Kwanini tunateseka kwa kuendelea kutumia kiingereza kama lugha ya kujifunzia?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,118
2,000
Nimerudi tena na hii hoja dhidi ya matumizi ya kiingereza kama Lugha ya kujifunzia.

Umewahi soma riwaya za kiingereza na kiswahili? Kama umewahi, utagundua kuwa utatumia muda mrefu sana kusoma riwaya ya kiingereza kuliko ya kiswahili. Riwaya ya kiswahili unayoweza kusoma kwa siku mbili, ikiwa kwa kiingereza unaweza tumia siku kumi na zaidi. Kusoma machapisho ya kiingereza kunaumiza sana akili kuliko kusoma ya kiswahili.

Na kujiumiza huku hakuna manufaa yoyote, mfano kama ni maarifa ya shule unaweza yapata yaleyale kwa kiingereza na kwa kiswahili. Mateso haya yanafanya watoto wengi wakate tamaa ya kuendelea na sekondari, wafeli, wasijisomee textbooks, na waishie kukariri. Inasemwa kuwa ni 15% ya wanafunzi wa sekondari ndiyo wanaelewa kiingereza kiasi cha kuweza kuitumia kama lugha ya kujifunzia.

Kosa kubwa kwenye elimu yetu ni kutumia kiingereza kama lugha ya kujifunzia. Na ndilo tatizo namba moja la elimu yetu. Tukirekebisha mambo yote, lakini bado tukiendelea kujifunza kwa kutumia lugha tusiyoielewa, hatutaelimika.

Nimewahi sema kuwa, kwa kuendelea kutumia kiingereza kama lugha ya kujifunzia, tunakuwa kama mtu aliyepotea njia lakini anaona uvivu kurudi nyuma.

Kwanini hatutumii kiswahili kama lugha ya kujifunzia katika ngazi zote za elimu?
 
Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,067

Hoja unayotoa ni ya msingi sana. Sasa tukirudi kwenye lugha ya kufundishia. Nadhani hili mtu aweze kuelewa vizuri mafundisho darasani ni lazima kuwepo na kiwango fulani cha lugha alichofikia. Sisi tuliowahi kutoka nje ya Tanzania na kusoma katika lugha za kigeni. Tulitumia mwaka au zaidi kujifunza lugha mpya. Na tulifundisha na waalimu waliokuwa utaalamu wa kufundisha lugha. Na baadaye tulifanya mitihani ya lugha iliyotathmini uwezo wetu wa kusoma taaluma kwa kutumia lugha za kigeni.

Kwa Tanzania, tatizo kubwa ni kuwa wanafunzi sio proficient katika lugha. Miaka mitano ya kujifunza kiingereza katika shule za msingi inatosha kumpa mwanafunzi uwezo wa kusikiliza na hata kuongea kwa kubabaisha. Tatizo ni kuwa wanaofundisha lugha yenyewe hawajui kufundisha kiingereza kwa watu wanaozungumza kiswahili.

Tukirudi kwenye matumizi ya kiswahili, inawezekana kabisa kutumia hiyo lugha. Kuna masomo mtu angeweza kuyasoma mpaka level ya PhD, kwa kiswahili. Tungeanzia huko kwanza. Masomo mengine yangejileta polepole. Kama unaweza kufundisha hisabati kwa kiswahili mpaka darasa la saba, utakuwa umebakiza misamiati michache sana ya kuweza kufundisha mpaka O level.
 
Na bahati nzuri kwenu mliokuwa nje, mliitumia hiyo lugha kila mahali mlikokwenda, hilo linarahisisha sana kujifunza lugha. pamoja na sababu ulizotoa, mwanafunzi huku anadisadvantage nyingine. katika hiyo miaka mitano, lugha ya kiingereza haitumii popote zaidi ya katika kipindi cha kiingereza.

Hii ya kusoma baadhi ya masomo kwa kiswahili mpaka elimu ya juu inaweza saidia sana na ukawa mwanzo mzuri. Nilisoma mahali kuwa Morocco ni masomo ya sayansi ndiyo yanafundishwa kwa kifaransa, mengine ni kwa kiarabu. Japo kwa maoni yangu naona kila somo linaweza fundishwa kwa kiswahili.
 
Siri kubwa ya kuelewa lugha ni mazoezi ya lugha na mapenzi ya lugha hiyo. Shule niliyosoma pamoja na kutumia lugha ya nchi yao kwenye kila kitu ilihimiza wanafunzi kuchukua lugha za kigeni. Na wanafunzi wengi walichukua kiingereza, kijerumani, kifaransa na kufanya vizuri tu.

Kwa maoni yangu binafsi suala kubwa kwa Tanzania ni ufundishaji wa masomo ya lugha zenyewe. Kiingereza ni lugha ya pili kwa Tanzania wengi na ifundishwe kama lugha ya pili na waalimu wenye uwezo wa kufundisha lugha ya pili. Nakumbuka nikiwa Tanzania, mwalimu wa kiingereza alikuwa hatumii kiswahili. Lakini wakati najifunza lugha zingine nje ya Tanzania, walimu walikuwa wanatumia lugha yoyote hile kufanya wanafunzi waelewe.

Kwa Tanzania tunaweza kutumia kiswahili kwa shughuli zote za darasani. Lakini ni lazima tujifunze lugha zingine kwa weledi wa hari ya juu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom