Kwanini uhangaike na majini wakati kuna malaika

Hata Mimi ninatamani kupata maarifa ya malaika
Malaika wamewekwa na Mungu kwa ajili yake (Mungu) na kwa msaada wetu (wanadamu). Tofauti na majini, malaika hawawezi kutenda maovu. Pia majini kamwe kiasili hayawezi kutenda mema.

Kwanini watu wengi hushindwa kuwatumia au kushirikiana na malaika? Kwasababu watu wengi wanataka kutumia malaika kutenda maovu; hii ni kinyume na asili ya viumbe hivi.

Pia wale wanaotumia majini kutaka kutenda mema hushindwa kwani kwa asili yao majini hawawezi kutenda mema.

Mema yote hutoka kwa Mungu iwe ni kama neema tu “grace” yaani kupewa jema hata bila kustahili, au hutokana na mastahili ya kazi nzuri. Maandiko yanasema: mfanyakazi anastahili ujira wake.

Malaika wapo kila wakati kwa ajili ya kutusaidia, na hutusaidia sana kila mara. Wahusika katika ulinzi wako na kuleta jumbe mbalimbali kutoka kwa Mungu.

Unapotenda jema unakuwa mmoja wa watendaji wa Ufalme wa Mbinguni, na hivyo malaika hujumuika pamoja nawe hata kama huwaoni.

Ni kinyume na Mbingu kuwatumia malaika kupata mali bila jasho lako ama njia nyingine isiyo halali. Ukitaka mafanikio unaweza kumwomba Mungu usaidizi wake ambavyo vinapatikana kama vile ulinzi dhidi ya waovu, hekima na maarifa, kukubalika, kusaidiwa na kupewa bure (neema).

Yakupasa kutumia vyote hivyo kwa utashi wako na utafanikiwa. Kumbuka kila wakati kuwa MAFANIKIO (baraka)=WEWE+MUNGU. Nje ya hapo hakuna mafanikio. Wanaotumia majini wanakitu kinachoonekana kufanana na mafanikio lakini ukweli ni kwamba siyo mafanikio bali na uongo unaotokana na baba wa uongo yaani shetani.
 
Ok..
Walikua na utofauti gan kwa u bin wao (baba zao ni nani) ?? Wote walikua wafalme ?? Wafalme wa wapi ??

Sina maana mbaya/kuikufuru imani yangu takatifu au ya mtu mwingine ila sometimes i feel kuna vitu bible haijaandika au niseme imeficha labda kwa dhumuni flan. Dhumuni gan sijui...ndio sabab nina raise such questions.

Akasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usio mwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji.
Basi tukaufanya upepo umtumikie, ukenda kwa amri yake, popote alipo taka kufika.
Na tukayafanya mashet'ani yamtumikie, wote wajenzi na wapiga mbizi.[QUR'AN 38:35-37]
 
Malaika wamewekwa na Mungu kwa ajili yake (Mungu) na kwa msaada wetu (wanadamu). Tofauti na majini, malaika hawawezi kutenda maovu. Pia majini kamwe kiasili hayawezi kutenda mema.

Kwanini watu wengi hushindwa kuwatumia au kushirikiana na malaika? Kwasababu watu wengi wanataka kutumia malaika kutenda maovu; hii ni kinyume na asili ya viumbe hivi.

Pia wale wanaotumia majini kutaka kutenda mema hushindwa kwani kwa asili yao majini hawawezi kutenda mema.

Mema yote hutoka kwa Mungu iwe ni kama neema tu “grace” yaani kupewa jema hata bila kustahili, au hutokana na mastahili ya kazi nzuri. Maandiko yanasema: mfanyakazi anastahili ujira wake.

Malaika wapo kila wakati kwa ajili ya kutusaidia, na hutusaidia sana kila mara. Wahusika katika ulinzi wako na kuleta jumbe mbalimbali kutoka kwa Mungu.

Unapotenda jema unakuwa mmoja wa watendaji wa Ufalme wa Mbinguni, na hivyo malaika hujumuika pamoja nawe hata kama huwaoni.

Ni kinyume na Mbingu kuwatumia malaika kupata mali bila jasho lako ama njia nyingine isiyo halali. Ukitaka mafanikio unaweza kumwomba Mungu usaidizi wake ambavyo vinapatikana kama vile ulinzi dhidi ya waovu, hekima na maarifa, kukubalika, kusaidiwa na kupewa bure (neema).

Yakupasa kutumia vyote hivyo kwa utashi wako na utafanikiwa. Kumbuka kila wakati kuwa MAFANIKIO (baraka)=WEWE+MUNGU. Nje ya hapo hakuna mafanikio. Wanaotumia majini wanakitu kinachoonekana kufanana na mafanikio lakini ukweli ni kwamba siyo mafanikio bali na uongo unaotokana na baba wa uongo yaani shetani.
Mkuu unasema majini kiasili hawawezi kutenda mema??

