Kwanini Udanganyifu, Ujanja Ujanja, Uongo Uongo, Umejaa Sana kwenye Jamii Yetu?

Mchanya

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
974
1,525
Fanya utafiti wako mdogo kwenye jamii jamii yetu utagundua kuna changamoto kubwa sana ya uaminifu karibu kwenye nyanja zote, kazini, kwenye biashara, mahusiano, siasa na hata kwenye masuala ya kiimani.

Kiwango cha watu kuonesha udanganyifu, wizi, uongo, ujanja ujanja, ni kikubwa mno. Waajiri wengi wa makampuni na mashirika na hata wamiliki wa biashara za kawaida za chini kabisa, wanalalamika kwamba wanatumia muda, fedha na nguvu kubwa katika kulinda wizi, uhalifu, udanganyifu ili kudhibiti mali na biashara zao kuliko kufanya uzalishaji na kuendeleza biashara zao.

1) Jaribu kutuma fedha kwa watu watano kwa njia simu, jifanye kwamba umekosea na uwaombe wakurudishie, unadhani wangapi watarudisha?

2) Umepanga kukutana na mtu muda fulani, lakini hajafika, unampigia uko wapi? anakwambia anafika 'dakika sifuri' lakini anakuja dakika 40 baadaye!!

3) Umeingia ubia wa kibisahara na mwenzako, mara tu anaposhika fedha, anabadilika, anapotea na fedha zote na hapatikani hata kwenye simu!!

4) Unapata mpenzi , anakuambia 'simu yake mbovu', 'amefiwa', anataka 'mtaji wa biashara' anasema anakupenda na baadaye unagundua kwamba yote haya ni uongo, why!!??

5) Fundi wa ujenzi anakupa gharama za materials, unampa pesa unashangaa vitu alivyonunua na pesa havilingani, unachunguza unagundua 'umepigwa'

6) Unaambiwa kwamba 'sisi kama nchi' hatutakopa nje, tunajenga kwa fedha zaetu za nje na nchi iko kwenye 'raiti traki' na kwamba soon maisha yetu yatakuwa bora, baadaye utagundua kwamba kumbe si kweli!

7) Watu wana degree za kawaida na Masters, PHDs lakini kumbe ukichimba sana utagundua ni udanganyifu mkubwa umefanyika
Najua wewe pia unayo mifano mingi - hebu iweke hapa,

Yaani inabidi uishi maisha yaliyo na mashaka mashaka kila siku, kwamba unasita kumwamini yeyote. Hivi hali hii inasababishwa na nini? Kwa anayejua tunaomba atujuze haya yote yanasababishwa na nini?
 
Unaulizwa taja eneo ambalo maandamano yangeanzia unajibu ni nchi nzima ""

Hata Arab Springs haikuanza nchi nzima kwa wakati mmoja kuna Benghaz na Tahariri Squere ,halafu maandamano nchi nzima ndo ugaidi

Hakika wasiyojulikana wanazidi kujulikana
 
Hiyo namba mbili inakera Sana, haiwezekani mtu unampigia simu anakwambia nisubiri kidogo ndani ya sekunde kumi nitakuwa nishafika,khaa! hivi watu wanazijua sekunde kumi kweli?...Utasubiri Kama nusu saa hivi ndo anatokea wakati mlishapanga mkutane muda gani,Hana dharura ya maana Wala nini, ni vitu vya kipuuzi tu ndo vimemchelewesha...
 
Back
Top Bottom