rodgers123
Senior Member
- Jul 12, 2015
- 159
- 125
Ndugu Watanzania,
Nimejaribu kufatilia nchi yetu na kuona kuwa miradi mikubwa inayofanyika au inayotarajiwa kufanyika tunategemea zaidi pesa kutoka nje ya nchi kama mikopo au wawekezaji.
Leo ninataka kujikita zaidi kwenye neno wawekezaji ili nitowe mawazo yangu kwa nini sisi watanzania tusijenge kwa pesa zetu wenyewe.
Ndugu watanzania wawekezaji wengi wanaokuja kuwekeza nchi mwetu wengi wao pesa wanazokuja kuwekeza sio pesa zao.Pesa zinaweza kuwa:
1. PESA ZA RAIA MBALIMBALI TOKA NCHI HUSIKA
Makampuni mengi yanakuja nchini mwetu yana sign mikataba kwa kuaminisha Serikali kuwa tunakuja kufanya au kuwekeza kwenye hiki kitu. Na baada ya kukubaliwa na ku sign mkatamba, makampuni haya hurudi kwao na kuanza harambee ya kutafuta capital ili ianze kazi.
Harambee hii inaweza kuwa kuchukua loan au kufanya joint na makampuni mengine ili kuja kufanya
uwekezaji. Hapa nina maana kuwa kwa sababu imeshapewa deal nono na wao wanaenda kuuza kipande cha deal kwa kutafuta joint kampuni ya kufanya nao uwekezaji. Na wanafanya hivi wakijua kuwawatapata faida kubwa sanaa.
MFANO:
Tumeona miaka michache iliyopita Maeneo ya Rukwa pamegundulika reserve kubwa ya gasi ya Hellium. Na gasi hii ni miongoni mwa gesi ambayo inatafuta nakutumika kwa wingi na nchi nyingi duniani.
Sasa amekuja muwekezaji akaomba kuchimba hiyo Hellium na serikali ikakubali ikijua kampuni hiyo ina pesa tayari mkononi za kuja kuwekeza.
Lakini ki ukweli baada ya kampuni kupewa deal na serikali. Na wao wamerudikwa na kuanza kutafuta watu kukusanya pesa ili kwa pamoja waje kuwekeza.
Kampuni inaenda kuji register kwenye Stock Market na kuuza hisa kwa watu mbali mbali ili kupata capital ya kuja kufanya uwekezaji kwa kutumia habari kuwa tumeshapewa deal la kuchimba Hellium na story zingine za kutamanisha wanunua hisa. Mfano article hii inaonyesha kampuni iliyopewa deal la kuchimbaHelium wanafanya harambee kukuza pesa za kuja kuwekeza.
Wanafanya hivi baada ya ku sign deal {The company was looking forward in raising £4 million ($5.31 million) of capital from the London bourse to fund the project.}
Sasa kwanini baada ya kampuni kupata deal ndio wanatafuta njia ya kupata mtaji?
Tumeona pia kampuni zinaweza kuja nchini mwetu kusema tunataka kuwekeza kwenyekujenga miundo mbinu hii. Lakini baada ya kupata kibali serikalini kampuni inarudi
nchi husika na kupewa pesa toka Serikali ya nchi husika.
Mifano mingi ya kampuni toka china. Kampuni nyingi za China zipo chini ya Serikali au zina mkono wa serikali. Zinaweza kuja kusema tunakuja kuwekeza kwenye hili. Kumbe nyingi huenda kuwa zimetumwa na Serikali yao. Wakishapata deal basi hurudi
na kupewa pesa na serikali. Na lengo kubwa ni kupata faida na kuweza kupata mengineyo kama nchi husika ikishindwa lipa au pata faida kwenye kitu walichowekeza.
Sasa Watanzania wenzangu kwa nini serikali yetu isipige hesabu pesa ambazo zinahitajika kujenga mfano bandari ya Bagamoyo. Ikaaanza uza hisa ili kwa asilimia kubwa tujenge watanzania wenyewe. Na faida tuweze gawana watanzania wenyewe kuliko ku risk kukopa au kuomba mtu wa nje aje atujengee.
