ni ndoa na kuzika.

Sababu kubwa ni kuepusha fitna ya dunia na maaswi.

Katika dunia ya Leo naona ndugu zetu wakristo mda mwingine nawahurumia hasa kwa wale masikini.
Ndoa imekuwa inawapa stress wanandoa kiasi kwamba hakuna furaha ili ndoa ikamilike inakuhitaji uwe na mamilioni.

Ila katika uislamu ndoa ni jambo jepesi mno nimeshuhudia MTU anaoa kwa laki1+mahari jambo ambalo kwa upande wa pili haliwezekani.

Katika uislamu unahitaji kumzika maiti pale tu akifariki hatakiwi kucheleweshwa na gharama uwa ndogo sana chini ya 50000 inategemea na mazingira ila kwa upande wa pili maiti ni gharama. Ndugu wanaumia kuchangishana coz ni dharura.

Ndugu zangu wakristo Kiukweli napata wasiwasi kwann ndoa na misiba yenu ni gharama mno?

Utaratibu huu kauleta nani? Kuna wenzi wanapenda na wanataka kufunga ndoa BT wanashindwa.

Wengine wanagombana michango ya sanduku la kuhifadhi maiti...ili halipo katika uislamu sisi tunatumia jeneza1 hakuna gharama.

Wenzetu shida wapi, au maandiko yanawahitaji kufanya haya?
 
Ikitokea tunaacha basi tuachane kwa heri siyo kwa ubaya" Kingine Waislam ibada ya Mazishi dakika chache tuu Lakini Wakristo aisee Mchungaji/Katekisti atasoma vitabu atahubiri masaa mengi sana mpaka wasikiliza neno hawaelewi washike lipi.
 
Kufunga ndoa kuwa simple kwani hiyo imewekwa na Dini au ni mtu tu anajiamulia tu?

Mkristo ukiamua kufunga ndoa simple unafunga tu, kanisa halikulazimishi kufanya sherehe kubwa,

Hukumsikia Magufuli anasema yeye na mke wake, ambao ni Wakristo walifunga ndoa bila suti na shela na wakanywa Pepsi na Mirinda tu?

Wapo Waislam wanafunga ndoa za gharama na sherehe kubwa pia

Hukumuona Ali Kiba na mdogo wake wakifunga harusi za gharama zilizokuwa publicized sana?

Kwenye maziko pia, unajiamulia pia wewe mwenyewe, mkiamua kumzika tu na sherehe ndogo hakuna atakayewazuia kuwa eti Wakristo hatuzikagi bila sherehe kubwa
 
Ikitokea tunaacha basi tuachane kwa heri siyo kwa ubaya" Kingine Waislam ibada ya Mazishi dakika chache tuu Lakini Wakristo aisee Mchungaji/Katekisti atasoma vitabu atahubiri masaa mengi sana mpaka wasikiliza neno hawaelewi washike lipi.
Hahahah
 
Kwenye hill LA ndoa nadhani ni uwezo wa MTU kuna waislamu wanafanya sherehe kubwa tu, na kuna wakristo ambao wanaenda kanisani wao na mashahidi wao kufunga ndoa bila gharama zozote.

Hapo kwenye misiba sina comment!
 
Back
Top Bottom