Kwanini tunawaita wazungu waje kuwekeza Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini tunawaita wazungu waje kuwekeza Tanzania?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Shamu, Jan 8, 2009.

 1. S

  Shamu JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Historia inaonyesha tuliwafukuza wazungu baada ya uhuru Tanzania. Serikali ya ujamaa ilivichukua viwanda vyote vya wazungu ili iviendeshe. Haya yalikuwa mawazo ya Marxism written theory, kwamba wazungu (north) wanaziibia nchi maskini (south). Baada ya muda mrefu Ujamaa ukatushinda. Mwinyi alipokuwa rais akaanza na sera za free market capitalism. Sasa kwanini serikali haianzishi viwanda halafu baadaye wakavibinafsisha kwa Watanzania? sasa hivi tunawaita wazungu warudi bongo waje kuekeza. Wazungu kuja kuekeza TZ, ni sawa na kuwaita wakoloni warudi tena kuja kutunyanyasa bongo.
   
 2. P

  PanguPakavu Amy Senior Member

  #2
  Jan 8, 2009
  Joined: Jul 7, 2007
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwa sababu sisi kama sisi hatuwezi kujiendeleza wenyewe.tumejaribu tumeshindwa.
  kwa lugha nyingine,we will fare better with colonisation(ina any form,investors or globalization),than we would by ourselves.
  tuliokuwa tunawaiga,China Cuba,etc didn't fare well in communism hence we will never fare any better.
  too bad we are so weak in mid to start our own establishment or we are too corrupt to monitor our own resources.
  otherwise if you ask most Tanzanians working for Western companies,they would say it's way better than working for a Mzalendo/mhindi company.
  i guess the western folks are just clever.they did it and they are doing it again!!in whole another level in a new definition.
   
 3. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa kuongezea tu maelezo ya Pangu Pakavu, ni kwamba ukuaji wa uchumi unategemea kila mwenye uwezo kuwekeza nchini. Walio ndani ya nchi waendelee kujitahidi kuwekeza na walio nje waje pia. Uchumi huru (Free Market Economy) inataka uwekeza usio na mipaka. Tukiweza kushawishi wawekezaji wa nje kuwekeza nchini, ni dhahiri kutakuwa na ongezeko la mitaji katika uwekezaji wetu. Kwani tunategemea watakuja na mitaji yao, technology mpya, na skills mpya ambazo tunahitaji kuzitumia kukuza uchumi wetu. Inaelekea tangu tuanze kufanya hivyo, maendeleo makubwa (hasa katika uwekezaji wa ndani) yameanza kujitokeza. Wananchi/wafanyakazi wameweza kupata mapato makubwa zaidi. Zaidi ya hayo, pesa za kigeni zinaingia kwa wingi zaidi.

  Nionavyo mimi ni kwamba, wawekezaji wasipokuja nchini, wataalamu wetu watawafuata huko walipo. Mifano ipo mingi ya kurudi/kurudishwa kwa wataalamu wetu kutokana na ajira walizopata nje ya nchi kwa makampuni ambayo yamewekeza nchini. Hii husaidia kuongeza pato la Taifa.
   
 4. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Naomba tafsiri ya neno, "wazungu"? Kama ni watu weupe, je wakina Nadine Gordimer ni wazungu? Unaweza kuwa na mzungu mwafrika? Kama ni watu wa Ulaya basi je nikichukua uraia wa nchi ya ulaya na mimi nakuwa mzungu? Mmarekani anawekwa katika kundi gani? Je Barack Obama ni mzungu? Mjapani tunamweka katika kundi gani? Na wakina Fidel Castro wako katika kundi gani? Nao wazungu?

  Amandla..........
   
