Kwanini UDSM walizuiwa kuhudhuria Kongamano la katiba UDOM?

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Mwananchi, uk 2

:A S cry::A S cry::A S cry:Kuna mambo mengine yanafanyika Tanzania yanachekesha na pia kuuzunisha sana. Wanafunzi 50 wa UDSM walizuiwa jana kuhudhuria kongamano la katiba UDOM eti kwa sababu za kiintelijensia , kwamba lengo llilikuwa kwenda kupandikiza chuki kwa
wanafunzi wa UDOM dhidi ya serikali. Walizuiwa maeneo ya Chamwino na polisi.

Katika maswala ya demokrasia TZ tunaenda mbele na kurudi nyuma. Hao wanafunzi wa UDSM wana chuki gani dhidi ya serikali? Au kwa vile labda wangezungumza mambo ambayo serikali isingependa kusikia? Inaumiza sana.:A S cry::A S cry::A S cry::A S cry::A S cry:
 
Mimi ninashangaa sana, nchi za wenzetu wanapenda sana kuwashirikisha wasomi katika michakato mbalimbali ya kuleta mabadiriko katika dola, lakini cha kushangaza sisi hapa kwetu ni tofauti kabisa, naomba mnikumbushe ni lini Kikwete ameenda UDSM kuhutubia jambo na kuomba maoni ya wasomi?, Sana sana nakumbuka serikali yake iliandaa mchakato wa kuwaandikisha kama wapiga kura katika maeneo ya vyuo na kuhakikisha wakati wa upigaji kura wanakuwa hawapo maeneo hayo. Serikali iache kuwaogopa wasomi izitumie vizuri changamoto wanazozitoa iachane na ule mning'inio wa kushangiliwa kwa kila kitu na wazee vijijini ambao wanaamini mabadiriko ni uvunjifu wa amani japo baadhi hata ukiwauliza amani inamaanisha nini hata hawajui.
 
Mchango wako nimeupenda lakini umekosea sehemu hiyo niliyoweka red, nadhani hapakuwa mahala pake
 
Hii ilifanyika lini? source yake ikoje?

Mleta mada toa details kama mana mada yako ni kama wote tulikuwepo
 
Mimi ninashangaa sana, nchi za wenzetu wanapenda sana kuwashirikisha wasomi katika michakato mbalimbali ya kuleta mabadiriko katika dola, lakini cha kushangaza sisi hapa kwetu ni tofauti kabisa, naomba mnikumbushe ni lini Kikwete ameenda UDSM kuhutubia jambo na kuomba maoni ya wasomi?, Sana sana nakumbuka serikali yake iliandaa mchakato wa kuwaandikisha kama wapiga kura katika maeneo ya vyuo na kuhakikisha wakati wa upigaji kura wanakuwa hawapo maeneo hayo. Serikali iache kuwaogopa wasomi izitumie vizuri changamoto wanazozitoa iachane na ule mning'inio wa kushangiliwa kwa kila kitu na wazee vijijini ambao wanaamini mabadiriko ni uvunjifu wa amani japo baadhi hata ukiwauliza amani inamaanisha nini hata hawajui.

****** hawez kuja UDSM, Labda kuwe na sherehe ya harusi Nkurumah
 
suala la kushiriki kongamano la katiba ni fursa huru kwa kila mtanzania. wasomi kunyimwa nafasi ni ishara ya serikali isiyojali michango ya wasomi na watalamu.
 
Back
Top Bottom