Mbona katika hizi imani zetu tunafundishwa kuwa majini kiasili ni malaika na kwengine tunaambiwa majini ni kama binaadamu kwa maana wapo wenye kutenda mema na wenye kutenda maovu?
 
Majini/ Pepo Wachafu. Hawa hawana ushirika na Mungu hata siku moja. Hawa ni watumishi wa Shetani. Biblia inawaita mapepo.au pepo wachafu. Kwa mkristo jini ni adui hata kama lina mletea chakula.

Ok...ni vitu gan Mungu alisema kwa vitabu vya dini tuna authority navyo ??

Tuna authority navyo ki vp ??

If so, kwann tusiwe na access navyo muda/wakat tunaoutaka sisi ??

Mbna hatukupewa such skills on using such beings ??

Kama kuna maarifa ya matumizi ya viumbe hawa wa upande wa pili, ni wapi kwenye vitabu vya dini vinaeleza maujanja hayo ??

Quran inasema Mfalme Suleiman alikua ana jeshi mpaka la majini na kwenye vita alikua akiwatumia sanaa na alikua lazima a win. Alibarikiwa na kupewa hekima nyingi, Je hakujua matumizi ya viumbe hao ni kukiuka mapenzi ya Mungu ?? Ina maana Mungu aliona sawa Suleiman kushirikiana na majini hata kwenye ujenzi wa hekalu lake ??

Why Suleiman NOT us ?? Kuna mpango wowote wa mwanadamu kumficha mwenzake na ukweli na uhalisia wa mambo ?? Kwann iwe hvyo ??

Sielewi.
 
Life is a choice, in artificial intelligence technology we will able to use robots for our own use. The physical World we live in is not ruled by those majini or whatever Wake up guys,when did you ever seen a jin?
 
Mkuu unasema majini kiasili hawawezi kutenda mema??

Mbona katika hizi imani zetu tunafundishwa kuwa majini kiasili ni malaika na kwengine tunaambiwa majini ni kama binaadamu kwa maana wapo wenye kutenda mema na wenye kutenda maovu?
Kuna uongo mkubwa kutoka kwa baba wa uongo-shetani. Ni uongo uliosukwa kijanja mno kiasi kwamba bila neema za Mungu Mwenyezi kamwe huwezi kuujua ukweli.

Majini ni viumbe walioanguka katika uasi dhidi ya Mungu, hawana lolote jema na hutenda katika ulimwengu wa giza kama watumishi wa mkuu wao yaani shetani.

Ukishirikiana nao utafanganyika na mwishowe kuangamia na kuwa mmoja katika anguko kuu.
 
Nimeelezea mitazamo ya mbili tofauti juu ya hao wanaoitwa majini,sasa hoja yako ya kwamba hao majini kiasili hawafanyi mema ndio imenishangaza kwa sababu hao majini tunaambiwa ni malaika.
 
Majini kwa “type of beings “ wapo katika kundi la malaika sawa., lakini hawa ni malaika waovu hatupaswi kufanya ushirika nao ni viumbe vyenye hadaa ya hali ya juu. Lengo lao ni kupoteza roho za wanadamu kwenye uovu na anguko kuu.
 
Ngoja nichangie kidogo kuhusu Hili, Yesu alivyofundisha kuomba katika (Mathayo 6:9 - 10)... 9. Inayosema Baba yetu uliye Mbinguni, jina lako litukuzwe. 10. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama Mbinguni.
Hiyo ni sala ambayo Yesu mwenyewe alifundisha Jinsi ya Kusali.
Yaani Baba yetu aliye Mbinguni, Ufalme wako ufike, Utakalo lifanyike duniani kama Mbinguni, Yaani Ufalme wa MUNGU ushuke ili uwe nasi. Na Utakalo lifanyike duniani Kama Mbinguni. Kwa sababu MUNGU ana Ufalme wake na huo Ufalme uje ili utusaidie hapa duniani (Kama andiko linavyosema), sasa Ufalme wa MUNGU una Malaika ambao anawatumia kama watenda kazi wake, Kwa hiyo ukiomba Ufalme wake uje maana yake unataka kuwatumia na watenda kazi wake ambao ni Malaika.
Kinachohitajika ni Imani yako tuu Brother. Yaani unaita Ufalme Kwa Imani na pia unawaagiza Malaika kwa Imani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna uongo mkubwa kutoka kwa baba wa uongo-shetani. Ni uongo uliosukwa kijanja mno kiasi kwamba bila neema za Mungu Mwenyezi kamwe huwezi kuujua ukweli.

Majini ni viumbe walioanguka katika uasi dhidi ya Mungu, hawana lolote jema na hutenda katika ulimwengu wa giza kama watumishi wa mkuu wao yaani shetani.

Ukishirikiana nao utafanganyika na mwishowe kuangamia na kuwa mmoja katika anguko kuu.
Hivi haya uliyo andika yapo kwenye vitabu vya Muumba au umetoa mawazo yako binafsi?

