Kwanini Tundu Lissu alikuwa anapata watu wengi kwenye mikutano yake ya kampeni hasa mikoani?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Hili swali unaweza kulidharau lakini ni la msingi sana hasa kwa sisi wana CCM kindakindaki.

Ni nini hasa kiliwavuta watu kwenye mikutano ya Tundu Lisu?

Je, ni huruma sababu alipigwa risasi nyingi?

Je, ni uwezo wake wa kutoa uongozi?

Je, ni mapenzi ya wananchi kwa Chadema?

Au ni watanzania wanataka mabadiliko CCM imewachosha?

Naomba maoni na mtazamo wenu Tafadhali!
 
Wananchi wengi hata wale CCM kindakindaki, Kanda ya Ziwa na wasomi tulimuunga mkono Tundu Lissu chinichini kwasababu alikuwa anapambana na adui namba moja wa taifa letu. Kiongozi huyu aliwahi kufanya uhaini mkubwa dhidi ya Jamhuri ya Muungano na mikono yake ilikuwa imejaa damu na vilio vya mamilioni ya watanzania wasiokuwa na hatia..
 
Kwanza Watu wengi walikuwa na ham ya kumuona Lissu laiv baada manyang'au wa ccm kutaka kumuaa

Pili ni uwezo wake wa kupangilia hoja zilizoshiba zilizokuwa zinatoa mwanga wa maisha bora kwa wananchi

Tatu, ni ukweli usiopingika watu wengi hawakuwa wanampenda mwendazake kutokana na ukatili wake....

Yapo mengi sana, Usisahau Lissu ni mbeba maono....
Na ccm haina jipya kwa Watanzania
 
Hili swali unaweza kulidharau lakini ni la msingi sana hasa kwa sisi wana CCM kindakindaki.

Ni nini hasa kiliwavuta watu kwenye mikutano ya Tundu Lisu?

Je, ni huruma sababu alipigwa risasi nyingi?

Je, ni uwezo wake wa kutoa uongozi?

Je, ni mapenzi ya wananchi kwa Chadema?

Au ni watanzania wanataka mabadiliko CCM imewachosha?

Naomba maoni na mtazamo wenu Tafadhali!
Anajua kujenga hoja n nini cha kuongea,meko n wenzake walikua wanaropoka na kusema ahadi za uwongo mwanzo mwenga
 
Hahahaha ukienda kwenye mikutano yote ya CCM wanamuongelea Lissu, Mbowe na Lema. Hata juzi kwenye uchaguzi mdogo Buhigwe na wewe pia hapa unaizungumzia CCM kwa mgongo wa Lissu.

Sasa wananchi wataachaje kuwa na mapenzi kwa mtu anayezungumziwa na kila mtu??
Learn to mind your own business
 
Watu wengi ni watu wangapi?

TAnzania tuna watu zaidi ya 60m, wakijitokeza kwenye mkutano watu elfu 5 unaweza kusema wengi.
 
Hahahaha ukienda kwenye mikutano yote ya CCM wanamuongelea Lissu, Mbowe na Lema. Hata juzi kwenye uchaguzi mdogo Buhigwe na wewe pia hapa unaizungumzia CCM kwa mgongo wa Lissu.

Sasa wananchi wataachaje kuwa na mapenzi kwa mtu anayezungumziwa na kila mtu??
Learn to mind your own business
Kwahiyo wewe una mapenzi na mtu anayezungumzwa na kila mtu!
 
Kwanza unatakiwa uelewe kuwa Tanzania hii tungekuwa na viumbe hai aina ya Lissu 8 tu nahisi Singapore tungeikaribia japo kidogo kwa maendeleo, lakini kumbuka kuwa kuwa wakiwepo watu 10 bungeni Kama Lisu wanatosha kabisa hatuhitaji bunge la watu 300 na ushee ila hakuna kinachoendelea.

Lisu alizaliwa tofauti na huenda tukitafuta watu wa aina yake Tz hii tukaishia kumuona yeye tu, tukiweka akili zetu pembeni za vyama na ujinga mwingine Lissu ni hazina nyingine ambayo Mungu ametupa watanzania ila hatujui kuzitumia, laiti watu wangekuwa wanajua thamani ya watu katika taifa lao Basi Lissu angetutoa mahali na kutuweka sehemu nyingine na huenda angeweka record ya dunia kuwa na vitu adimu kichwani mwake.

Mungu mtunze mhifadhi ulimleta kwa maksudi japo bado hatulijui kusudi la wewe kutupa huyu kiumbe Lissu.
 
Hili swali unaweza kulidharau lakini ni la msingi sana hasa kwa sisi wana CCM kindakindaki.

Ni nini hasa kiliwavuta watu kwenye mikutano ya Tundu Lisu?

Je, ni huruma sababu alipigwa risasi nyingi?

Je, ni uwezo wake wa kutoa uongozi?

Je, ni mapenzi ya wananchi kwa Chadema?

Au ni watanzania wanataka mabadiliko CCM imewachosha?

Naomba maoni na mtazamo wenu Tafadhali!
Wengi walijitokeza kumuona mtu aliyetoka mautini na kuwa tena hai....
 
Wananchi wengi hata wale CCM kindakindaki, Kanda ya Ziwa na wasomi tulimuunga mkono Tundu Lissu chinichini kwasababu alikuwa anapambana na adui namba moja wa taifa letu. Kiongozi huyu aliwahi kufanya uhaini mkubwa dhidi ya Jamhuri ya Muungano na mikono yake ilikuwa imejaa damu na vilio vya mamilioni ya watanzania wasiokuwa na hatia.
Majibu mazuri sn
 
1622276586986.png
 
Back
Top Bottom