 5. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Hii ni mada nzuri na nzito.Mkuu Shamu ni vyema umeileta ingawaje blogu hii haitoshi kuichambua mada yenyewe.
  Mkuu Shamu amegusia siasa na kuichanganya na uchumi, si vibaya maana siasa ndio uchumi wenyewe.
  Socialist economy ya wakati wa mwalimu, baada ya uhuru, ilitilia maanani ya kuwaendeleza watu sana sana katika elimu na kuondoa magonjwa.Mikakati ya kuondoa umaskini ilikuwa katika kugawana kidogo kilichopo na sio kutilia mkazo uzalishaji wa mali kibinafsi.
  Mikakati ya elimu haikuwa mibaya, mtu wa Kagera alisoma Rungwe na mtu wa Tandahimba aksoma Arusha.
  Lazima tukubali kuwa umoja wa kitaifa ulipatikana katika mkakati huo, ikiwa ni pamoja na kuondoa ukanda ,udini, ukabila n.k.
  Kasheshe ilikuja katika uchumi.
  Watu walikazania kugawana umaskini.Viwanda vichache vilivyotaifishwa vilijaza wafanyakazi kupita hata uwezo wa kuwalipa mishahara.Hata vile vilivuyoanzishwa na serikali vilijaza watu kupita kiasi.
  Tatizo likawa viwanda na mashirika hayo yakakosa tija kabisa.Na katika hili hakuna shirika/kiwanda kilichopona, wafanyakazi wakaanza kuviibia na kujichotea kama ni mali zao.Hapakuwepo na uchungu pale maana mali ilikuwa haina mtu.
  Mzee Ruksa akabadili mwelekeo wa uchumi kwa kuingiza ushindani, mwenyewe alisema anafungua madirisha ili hewa nzuri ipate kuingia!
  Ushindani wa wafanyabiashatra ukaanza kuua taratibu mashirika yanayo endeshwa kizembe.
  Hata yale yaliyokuwa yakiheshimika(NBC,BIMA,BORA etc) yaanza kudorora.

  Wakati huo huo wananchi walio wengi wa Tanzania bado walikuwa wakiendelea kulala kwa kutojiingiza kikamilifu katika uchumi.
  Mzee Mkapa kaingia, yeye akayauza kabisa mashirika yote.
  Mimi nafikiri hapa ndio kosa letu lilipoanzia.
  Mawazo ya wanasiasa wengi ni kuwa ili tuendelee twahitaji wazungu,Ni kosa kubwa , tunachohitaji ni mtaji, namna ya kuupata ndio ujanja.
  Kuna viwanda /mashirika mengi yaliyouzwa ambayo sasa yamekuwa magodown/ghala za kuhifadhi mali za wajanja waliyoyanunua mashirika hayo.
  Si kweli kuwa wazungu ndio wataiendeleza Tanzania bali waTanzania wenyewe.Inabidi waTanzania wajiwezeshe kupata mitaji ambayo itatumika ipasavyo kwa maendeleo.Kwa maoni yangu ni aibu kwa Mtanzania aliyejiwezesha kupatamtaji(hata huo usio halali kama EPA) kukata kiu ya umbumbu wa anasa kwa kuagiza magari ya kifahari kama Vogue au Mercedes Benz S Class badala ya kureinvest.
  Hata kabla ya uchumi wa dunia kuzorota bado waTanzania tungeweza kupata mitaji kutoka kokote duniani kwa collateral ya mali iliyopo nchini.
  Vilevile kuna kila sdalili kuwa waTanzania nao wana kiu ya kuwekeza.
  Ule uuzaji wa hisa katika makampuni makubwa kama TWIGA CEMENT na hata megine umeweza kuonyesha kwamba kuna idle capital nchini inayoweza kutumika vizuri, ni uhamasishaji na uhakikisho kuwa fedha ya mwekezaji , hata ikiwa ndigo itarudi na faida.
  Na hili ndio somo kubwa tunalolikosa waTanzania.
   
  Last edited: Jan 8, 2009
 6. mwakatojofu

  mwakatojofu JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pamoja na kuwaita hao wawekezaji (wazungu na wengineo) kwania ya kupata mitaji na mengineyo kama ilivyoelezwa na wengine hapo juu, pia utaalamu wao unatakiwa. hebu kumbuka tulivyowaita wasauzi kuja kuendesha tanesco (japo matokeo yake wengi wanasema si mazuri).
  unaweza kuwa na mtaji lakin ukashindwa kuendesha biashara/kampuni. na hasahasa katika ulimwengu wa leo wa utandawaz. kampun/biashsra yako lazima ujue kuwa itakuwa inashindana na makampuni mengi mengine world wide
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hakuna nchi yoyote duniani iliyojiendeleza kwa kutegemea wageni. Kama hatuna uwezo tuutafute. Kama hatuna elimu tuitafute, lakini huwezi kutegemea mtoka nje aje akujengee. Huyu atakuwa anajijengea tu. Nisieleweke kama napinga uwekezaji, la hasha. Lakini tunahitajiwa wenyewe kushika mpini wa uwekezaji huo.
   
 8. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180

  Mawazo kama haya ni ya kuukubali utwana na kutumika(servitude),swala ambalo linahitaji ukombozi wa fikra .
  Mkuu Pangu Pakavu you have a long way to go!
   
