Kwanini tunatimkia Loliondo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini tunatimkia Loliondo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Apr 7, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Picha hii inaelezea mojawapo tu ya sababu lukuki za kwa nini watu wanaamua kuacha matibabu na kuamua kukimbilia Loliondo kwa matumaini ya kuwa watapona na kuondokana na adha za magonjwa waliyonayo.

  Nyinginezo ya sababu, wachilia hii ya dawa feki ambazo zimekuwa zikipigwa vita, ni pamoja na:-
  "kadhia" na "usumbufu" wa mazingira ya hospitalini
  Huduma zisizoridhisha mahospitalini
  Huduma hafifu, duni au zilizokosekana kabisa mahospitalini
  Kukata tamaa baada ya matibabu ya muda mrefu
  Kutaka tiba ya haraka bila gharama kubwa (matibabu mkato)
  Kutokuwa na elimu wala ufahamu wa tiba za mahospitalini
  Jamii kukua katika mazingira ya kuamini 'uganga' zaidi
  Kutaka kupata ahueni kwa gharama yoyote ile
  na sababu kadha wa kadha unazoweza pia ukawa unazifahamu au umezisikia. Si vibaya ukiziorodhesha hapa pia, pengine wako wanaochukua 'notes' watasoma na kujua namna ya kurekebisha mfumo wa afya nchini na hivyo kurudisha imani ya Watanzania katika huduma wanazopewa na Wasomi/Wataalamu wetu.

  1099576.jpg
   
Loading...