Kwanini tuwanyime kura wapinzani oktoba 31? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini tuwanyime kura wapinzani oktoba 31?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by saider, Oct 14, 2010.

 1. s

  saider New Member

  #1
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama inavyofahamika kuwa watanzania wote wazalendo tutajumuika kwa pamoja katika kuchagua viongozi wetu watakaotuongoza na kututumikia kwa miaka matano ijayo 2010-2015 lakini sasa swali kubwa linaloniumiza kichwa mpaka je watanzania wenzangu tunautambua mchango wa serikali iliyopita maana kuna propaganda nyingi za kisa ambazo baadhi ya vyama vya siasa zinazitumia katika kutufumba macho watanzania na wengine wanadiliki mpaka kututukana kama sio kutuvua nguo kwa kile wanachodai kuwa toka zama za uhuru wetu mpaka sasa nchi yetu haijapiga hatua yoyote ya maendeleo kweli jamani?ina maana mabadiliko ya nyanja mbalimbali nchini mwetu hatuyaoni?au ina maana wanatuona sisi kama majani makavu tu tunapeperushwa na upepo hatujielewi hata chepe jamani wakisema tusiache kuwasikiliza katu tuwasikilize kama kawaida ila baadae tukae chini na kupembua hizo sera zao wasemazo je kweli zitasaidia?zinalenga kutujenga na kutuimarisha au kutubomoa? na kwanini wasiweke wazi basi japo robo ya mema yaliyofanywa na serikali iliyopita?jamani hawa watu wanataka wao ni kututawala tu lakini sio kutupa maendeleo wana uchu na uongozi na wala sio nia ya kutuongoza jamani ni mengi yamefanywa na yanaendelea kufanywa siku hadi siku napenda kukiri wazi wazi kuwa mimi kama mtanzania bado nina imani kubwa na serikali ya CCM kwa yale ambayo wameyaonyesha katika Tanzania huru natumaini na kuamini ni mengi yanafuata kwasababu waliahidi wametimiza mengi na mengine yanaendelea kufata utekelezaji siku hadi natamani kuiona Tanzania ya baada ya 5 ijayo namuomba MUNGU anifikishe ili hata wale wanaipinga serikali ya sasa watafute lengine la kuzua ila jamani oktoba 31 tusitetereke hata kidogo kura zaidi kwa ccm maendeleo stahiki ya Tanzania endelevu
   
 2. M

  Maluo Member

  #2
  Oct 14, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  imenisikitisha sana kupoteza muda kuandika kuwa ni maendeleo yaliyofanywa kwa sera za kulipa fadhila na kuteuana kwa kuwa umekosa kwenye ubunge je kuna uhalali gani wa kumpa Nape Nnauye ukuu wa wilaya ana nini alichafanya cha ziada zaidi ya watanzania wengine JK aliseme atajitahidi kuwapa kipaumbele wale waliopo serikalini wakati akifanya teuzi mbali mbali mimi nataka kujua hata kauli yake imeshinda anateua mtu nje ya wafanyakazi wa serikali sasa mtu huyu ataweza kufanya maamuzi ama atakuwa na kazi ya kutizama mkuu anataka nini hili ni sawa na kauli ya waziri mkuu mstaafu aliposema kuwa mtu akichaguliwa kwa rushwa hawezi kuwa kiongozi wa wananchi wa kawaida italazimu atimize matakwa ya akina Mramba, Lowassa na chenge kwani wote hawa kawapa sifa lukuki alipowaombea kura katika majimbo yao je nalo hili unahitaji kuchagua ufisadi ama na wewe ni mmoja katika waliofaidika na ufisadi huo

  kwa maana ukiona mtanzania yeyote mwenye uwezo wa kuona na kutafakari kwa makini lakini bado anashabikia CCM ni kuwa uwepo wa system husika inapa faida kubwa kuliko kinachofanywa katika kuliendeleza taifa kwa ujumla na kama upo kwa ajili ya nini CCM inakufanyia endelea kuipa shavu kama unahitaji kuona maendeleo yenye kujitosheleza achana na CCM haina sera dira wala mwelekeo alishasema hayati kolimba
   
 3. m

  mzalendo2010 Member

  #3
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa Mtanzania yeyote mwenye akili timamu, mwenye macho na masikio yanayofanya kazi atajiuliza kitu kimoja tu, Je kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita 2005-2010 serikali imefanya jambo gani ambalo ni visible as far as development is concerned?
  Katika sekta ya elimu, wakati mwl Nyerere anaondoka madarakani asilimia ya wananchi wasio jua kusoma na kuandika ilikuwa ni 9% leo hii imefikia 30%, katika afya je ni kipi kimefanyika ili kuboresha sekta hii? kama sio politiki za yule ndege wake aitwae ng'ong'ona, Well katika sekta ya miundombinu hali ni mbaya....Miaka 50 ya uhuru, Kigoma/Tabora/Mpanda na sehemu kibao hapafikiki....umeme ni tatizo Kigoma/Ruvuma etc..etc...Thamani ya shilingi imeendelea kudorora...nakumbuka early of nineteens dola moja ya kimarekani ilikuwa ni sawa na Tshs 180 leo hii ni sawa na shs 1600, Thamani ya shilingi imeanguka mweleka wa mende Tangu JK aanze...mwaka 2005 1 USD ilikuwa ni sawa ni TSHS 1050 leo hii hali si hali, Ameua Shirika la reli kwa manufaa ya kuchota pesa, serikali inaongozwa na wafanya biashara, tumeshuhudia Serikali inaweka kapuni maazimio 23 ya Bunge, hakuna uwajibikaji, ufisadi katika sekta ya madini, Ukifika shinyanga ni kilio tupu, mkoa uliobarikiwa kuwa na madini ya kila namna lakini umasikini umeota mizizi......Jamani Serikali itajitetea kwa lipi? Serikali imeoza, Ikulu imegeuzwa kuwa pango la wanyang'anyi......Tafadhali iwapo kuna yeyote aliyeona jambo lililofanywa na serikali ya SISEM 2005-2010 amwage point.... Naamini kwa rasilimali tulizonazo hatukustahili kuwa na hali hii ya umasikini, rejea tangazo la Policy Forum, we are tired of SISIEM, we need change, tusiwe bendera kufuata upepo na ndio maana wagombea wa SISIEM wamekimbia mdahalo wa kampeni......
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 9,810
  Likes Received: 566
  Trophy Points: 280
  Nani apigie kura Chama Cha Wahindi?
   
 5. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,330
  Likes Received: 3,535
  Trophy Points: 280
  Kama unataka kuitumia JF kujipendekeza huko kwa walio kutuma umeliwa, hapa tupo great thinkers vi hoja dhaifu kama vyako hazitushawishi. Kwanza umeshindwa kutuambia specifically ni nini hasa hiyo serikali unayoipigia debe imefanya na kuishia kuongelea kijumlajumla tu bila kuwa na data. Najua we umeshauiriwa kuingia JF ili kuongeza kura za JK ktk opinion poll huna lolote jipya. Kufanya mazuri ni kutimiza wajibu, hakuna kusifiwa kwa hilo kwa kuwa mnalipwa mishahara, Ukitaka kusifiwa kwa mazuri ni hadi ukifa. Kwa sasa tutakosoa kila baya lililofanywa na JK ikiwemo kukumbatia majizi na mafisadi.
   
 6. pons

  pons Member

  #6
  Oct 14, 2010
  Joined: Sep 8, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mamluki huyo aogopwe kama ukoma..
   
Loading...