 9. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Habari ndiyo hiyo, wanakuja kujijengea wakinufaika wanaondoka sisi ziii. Tusubiri watatuwekeza hata sisi tukicheza
   
 10. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Lakini kama wageni wanaweza kuleta chachu za maendeleo kwanini wasikaribishwe ???
   
 11. S

  Sahiba JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakubwa tatizo si wawekezaji ni sisi wenyewe tunaowaruhusu hao wawekezaji kuchukua faida kubwa katika huo uwekezaji kwa mikataba feki na isiyo na manufaa kwa nchi na wananchi isipokuwa CCM na mafisadi wake.Hakuna ufisadi mkubwa kama tuliofanyiwa na baba la mafisadi bwana Mkapa wa kujibinafsisha/kuiba mradi mzima wa kiwira.Ni wizi wa kimachomacho katudhulumu wananchi wote wa Tanzania na si serikali kwani serikali inatuwakilisha sisi.Ikiwa wazalendo wanapopata nafasi wanatuibia tena bila huruma na hata hao wawekezaji wa nje wanapokuja pia wanatumiwa na wazalendo wenzetu tuliowaamini kujinufaisha kama ilivyo kwenye miradi ya madini na mikataba yao iliyosainiwa England.Kinachotakiwa ni mapinduzi ya kweli turudi tukachukue nchi yetu bila kujali chama tuwaelimishe wananchi na tuwaongoze katika maendeleo ya kweli na sisi tukiwa ni mifano ya kuigwa na si kulalama pasi na action.SEMENI WANAJAMII WANGAPI MKO TAYARI KUINGIA KAMBINI NA IKIWA MNAOGOPA BASI BORA TUMRUDISHE MWINGEREZA TUJUE MOJA.
   
 12. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu Sahiba unaweza kuwa na analysis nzuri ya tatizo, lakini conclusion yako is dead wrong!
  Sijui kama umepitia hata mgambo weye mkuu!!
  Cheki Congo,Rwanda Burundi na hata jirani yetu Kenya.Mkuu Sahiba mkumbuke shangazi yako aliyeko kijijini ,jamaa, wapinzani wako wakimkog'oli ndo utaelewa uzito wa usemalo.
  Mbaya zaidi kutaka utawaliwe na mwingereza, huna haja ya kumwomba arudi weye nenda kule ukatumike.
   
 13. P

  PanguPakavu Amy Senior Member

  #13
  Jan 13, 2009
  Joined: Jul 7, 2007
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  if you look at the current situation in Tanzania and most african countries you will agree with me.

  Africans were way better economically during Colonisation,especially during 60's and seventies.na kwa zile nchi zilizopata bahati ya kukaliwa na wakoloni hadi eightees(zimbabwe) and 90's(SA).have been leading economies in AFRICA.

  kitu kibaya kinachoendelea sasa hivi africa(tz included).leaders are worse than our masters were,they don't build infrastructures they give away our resources,they act like Godfathers all the way.

  i never liked the idea of colonialism BUT the the truth remains to be seen.

  1.Dar master Plan was last created by british masters,and the only good place to live remains the places they did BUILD!!look at masaki,magomeni,ada estate...,the list goes on.
  2.Shule zetu kubwa za sekondari Tabora boys,Mzumbe,Azania,Tabora girls,Zanaki and soo many..,all of them were built during colonial era!!and now they have only gotten worse in terms of students:teacher ratio etc!
  when you look at schoold that our so called onvestors are building you might
  cry.some vry low quality schoold,no labs no sufficeint toilets.
  3.majengo ya wakuu wa miko na wilaya,hospitali kuu za wilaya na mikoa..,zote zimejengwa na wakoloni whose only reason to build them was for their benefits

  i could go on listing so many things done during ukoloni.that remains today.

  i have always wished our leaders would better that,never!all they do is shameless scandals.

  siwapendi wakoloni ,siwataki,ila ukweli ni kuwa waliifanyia tanzania mengi ambayo viongozi wetu wameshindwa for 50 gadamn years.

  unless these so called viongozi step up their game,there is no reason to hate colonialism as we still have the smae exploitation now,only that who does it is a fellow countryman.be it a politician or a corrupt businessman.
   
 14. S

  Sahiba JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lole we ukisikia kambini unawaza vita nop that is not a solution na kwenda kutumika kwao is not either rather than kuzidi kuwatajirisha.The good thing is wanapokutuma wankulipa pesa za kutosha kumaliza mwezi rather than kwetu lazima uongeze na mission town/uibe ili ujikimu mahitaji ya mwezi.Next time muheshimiwa Lola usiitetee tu CCM isome message uielewe usiruke tu na kujibu kwa jazba,je uko tayari we need new idea is about change but not just change.CHANGE WE CAN BELIEVE not nguvu mpya kasi mpya guys tell us where is our destination and if we believe you then show us something we need to see this crooks goes down including their father is not about party is about people who vote for you.. THAT'S RIGHT.
   
