Kwanini uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma haujafanyika Zanzibar?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,883
Habari wadau!

Tunajikubali kuwa tuna nchi inaitwa Tanzania na rais wake anajulikana na akitoa amri inatakiwa itekelezwe pande zote za nchi.

Lakini sio kweli amri ya rais wa Tanzania iliyojificha kwenye koti la muungano (Tanganyika) inaishia baharini hivyo ni rais wa Tanganyika sio Tanzania kama wanavyo waaminisha wananchi.

Amri ya uhakiki wa watumishi tena wakisema asilimia kubwa ya mishahata hutoka Tanganyika kuwalipa watumishi wa Zanzibar wao hawajaguswa na amri ya amiri jeshi mkuu.

Sasa Zanzibar haiko Tanzania? Je amri ya mkuu haiwahusu wakati payroll ni moja? Mifuko ya hifanyi zankijamii wanategemea tanganyika?

Hii ni serikali moja,mbili au tatu?
 
  • Thanks
Reactions: GUI
hivi yule waziri wa utumishi anavuka maji? ..
nadhani hata matamko ya font feji pia hayavuki maji muungano upo kinadharia tu
 
Ukweli utaendelea kubaki kuwa ukweli, Muungano ni kwa faida ya Zanzibar na si vinginevyo, lakini kwa Tanganyika tulichonacho kikubwa ni hilo jina la "Tanzania "
 
Si kweli,mbona kila uchaguzi hupelekwa vifaru na majeshi zanzibar kupindua maamuzi ya wazanzibar,muungano huu ni wa kupeleka vifaru tu na majeshi na si jenginelo.
 
Muwe mnajifunza siasa za ndani pia.... JPM hahusiki na watumishi wa SMZ. Wao wana wizara yao kamili na ya utumisi. Hata hivyo kwa zile taasisi za Muungano wapo watumishi wa taasisi hizo waliopo zanzibar ambao hili sakata limewagusa.
 
Si kweli,mbona kila uchaguzi hupelekwa vifaru na majeshi zanzibar kupindua maamuzi ya wazanzibar,muungano huu ni wa kupeleka vifaru tu na majeshi na si jenginelo.
Ndiyo maana nikasema ni kwa faida ya Zanzibar hasa zaidi zaidi kiuchumi Zanzibar inafaidika na muungano na unajuwa mtu akishakugharimikia lazima atataka awe na sauti juu yako na ndiyo kisa cha vifaru.
 
Kuna baadhi ya watu akili zao ni sifuri kabisa. Yanajibu hoja ki-mihemko Tu bila kujua kinachoendelea kule Zbar.
Zbar kuna watumishi wa serikali wa namna mbili, wale wanaotumikia SMZ ambao ni wengi, na wale wanaotumikia serikali ya Jamhuri Mungano wa Tanzania ambao ni wachache sana. Na hawa watumishi wa SMT kama wenyewe wanavyowaita wameingia kwenye kwenye mkondo wa uhakiki. Watumishi kama vile wa BOT, Posta, TMA, nk walifanyiwa pia uhakiki.
 
Zanzibar ipo kwenye kundi la wanasiasa, maDC, maRC, n.k. wao nao wanatakiwa kujua kusoma na kuandika tu
 
Kuna baadhi ya watu akili zao ni sifuri kabisa. Yanajibu hoja ki-mihemko Tu bila kujua kinachoendelea kule Zbar.
Zbar kuna watumishi wa serikali wa namna mbili, wale wanaotumikia SMZ ambao ni wengi, na wale wanaotumikia serikali ya Jamhuri Mungano wa Tanzania ambao ni wachache sana. Na hawa watumishi wa SMT kama wenyewe wanavyowaita wameingia kwenye kwenye mkondo wa uhakiki. Watumishi kama vile wa BOT, Posta, TMA, nk walifanyiwa pia uhakiki.
Kati ya wale na ww yupi mwenye mihemko? Naona ww ndiyo unamihemko.
Kubali kataa kuna TANGANYIKA NA ZANZIBAR KIMVULI CHAKE NI TANZANIA
Unaposema kenya, uganda, n.k hiz zote ni nchi mmoja kwahiyo sheria ni moja tu kwa watu wote.
Mkuu hebu kaa chini na utulize akili.

1.USHAWAHI KUONA NCHI MOJA MARAIS WAWILI?
Yes! Unaweza kutoa mfano wa sudan lkn ukumbuke Sudan imeshagawanyika kuna sudan kusin na kaskazini.
Sheria ikitolewa ni kwa watu wote. Mkuu km hauamin ZANZIBAR NI NCHI KM ZINGINE
Hebu nenda zanzibar ukanunue Flat screen tu halafu uje nayo bara huku kwa watanganyika ndiyo uone muziki wake.
 
Habari wadau!

Tunajikubali kuwa tuna nchi inaitwa Tanzania na rais wake anajulikana na akitoa amri inatakiwa itekelezwe pande zote za nchi.

Lakini sio kweli amri ya rais wa Tanzania iliyojificha kwenye koti la muungano (Tanganyika) inaishia baharini hivyo ni rais wa Tanganyika sio Tanzania kama wanavyo waaminisha wananchi.

Amri ya uhakiki wa watumishi tena wakisema asilimia kubwa ya mishahata hutoka Tanganyika kuwalipa watumishi wa Zanzibar wao hawajaguswa na amri ya amiri jeshi mkuu.

Sasa Zanzibar haiko Tanzania? Je amri ya mkuu haiwahusu wakati payroll ni moja? Mifuko ya hifanyi zankijamii wanategemea tanganyika?

Hii ni serikali moja,mbili au tatu?
zanzibar ni serikali tofauti ya ya tanzania bara
 
Back
Top Bottom