Kwanini TV na Redio zote zimeacha kuripoti mikutano ya CHADEMA lgunga?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,645
155,015
Kuanzia kampeni za lgunga zianze sijaona Tv wala Sijasikia redio ikiripoti kiufasaha juu ya mikutano ya kampeni ya Chadema lgunga.
Tatizo ni nini? Je Tv na redio nyingine zimesha lamba pilau, tshirt na kapelo za bure au Chadema haibebeki na hailipi?
 
Hawafanyi mikutano! Wao ni wanamagwanda kazi yao ni kufanya uhuni tu, sasa unataka TV ziripoti uhuni?
 
Hata wasiporipoti, haina taabu.
Siku hizi wananchi wanajua menu wanayoitaka kwenye uwanja wa siasa.
Enzi za kulishwa propaganda kwny vyombo vya habari vyenye idadi kuuubwa ya makanjanja na waliokimbia umande zimepita.
We jiulize, hizi ghilba, kubeba silaha kweupe, kupeleka polisi maalum, kuhamishia Wabunge wooote kule, kugawa mahindi msimu wa kampeni tu, ni juu ya nini? Wameona maji ya shingo!
Itafika siku hata hizo Media houses zitachoshwa na huo unafiki na wataanza kuisemea jamii.
Wanamageuzi, kazeni buti, Wananchi wameeshajua, mbivu ni ipi, na mbovu ni ipi pia.
 
Hata pasingekuwepo na hizo takataka mnazoziita vyombo vya habari hapo Igunga bado CDM wanatoboa tu kwasababu tokea awali makanjanja wamepewa ubwabwa na bado mziki wa CDM unawaunguza..walipewa 35ml wakale pilau
 
Ziara za Nape kwenye vyombo vya habari. Vyote vimeufyata. Solution ni CHADEMA (na vyama vingine vya upinzani) kuwa na vyombo vyake wenyewe. TBC tunaijua wanafuata amri ya mwajiri. Uhuru inajulikana. IPP Media huwa ni kigeugeu. Mwelekeo wao unategemea hali ya maslahi ya mmiliki kwa wakati huo. Star TV ni ya Gamba. Clouds TV ni ya maswahiba wa mkuu wa kaya. Vingine ni vya mafisadi waliokubuu. Juzi nilimuona waziri Nchimbi akiwa AGAPE. Sasa hivi wanahaha kuhakikisha vyombo vyote vinakuwa upande wao. Wanajifanya wastaarabu lakini ujumbe wanaoufikisha ni 'usipokuwa nasi wewe ni adui yetu. Tutakushughulikia'.
 
Bora hizi media zisingekuwepo. Zinapotosha mambo. Chadema mbele kwa mbele, mwishoni wataachia tu.
 
Kuanzia kampeni za lgunga zianze sijaona Tv wala Sijasikia redio ikiripoti kiufasaha juu ya mikutano ya kampeni ya Chadema lgunga.
Tatizo ni nini? Je Tv na redio nyingine zimesha lamba pilau, tshirt na kapelo za bure au Chadema haibebeki na hailipi?

Kuna taarifa kuwa Mkuu wa kaya aliwaita akawalaumu sana kwamba wametoka mbali lakini wamekuwa wanamuweka kwenye mazingira magumu ya kutawala nchi. Ndio maana nasema cdm waanzishe TV na redio yao. Nna uhakika itabamba sana we acha tu
 
Hata kenya ilkuwa hivy hivyo wakati kibaki anachuana na katotot ka kenyata. KBC hadi dk za mwisho walikuwa upande wa serikali tawala ya wakati huo. Mpaka walipokuja kuambiwa upinzani unachukua nchi ndo wakaanza kupeleka hewani matukio ya kina odinga na kibaki
 
Ziara za Nape kwenye vyombo vya habari. Vyote vimeufyata. Solution ni CHADEMA (na vyama vingine vya upinzani) kuwa na vyombo vyake wenyewe. TBC tunaijua wanafuata amri ya mwajiri. Uhuru inajulikana. IPP Media huwa ni kigeugeu. Mwelekeo wao unategemea hali ya maslahi ya mmiliki kwa wakati huo. Star TV ni ya Gamba. Clouds TV ni ya maswahiba wa mkuu wa kaya. Vingine ni vya mafisadi waliokubuu. Juzi nilimuona waziri Nchimbi akiwa AGAPE. Sasa hivi wanahaha kuhakikisha vyombo vyote vinakuwa upande wao. Wanajifanya wastaarabu lakini ujumbe wanaoufikisha ni 'usipokuwa nasi wewe ni adui yetu. Tutakushughulikia'.

Mkuu kina baadhi ya vyombo vya habari vya dini haviingiliki hata kwa mtutu
 
Hawafanyi mikutano! Wao ni wanamagwanda kazi yao ni kufanya uhuni tu, sasa unataka TV ziripoti uhuni?

Uhuni unaousema hapa ni upi ambao vyama vingine haviufanyi isipokuwa CDM tu? Acha uonevu wako mkuu.
 
Back
Top Bottom