Kwanini tutumie katiba mbovu kutengeneza katiba nzuri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini tutumie katiba mbovu kutengeneza katiba nzuri?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by naggy, Nov 19, 2011.

 1. n

  naggy Member

  #1
  Nov 19, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 15
  Mimi si mtaalamu wa sheria lakini napata wasiwasi kwa kutumia ufahamu wa kawaida. Kuna uhalari gani wa kurejea kwenye vifungu vya katiba ambayo sote tumeiona haifai, kutengeneza katiba itakayokidhi matakwa ta wananchi? Ni kweli, kwa mujibu wa katiba ya sasa rais ana mamlaka makubwa sana na ni halari kwa yeye kufanya kama mswaada uliopitishwa unasema. Lakini tukumbuke hatuwezi kutumia malighafi mbovu, iliyooza, isiyo na ubora, kutengeneza bidhaa bora. Kwamba haramu haiwezi kuzaa halari hata siku moja. Sote hili tunalifahamu, wanaccm wanalifahamu, hata rais pia analifahamu. Halihitaji mtu awe na elimu ya chuo kikuu, just logic- simple reasoning. Hata sisi tunaoupinga huu mswaada wa mchakato wa kupata katiba mpya hatujaliweka wazi hili katika kutetea hoja zetu. Nahisi hili tulitumie kutetea hoja zetu za kuupinga mswaada unaotegemewa kusainiwa. Mchakato huu ulipaswa uwe huru kabisa, tukitumia matakwa ya wananchi kama ndo mwongozo wa kutengeneza mchakato, na si katiba na taratibu zilizopo.

  Swala la mamlaka makubwa ya rais ni swala moja kubwa linalopigiwa kelele kwenye katiba ya sasa. Na kwamba katiba mpya tunayotegemea kuiunda hakika hatutegemei rais awe na mamlaka makubwa kiasi hicho. Tukikubari rais atumie mamlaka makubwa aliyonayo katika mchakato huu, kuna hatari ya kupata katiba ambayo haitakuwa na tofauti sana na iliyopo. Kwamba, ingekuwa ni bora zaidi kufanya marekebisho ya katiba kwa baadhi ya vifungu kuliko kutumia gharama kubwa kwa kufanya kiini macho cha kukidhi haja ya wananchi ya kutaka katiba mpya. Napatwa na wasiwasi kwamba rais wetu, mawaziri wake na wabunge wake wote, kama kweli wanadhamira ya kweli ya kuunda katiba mpya. Nahisi wanataka kufanya kiini macho tu. Kulikuwa na tatizo gani mswaad huu kuusoma kwa mara ya kwanza? Kuna tatizo gani la kuwaacha wananchi wao wenyewe waamue namna ya kupata katiba mpya? Kwa nini wabunge wa ccm wameshupaa kuutetea? Nalazimika kuamini kwamba kuna ajenda ya siri hapa tunayopaswa kuipinga kwa pamoja.

  Lakini ndo hivyo, wamepitisha, na rais kasema atausaini katika hotuba yake jana akiongea na wazee wa Dar es Salaam. Swali muhimu la kujiuliza TUTAFANYAJE KUZUIA HIZI NJAMA ZA SERIKALI KUUTEKA MCHAKATO WA KUPATA KATIBA MPYA? KILICHOAMULIWA KUFANYWA NA JUKWAA LA KATIBA NA WANA CHADEMA NA NCCR KITAFANIKIWA? KISIPOFANIKIWA TUTAFANYAJE? Kwa jukwaa la katiba na vyama vya upinzani(CDM na NCCR) TUNAFAHAMU AINA YA WATANZANIA TULIO NAO AMBAO NDIYO MTAJI WA KUFANIKISHA HAKI AMBAYO WENGI WANAITAKA (PEOPLES' POWER)? Tusaidiane kwa haya.

  Nawasilisha!
   
 2. P

  Paul J Senior Member

  #2
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe umeyaona hayo kama wengine tulivyo yaona.Kwa mfumo uliopo sasa wa watu wasiotaka kukubali ukweli badala yake wanatanguliza maslahi binafsi na ya chama chao, katiba ya kukidhi mahitaji ya taifa la leo la Tanzania na la siku za usoni itakuwa ni mwendelezo wa usanii kama ilivyo safu ya viongozi wasanii. Huwezi kuhalalisha uundwaji wa mchakato wa katiba mpya kwa kusema eti wao walifanya hivyo, nami nafanya hivyo! Ikumbukwe kwamba madai ya katiba mpya yamekuwepo kwa sababu ya mapungufu makubwa na ya kimsingi yaliyopo katika katiba iliyopo na kama tukiitumia katiba hiyohiyo kuhalalisha mswada wa uundwaji wa katiba mpya, basi wanaofanya hivyo watakidhi kiu yao ya sasa lakini si kiu ya watanzania na kizazi cha kesho. Kwa kutumia katiba hii iliyopo watawala wameweza kuwachagulia wananchi viongozi, upige kura usipige ccm ikisema huyu ndiye rais na atakuwa! rasilimali zetu zinaporwa kila kukicha sababu ya hii katiba mbovu isiyoweza kumwajibisha mkuu wa nchi kwa kushindwa kutetea maslahi ya taifa,ufisadi mkubwa na wa kutisha unaendelea kila sehemu, bado wanasema katiba inawapa mamlaka hiyo na ukweli uko hivyo, iweje leo hii waseme wanayo nia ya kweli ya kutupatia katiba mpya yenye kulenga kutetea maslahi ya taifa na watu wake? Msimamo wangu katika hili ni kwamba sitegemei katiba nzuri ya kukidhi matakwa ya kizazi kilichopo na kijacho na taifa lenye ustawi chini ya utawala huu wa kiimla!Hata kama itatungwa, muda si mrefu tutakiwa kutunga katiba ya WATANZANIA WA LEO, KESHO NA MIAKA HATA MIA IJAYO. KATIBA YA UTAWALA WA SASA INALENGA KUIMARISHA NA KULINDA MASLSHI YA CHAMA TAWALA IKIWA NI PAMOJA NA MWENDELEZO WA KUICHAGULIA TANZANIA RAISI. TUIPINGE KWA NGUVU ZETU ZOTE
   
 3. CtVKiLaZA

  CtVKiLaZA JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hilo ndilo swali langu hasa kwa wanasheria? Kwa nini wanaendelea kutumia vifungu vya katiba ya zamani kutuletea katiba mpya?
  Labda kama katiba inaboreshwa.
   
Loading...