PENDEKEZO:
Jamani huu ni mtazamo wangu.
Kuna mahali naweza kuwe nimekosea mnisamehe. Ila lengo ni tutafute jitihada za kujenga Bandari kwa pesa yetu wenyewe kwa serikali kuelimisha umma na kuanza kuuza hisa.
Natanguliza shukrani,

- Pesa za raia wa nchi husika au mataifa husika ambazo wanachanga ili kupata pesa za kuja kuwekeza.
- Pesa za serikali toka nchi husika ya wawekezaji.

- Kwa nini serikali yetu isihamasishe watanzania kwa kutoa elimu bora kuhusu uwekezaji pamoja na kutangaza kwenye vyombo vya habari ili watanzania wenyewe tuwezi kununua hisa na serikali ikapata mtaji wa kununua mitambo ya kuchimbia..?
- Je kwa nini miradi kama Bandari ya Bagamoyo serikali isianze kuhamasisha watanzania na wakaanza kununua hisa ili serikali ikapata mtaji na kuweza kujenga Bandari kwa pesa zetu wenyewe. Japo hata 75% ya gharama zote zikatoka kwa Watanzania
Tumeona pia kampuni zinaweza kuja nchini mwetu kusema tunataka kuwekeza kwenyekujenga miundo mbinu hii. Lakini baada ya kupata kibali serikalini kampuni inarudi
nchi husika na kupewa pesa toka Serikali ya nchi husika.
Mifano mingi ya kampuni toka china. Kampuni nyingi za China zipo chini ya Serikali au zina mkono wa serikali. Zinaweza kuja kusema tunakuja kuwekeza kwenye hili. Kumbe nyingi huenda kuwa zimetumwa na Serikali yao. Wakishapata deal basi hurudi
na kupewa pesa na serikali. Na lengo kubwa ni kupata faida na kuweza kupata mengineyo kama nchi husika ikishindwa lipa au pata faida kwenye kitu walichowekeza.
Sasa Watanzania wenzangu kwa nini serikali yetu isipige hesabu pesa ambazo zinahitajika kujenga mfano bandari ya Bagamoyo. Ikaaanza uza hisa ili kwa asilimia kubwa tujenge watanzania wenyewe. Na faida tuweze gawana watanzania wenyewe kuliko ku risk kukopa au kuomba mtu wa nje aje atujengee.
PENDEKEZO:
- Serikali ipitie gharama ya kujenga hiyo Bandari ya Bagamoyo upya maana kama muwekezaji ndio ametoa hiyo gharama lazima atakuwa ame i over estimate(kaweka gharama kubwa). Alafu ianze kuuza hisa kukuza mtaji ili tuje kujenga japo kwa asimilia 75% kwa pesa zetu watanzania kwa ujumla. Na kila mtu atakuja pata faida kadri biashara itakavyokua. Kwani risk ya Wachina kuja kujenga, wachina mbali na kutumia Bandari nk. Wachina wengi na watapewa hayo maeneo ya viwanda na kufanya kama store ya kuweka bidhaa zao kuanza kuuza sio Tanzania tuu bali nchi jirani za Afrika. Hivyo wataua masoko mengi sana maana kila mtu atafunga safari kwenda kununua biadhaa hapo ndani. Na sijui kama wakiuza mzigo nje ya nchi TRA itapata chochote. NB: Kumbuka pesa zitatoka serikalini hivyo kuna risk kubwa ya kupoteza eneo kama kwa muda wote huo wawekezaji wakashindwa kurudisha pesa zao
- Ili kufanikisha uuzaji wa hisa serikali inabidi ichukue hatua kali kwa viongozi watakaofuja pesa hizi ambazo wananchi watachanga kwa ajili ya Ujenzi wa Bandari. Ili kuonyesha seriousness ya kufanikisha ujenzi huu.