Kwanini tunateseka kwa kuendelea kutumia Kiingereza kama lugha ya kujifunzia?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Nimerudi tena na hii hoja dhidi ya matumizi ya kiingereza kama Lugha ya kujifunzia.

Umewahi soma riwaya za kiingereza na kiswahili? Kama umewahi, utagundua kuwa utatumia muda mrefu sana kusoma riwaya ya kiingereza kuliko ya kiswahili. Riwaya ya kiswahili unayoweza kusoma kwa siku mbili, ikiwa kwa kiingereza unaweza tumia siku kumi na zaidi. Kusoma machapisho ya kiingereza kunaumiza sana akili kuliko kusoma ya Kiswahili.

Na kujiumiza huku hakuna manufaa yoyote, mfano kama ni maarifa ya shule unaweza yapata yaleyale kwa kiingereza na kwa kiswahili. Mateso haya yanafanya watoto wengi wakate tamaa ya kuendelea na sekondari, wafeli, wasijisomee textbooks, na waishie kukariri. Inasemwa kuwa ni 15% ya wanafunzi wa sekondari ndiyo wanaelewa kiingereza kiasi cha kuweza kuitumia kama lugha ya kujifunzia.

Kosa kubwa kwenye elimu yetu ni kutumia kiingereza kama lugha ya kujifunzia. Na ndilo tatizo namba moja la elimu yetu. Tukirekebisha mambo yote, lakini bado tukiendelea kujifunza kwa kutumia lugha tusiyoielewa, hatutaelimika.

Nimewahi sema kuwa, kwa kuendelea kutumia kiingereza kama lugha ya kujifunzia, tunakuwa kama mtu aliyepotea njia lakini anaona uvivu kurudi nyuma.

Kwanini hatutumii kiswahili kama lugha ya kujifunzia katika ngazi zote za elimu?
 
Hoja unayotoa ni ya msingi sana. Sasa tukirudi kwenye lugha ya kufundishia. Nadhani hili mtu aweze kuelewa vizuri mafundisho darasani ni lazima kuwepo na kiwango fulani cha lugha alichofikia. Sisi tuliowahi kutoka nje ya Tanzania na kusoma katika lugha za kigeni. Tulitumia mwaka au zaidi kujifunza lugha mpya. Na tulifundisha na waalimu waliokuwa utaalamu wa kufundisha lugha. Na baadaye tulifanya mitihani ya lugha iliyotathmini uwezo wetu wa kusoma taaluma kwa kutumia lugha za kigeni.

Kwa Tanzania, tatizo kubwa ni kuwa wanafunzi sio proficient katika lugha. Miaka mitano ya kujifunza kiingereza katika shule za msingi inatosha kumpa mwanafunzi uwezo wa kusikiliza na hata kuongea kwa kubabaisha. Tatizo ni kuwa wanaofundisha lugha yenyewe hawajui kufundisha kiingereza kwa watu wanaozungumza kiswahili.

Tukirudi kwenye matumizi ya kiswahili, inawezekana kabisa kutumia hiyo lugha. Kuna masomo mtu angeweza kuyasoma mpaka level ya PhD, kwa kiswahili. Tungeanzia huko kwanza. Masomo mengine yangejileta polepole. Kama unaweza kufundisha hisabati kwa kiswahili mpaka darasa la saba, utakuwa umebakiza misamiati michache sana ya kuweza kufundisha mpaka O level.
 
Na bahati nzuri kwenu mliokuwa nje, mliitumia hiyo lugha kila mahali mlikokwenda, hilo linarahisisha sana kujifunza lugha. pamoja na sababu ulizotoa, mwanafunzi huku anadisadvantage nyingine. katika hiyo miaka mitano, lugha ya kiingereza haitumii popote zaidi ya katika kipindi cha kiingereza.

Hii ya kusoma baadhi ya masomo kwa kiswahili mpaka elimu ya juu inaweza saidia sana na ukawa mwanzo mzuri. Nilisoma mahali kuwa Morocco ni masomo ya sayansi ndiyo yanafundishwa kwa kifaransa, mengine ni kwa kiarabu. Japo kwa maoni yangu naona kila somo linaweza fundishwa kwa kiswahili.
 
Siri kubwa ya kuelewa lugha ni mazoezi ya lugha na mapenzi ya lugha hiyo. Shule niliyosoma pamoja na kutumia lugha ya nchi yao kwenye kila kitu ilihimiza wanafunzi kuchukua lugha za kigeni. Na wanafunzi wengi walichukua kiingereza, kijerumani, kifaransa na kufanya vizuri tu.

