Landson Tz
JF-Expert Member
- May 8, 2011
- 295
- 221
Ni muda sasa unaendelea kupita tangu baadhi ya watu wakiwemo viongozi hasa wabunge wakijitokeza hadharani na kutoa kauli za kuvunja katiba bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria.
Wabunge wa bunge lilipita wakiwemo na hata hili la sasa wanajitokeza kwenye vikao vya bunge na kutaka kumshawishi na wengine wanatamani kumlazimisha Rais wetu kuvunja katiba ili kutawala mihula zaidi ya miwili.
Ikumbukwe kuwa machafuko mengi yanayotokea Afrika yanatokana na watawala kung'angania (wengine wanaita kung'ang'anizwa) madaraka.
Kazi anayoifanya Rais wetu ni nzuri lakini akimaliza muda wake hatuta shangaa anapatikana Rais mwingine ambaye anaweza kufanya mazuri zaidi ambayo hata Rais mwenyewe atafurahi kuya shuhudia.
Kutokana na mfumo mzuri wa kutawala kwa mihula miwili, mmoja baada ya mmoja iliyo asisiwa na baba wa taifa ni mfumo mzuri ambao ni kiwango cha kimataifa tuulinde na kuu heshimu.
Watanzania tuwekeze katika kujenga mifumo imara na si kujenga watu imara, maana watu wa Mungu waliumbwa kwa udongo!!
Naomba nitowe rai kwa wanao kereketwa na kutoa kauli za kuvunja katiba, kuchunga sana mihemuko yao maana taifa likiangamia historia haita waacha salama.
Mwisho: Nashauri serikali, wana harakati na wanasheria wetu kuweka utaratibu wa kuwafungulia mashika watu wa namna hii na kufungulia mashitaka ya kuvunja katiba na hatimaye adhabu kali itolewe ili iwe fundisho kwa wengine!!
Naomba kuwasilisha.