 15. S

  Sahiba JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pangu Pakavu,
  I like your analysis ZILIZOPATA BAHATI.YES YOU ARE DAMN RIGHT They did alot of good things for us compare to wazalendo wetu in all these years.Honestly speaking you have to be out of your mind to believe Mugabe is taking them somewhere may be to the grave G_D knows.The truth is many African leaders are so selfish they think about themseves not the country WE NEED CHANGE MAY BE WE NEED PEOPLE LIKE IDD AMIN GUYS IS NOT WORKING LET'S MAKE IT WORK FIND THE REAL SOLUTION LET'S PULL UP OUR PANTS AND GO TO WORK......YES.
   
 16. mwakatojofu

  mwakatojofu JF-Expert Member

  #16
  Jan 15, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuukubali ukweli mwingine ni vigumu sana. unauma. lakini je, ni kweli kipindi cha ukoloni africa palikuwa pazuri kuliko leo (hasahasa kiuchumi, kiusalama, kijamii)? tuangalie ujumla wake. tusiangalie baadhi ya vitu.

  kama leo tunazidi kuwa katika hali mbaya kuliko ilivyokuwa zaman za mkoloni ni jambo ambalo si zuri.
  kuwatoa wakoloni haikuwa lelemama. mababu zetu walipoteza vingi kuupata uhuru - ikiwemo kumwaga damu zao. lengo lao ilikuwa si tu kumtoa mweupe madarakani bali pia kupata hali bora zaidi maishani. wao na vizaz vijavyo

  na kama mweupe ametoka lakin hali zetu zi bado mbaya au zinazid kuwa mbaya, malengo hayajatimia.
   
 17. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #17
  Jan 15, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Waafrika bado tuna kutu vichwani mwetu ya kutopenda vya kwetu. Ndio maana nchi zilizotawaliwa na Wafaransa wao macho yao yote yapo Ufaranza na sisi tuliotawaliwa na Waingereza pia tunatazama huko vivyo hivyo kwa waliotawaliwa na Wabelgiji na Wareno. Huu ukoloni mambo leo umetuingia sana na kuuondoa imekuwa shida sana. Ndio kwa maana tunajali sana mwekezaji wa nje tukitumainia atatuokoa kuliko wa ndani japo huko kwao pesa amezipata kwa njia ya udanganyifu au utapeli sisi tunamkumbatia na kumpa misamaha ya kodi kuliko mzalendo. Wanapewa utajiri kwa muda mfupi lakini nchi haifaidiki. Kama ingekuwa mabenki ya kizalendo yanawapa nguvu wazalendo kuanzisha miradi mikubwa kama hao wanaoitwa wawekezaji wa nje wanavyosaidiwa na mabenki yao basi tungekuwa mbali. Tazama Zimbabwe wakati wazungu walipokuwa wakilima tumbaku na mazao mengine walikuwa wanasaidiwa sana na yale mabenki yao naya nje. Lakini Ardhi iliporudishwa kwa wazawa mabenki yamemuacha huyo mzawa na hiyo ardhi na kushindwa kuitumia kibiashara na matatizo kibao yamezuka katika nchi ile. Kwa kumalizia ni kwamba si lazima uwekezaji kutoka nje ndio utakaotukomboa hata wazawa wakiwezeshwa wanaweza na tutapiga hatua kubwa kama na wananchi watapenda bidhaa ambazo zitazalishwa nchini.
   
 18. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #18
  Jan 15, 2009
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwasababu waswahili hawaaminiani na kazi inawashinda...(ATC, TANESCO,PResidency, BOT, Mali asili, Mugabe etc etc) wezi wezi tu...serikalini wachache tu wanajali maslahi ya nchi, mambo mengi waswahili tunaweza uyatatua wenyewe (nimetaja serikali kwasababu hiki ndio kikwazo kikubwa cha maendeleo yetu due to poor performance, na this is where things rare regulated, such as investments etc etc)...sema miafrika inakuwa very easily manipulated...no matter how much we try, litakuja jitu ambalo sole purpose ni kuhakikisha hufanikiwi kibiashara, na siyo kwamba ni kwasababu ana ushindani na wewe..ni kwasababu hapendi kuona mtu ana-succeed, sorry but true...
   
Loading...