Kwanini ugomvi wa wazazi wa pande zote mbili iwe kikwazo cha sisi kuoana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini ugomvi wa wazazi wa pande zote mbili iwe kikwazo cha sisi kuoana

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by GM7, Jan 26, 2010.

 1. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wana JF na wazazi wote wenye hali kama hiyo kwenye kichwa cha habari,
  Kuna kijana mmoja amebahatika kumpata mchumba mzuri sana na wanaelewana sana na wanapendana kweli kweli. Sasa wakakubaliana wafuate taratibu zote ili wafunge ndoa. Tatizo kubwa likawa ni kwa wazazi wao. Wazazi hawa wa upande wa kiume na wa kike waliwahi kugombana siku za nyuma sana hadi sasa wazazi hao hawaelewani kabisa.

  Sasa kijana wa kiume alipowaeleza wazazi wake kuwa amepata mchumba katika familia hiyo ya upande wa kike na wanataka wafunge ndoa, wazazi wa kijana wa kiume wakakataa katakata. Vile vile kwa upande wa binti aliwaeleza kuwa amepata mchumba kwenye familia hii na wao pia walikataa katakata. Sababu za kukataa ni ugomvi wao wa siku za nyuma ambao hauhusiana kabisa na watoto wao.

  Naamini wazazi wetu wamo humu JF, hebu tujadili mada hii, Kwanini ugomvi wa wazazi wetu iwe kikwazo kwa sisi vijana tuliopendana tena mapenzi ya dhati kabisa?

  (Hii siyo story ni ishu ya kweli kabisa)
   
Loading...