Kwanini Tundu Lissu anafaa kuwa rais wa TLS?

BAKOI

JF-Expert Member
Jan 31, 2016
1,211
2,328
KWA NINI TUNDU LISSU NI CHAGUO SAHIHI TLS?
Nimekua katika mazingira ya kuambiwa kila uchao kwamba ili nchi iendelee inahitaji mambo manne: watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Kauli mbiu hiyo ilitoka kinywani mwa Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere na kisha ikapalizwa kila mahali.

Toka nimesikia kali hiyo kwa mara ya kwanza nikiwa bado mtoto mpaka leo sijaona maendeleo tuliyotarajia kuyapata. Nimebakia na maswali mengi hivi ni nini kilichokosekana katika hayo manne aliyoyataja Mwl. Nyerere?

Hebu chunguza mwenyewe je hatuna ARDHI? Hatuna watu WATU? Je vipi kuhusu SIASA SAFI? Na pia vipi kuhusu UONGOZI BORA? Naamini iwapo utaipa akili yako kazi kidogo basi itakujibu kwamba yanayokosekana hapo ni hayo mawili ya mwisho.

Labda kama tumekubaliana kwamba tunachokikosa ni SIASA SAFI na UONGOZI BORA sasa twende kwenye ufumbuzi badala ya kulalamika na kulialia kila siku, na ufumbuzi utakuwa ni mmoja tu: kuwakubali watu wenye mawazo mpya ambayo ni chanya.

Nimemsikia Tundu Lissu miaka mingi toka akiwa LEAT yaani wanasheria wa mazingira, na issue kubwa iliyomuibua kulingana na kumbu kumbu zangu ni HAKI ZA BINADAMU ikihusu kufukiwa kwa watu huku wakiwa hai huko Kahama mwaka 1996 (miaka 21 iliyopita).

Wahusika wakuu wa ufukiaji huo walikuwa ni Waziri wa Madini na Nishati kwa wakati huo, Dk. William Shija (kwa sasa amefariki) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa wakati huo Tumainiel Kiwelu.

Binafsi nina ushahidi wa dhahiri kwamba huko kuna watu walifukiwa wakiwa hai na walifariki. Ushahidi wa kwanza nina mikanda ya video ya miili ya watu ikfukuliwa baada ya kufukiwa na katapila baada ya amri ya mkuu wa mkoa saa mbili kabla ya zoezi zima la fukia fukia.

Pili ni kwamba mwaka huo huo 1998 niliongea na afisa wa Ikulu aliyetumwa kumhunguza Dk. Shija kwa nini alikuwa anachukiwa sana na wapiga kura wake Sengerema (ndilo jimbo langu pia). Afisa huyo alimkabidhi ripoti yake Rais Mkapa na kuanika mambo mengi kama ifuatavyo:

Shija hakupenda kabisa kukosolewa, alikuwa ni mkatili na pia alipandikiza mbegu za ukabila kati ya Wazinza na Wasukuma jimboni kwake na katika wilaya nzima ya Sengerema.

Mpaka leo upo usemi wa kichochezi (abazinza twimanye tulibache) ukimaanisha kwamba Wazinza tupendane kwa sababu tupo wachache(mimi ni Mzinza kwa kabila). Usemi huo ulilenga kuwafanya Wasukuma ambao ni wengi katika wilaya hiyo kuwachukia Wazinza ambao ni wachache.

Lengo hasa ikiwa ni kumshinda katika uchaguzi Dk. Fortunatus Masha ambaye pia ni Mzinza. Mungu ni mwema Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa wakati huo Mzee Philip Mangula ambaye kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho na ambaye aliwahi kufanya kazi kama Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza alizipinga vilivyo siasa hizo za ukabila.

Kulingana na taarifa za afisa yule wa Ikulu Mzee Mkapa alipokabidhiwa ripoti na kuisoma alisema mambo mawili: “Nimepata taarifa nyingi juu ya tabia mbaya za Dk. Shija, pia nimearifiwa kwamba ni mtu mkatili sana.”

Na akamalizia kwa kusema “ni kweli alitoa amri ya kufukiwa watu wakiwa hai Kahama ndiyo maana nilimuondoa Wizara ya madini na Nishati nikamhamishia Wizara ya Viwanda na Biashara, tutamsaidia ashinde ubunge lakini kamwe sitampatia tena uwaziri.”

Hayo yalikuwa maneno ya Mzee Mkapa katika kile kinacoitwa ‘classified information’ yaani SIRI KUBWA ZA SERIKALI. Twende mbele turudi nyuma tunaona kelele za Tundu Lissu katika kulaani mauji hayo na kutaka waathrika walipwe fidia zilikuwa na maana kubwa kwa taifa hili.

Ndiyo maana binafsi naona kwamba Mhe. Tundu Lissu anastahili kupewa dhamana ya kuiongoza TLS ikiwa ni katika azma ya kuleta UTAWALA BORA na kwa mantiki hiyo kuunga mkono kauli mbiu ya Mwl. Nyerere kwamba miongoni mwa mambo manne ya kuleta maendeleo mojawapo ni UONGOZI BORA!

Sitaki kabisa kujiingiza katika mijadala ya kumtambua Tundu Lissu kama mwana-CHADEMA, mbunge au mwanasiasa kwa sababu hoja yangu hapa ni HAKI ZA BINADAMU na wala siyo siasa.

Iwapo kuna mtu andhania nimeandika makala hii ili kuwachafua watu basi nitakuwa tayari hata kuufikisha mahakamani mkanda wa video wa Mkuu wa Mkoa kiwelu (uliopigwa marufuku na serikali) akiwafukuza watu wawe wameondoka ndani ya mgodi katika kipindi cha saa mbili, na yanayomhusu Dk. Shija jisomee mwenyewe hapa: Serikali kumlipa fidia baba wa Waziri Masha
Na hapo tena: Kutoka kuvuna dhahabu hadi ufukara wa milele | Gazeti la MwanaHalisi

Muwe na mapumziko mema Jumapili ya leo…

Na Eliasi Mhegera
 
Back
Top Bottom