Kwa maoni yangu binafsi suala kubwa kwa Tanzania ni ufundishaji wa masomo ya lugha zenyewe. Kiingereza ni lugha ya pili kwa Tanzania wengi na ifundishwe kama lugha ya pili na waalimu wenye uwezo wa kufundisha lugha ya pili. Nakumbuka nikiwa Tanzania, mwalimu wa kiingereza alikuwa hatumii kiswahili. Lakini wakati najifunza lugha zingine nje ya Tanzania, walimu walikuwa wanatumia lugha yoyote hile kufanya wanafunzi waelewe.

Kwa Tanzania tunaweza kutumia kiswahili kwa shughuli zote za darasani. Lakini ni lazima tujifunze lugha zingine kwa weledi wa hari ya juu.
 
Ngoja nami nitie mkono kwenye mada hii isiyokwisha miaka kwa miaka

Wakati hoja kuwa lugha unayoilewa ndiyo bora kujifunzia kama inavyodaiwa na watafiti, tusijisahau hapo pekeee. Tatizo la elimu ya bongo ni zaidi ya lugha ndugu yangu. Tazama hili. Tangu tunapata uhuru, matumizi ya lugha za kufundishia yapo vilevile. Kiingereza na Kiswahili zimebaki katika namna ileile. Kama kuna mabadiliko kimfumo wa madarasa ni kidogo sana. Lakini unaweza jiuliza, huu ukilaza tunaouona siku hizi unatoka wapi? Kwanini ukimchukua mhitimu wa leo (iwe la saba, kidato cha nne au sita, cheti, stashahada ama chuo kikuu) hafanani na wa mwaka jana, wa mwaka jana hafanani na mwaka juzi. Endelea kurudi kinyumenyume mpaka ufike kwa mkoloni kisha utagundua kadiri tunavyosonga mbele ndivyo ubora wa elimu unashuka.

Hoja yangu ni, kwanza, ninakiri mchango wa lugha ya kufundishia, kwamba ukifundishwa kwa lugha unayoimudu, unaelewa dhana zilizokusudiwa kirahisi. Lakini, kwa kesi ya Tz , ni tofauti kidogo. Tuna shida katika mfumo/mtaala na zoezi zima la ufundishaji linavyofanyika. Shule za msingi za uma wanatumia Kiswahili, tuwatoe watoto wa vijijini, maana unaweza sema wao hawana uwezo wa Kiswahili kihivyo (wengi Kiswahili ni lugha ya pili), tubaki na hawa wa mijini. Je, unaridhika na watoto wa mijini katika uelewa wao? Si wanatumia Kiswahili?

Haya, kuna hili kundi la shule za binafsi, nyingi zinaitwa English medium. Haya, kila kukicha tunasikia sifa za ufaulu wa watoto wa shule hizi, kwa miaka kadhaa walipindua meza. Sawa, watoto hawakosi Kiingereza cha kuombea maji. Lakini umewahi kujiuliza hawa watoto mwisho wao ni wapi? Umewahi kuona miujiza yoyote kwa zile A zinazotolewa na mashule ya private? Umewahi kukutana na watoto waliotoka English medium vyuoni?

Kama umekutana nao, umeona wana miujiza yoyote? Hawa ndiyo tulitegemea wafikapo vyuoni, wawe na uwezo mkubwa sana wa kubukua nondo zilichapwa Kiingereza na kufanya miujiza ndani na nje ya darasa,lakini, hali haipo hivyo hata kidogo. Tumesoma nao, tunawaona uwezo wao. Baadhi tumewakimbiza sana tu huko vyuoni. Sasa kule shule ya msingi za uma Kiswahili, wamechoka, zile za binafsi Kiingereza, bado hawaoneshi uwezo kihivyo wafikapo ngazi za vyuo. Tumelogwa?

Mimi ninaamini hata tungebaki na lugha hizihizi, kwa mtindo huuhuu uliopo sasa , tukawaivisha watoto pande zote, kwenye lugha zinazotumika kufundishia na kule kwenye masomo ya maudhui (sayansi, hesabu, historia nk.) bado tungeweza kuwa na vijana wazuri tu kama ilivyokuwa zamani. Kuna mahali tumeyumba kama taifa.

Waasalam
 
Back
Top Bottom