Kama yapo tuonyeshe maandiko tafadhali, mana sijawahi ona shule inafundisha elimu hii isipokuwa lazima vitabu vya Mungu vihusike.

Naomba unifundishe kwanini neno JINI litumike na isiwe neno SHETANI pekee?

Kwanini katika maovu yote wanadamu tumezoea kumhusisha SHETANI na lisitajwe neno JINI?

Je SHETANI ni kiumbe au ni cheo cha uovu?

Je lengo la kuumbwa MAJINI ni lipi?( Kwanini Mungu ameumba majini?) kwa mujibu wa Biblia.

NB: Biblia na Korani zihusike sana katika kujibu haya tafadhali, mana najua hakuna mwanadamu ajuae elimu hii isipokuwa kupitia vitabu vya Mungu.

Ninayoandika hapa ni kwa mujibu wa maandiko matakatifu (Biblia) na uvuvio wa moja kwa moja. Siandiki kwa mujibu wa korani kwani najua ukweli haupo huko.

Jini ni viumbe vya ngazi ya chini, shetani ni wa juu kuliko majini. Kuna mashetani ya ngazi mbalimbali lakini wapo wakuu wao kama vile belzebul mkuu wa mapepo, Lucifer malaika wa mwanga, nk

Maovu yote yanahusishwa na shetani kwasababu yeye ndiye mkuu wa jeshi la uovu na kazi zote za uovu hufanywa kwa amri yake.

Shetani ni kiumbe (malaika) aliye asi mamlaka ya Bwana Mungu. Pia shetani ni cheo yaani ni malaika mwovu wa ngazi ya juu mwenye nguvu na mamlaka juu ya malaika wengine waovu kama vile mapepo na majini.

Mungu hakuumba kiumbe kinachoitwa jini au shetani. Aliumba malaika wema. Baadhi yao waliasi na kupoteza utukufu wa Mungu na hivyo kuwa mashetani na majini. Hawa wametupwa nje ya Ufalme wa Mungu na hawatubu na wanasubiri hukumu yao, maangamizo makuu.

Korani inazungumzia majini kama viumbe vizuri tu na mwanadamu anaweza kushirikiana navyo kufanya mazuri, huu ni upotofu mkubwa. Mvuvio huu wa kipepo ndio uwafanyao waislamu wengi kuingia shirki na dini nzima kuwa chini ya himaya ya shetani. Shetani ni baba wa uongo wote na hutumia uongo kuwaangusha wanadamu kama ilivyokuwa pale bustani ya Eden.

Watu wengi wanafanya kazi na majini kwa kujua na bila kijua pia. Yesu Kristo ni Mungu na jina lake tu likitajwa viumbe vyote vya kiroho husujudu kifudifudi. Mtu aliyepagawa na mapepo kamwe hatotaja jina la Yesu mpaka majini yaondolewe. Kwa jina la Yesu kila goti litapigwa, Biblia inasema.
 
Mkuu hayo ni maneno yako, nataka maandiko. Ukiniambia kwa mujibu wa Biblia lakini huna andiko lolote unalotoa kusapoti mawazo yako hapo unakuwa hukufundisha isipokuwa mawazo yako tu.

Acha yale mambo ya kusema Biblia inasema...ili kutaka Watu wakuamini kwa kuwa umetaja Biblia.

Binafsi mawazo yako hayo bado sijayakubali mpaka yasapotiwe na vifungu, mimi sitaki yale maneno ya wachungaji ya kuwa biblia inasema... lakini andiko halitajwi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majini kwa “type of beings “ wapo katika kundi la malaika sawa., lakini hawa ni malaika waovu hatupaswi kufanya ushirika nao ni viumbe vyenye hadaa ya hali ya juu. Lengo lao ni kupoteza roho za wanadamu kwenye uovu na anguko kuu.
Sasa mkuu tatizo ni kwamba kwenye Qur'an jini amezungumziwa kama kiumbe kilichoumbwa na Mungu(si malaika) yani kuna Binaadamu,malaika na hao majini.
Ila biblia haisemi kuwa Mungu aliumba majini,sasa sijajua ni vigezo gani vinatumika kutambua kuwa hao viumbe majini waliyozungumziwa kwenye Qur'an ndio hao malaika tena waliyoasi? Au neno jini lina maana gani hao malaika waliyoasi ndio waitwe majini?

Kwa sababu mara nyingi utakuta watu wanasema Yesu sio Isa na Isa sio Yesu,kwamba hao wawili tofauti na wanaeleza hutofauti wao,ila mwenye upande wa majini pamoja na kuwa Qur'an inaeleza asili yao ni tofauti na malaika ila wakristo wanawahusisha na malaika(waovu).
 
Mkuu unasema majini kiasili hawawezi kutenda mema??

Mbona katika hizi imani zetu tunafundishwa kuwa majini kiasili ni malaika na kwengine tunaambiwa majini ni kama binaadamu kwa maana wapo wenye kutenda mema na wenye kutenda maovu?
Majini ni ufalme wa shetani, kwa mujibu wa mafundisho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom