Kwanini tunataka mtu mwenye maono mazuri kwa Mustakabali wa taifa letu?

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
7,664
2,000
Amani iwe nanyi wakuu,

Nikiwa natafakari kuhusu mustakabali wa Nchi yetu huko mbeleni kuna kitu nimekuwa nikikiwaza sana na leo nimeona nishirikiane na wenzangu juu ya hili suala kupitia hili jukwaa linalosifika kuwa jukwaa la Great Thinkers.

Tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu huku macho ya watanzania wote yakiwa yanatazama ni nani anatufaa kwa ajili ya mustakabali mzuri wa taifa letu huko mbeleni hasa kwenye suala la maisha ya watanzania na ustawi safi na mzuri wan chi yao unaowanufaisha wao na vizazi vyao, napenda nitoe mchango wangu kwa watanzania wenzangu wote watakaoisoma hii thread na naomba watumie muda wao wanaopewa na Mungu kusambaza hii elimu.

Kuna kitu kikubwa sana ambacho nchi nyingi duniani wamekuwa wakikikosa na hapo ndo mataifa makubwa yamekuwa yakikitumia kama fimbo na silaha yao kuu katika kuendelea kuitawala dunia na hicho kitu ni UCHUMI IMARA.

UCHUMI IMARA unaweza kuonekana kama ni msamiati kwa baadhi ya watu lakini ndugu zanguni hapa ndo ilipo siri ya ubabe wa hawa tunaowaita wababe wa dunia hii ya leo. Hapa duniani kuna pande mbili zinazokinzana nazo ni MAGHARIBI kwa kifupi wakiongozwa na Marekani na washirika wake wengi wakiwa Ulaya na MASHARIKI wakiongozwa na Urusi, China na washirika wao.

Hawa ndo wamekuwa wakiiendesha dunia kwa maslahi yao. Mfano mkubwa wa hawa watu kuiendesha dunia ni kwa kifupi ili wenzangu mnielewe haraka ni kushuka kwa bei ya mafuta na gesi kulikotokea hivi karibuni.

Kuna watu watajiuliza kwa nini hii bei ilishuka lakini kwa kifupi huku kulitokana na Marekani kutaka kumkomoa urusi ambaye ndo mzalishaji mkuu wa gesi ulaya kutokana na kiburi chake kwenye mgogoro wa Ukraine.

Hii inaonesha kuwa njia na sera za Uchumi wa dunia zinashikwa na hawa watu na hawa watu ndo wanaocontrol uchumi wa dunia sasa swali kubwa hapa kwetu mwaka huu wa uchaguzi ni kuwa tunaitaji kiongozi wa namna gani ili tuweze kusurvive na kuwa salama kwenye dunia hii ya ushindani iliyoshikwa na hawa mabwana wawili?

Kabla ya kwenda huko napenda kuwatolea mfano viongozi wawili wan chi za Afrika ambao mmoja ni marehemu na mwingine bado yu hai ili tuweze kujifunza kitu watanzania wenzangu hasa kipindi hiki tunapoenda kuamua nani wa kumpa hii nchi kwqa miaka mitano ijayo.

Wa kwanza ni Coloner Muahamad Ghadafi, huyu ndo alikuwa mfano mzuri kwa viongozi wa kiafrika hasa kwenye kujenga nchi imara kiuchumi kwa mustakabali wa taifa lake na wananchi wake. Ghadafi alijua silaha kubwa ya West ni UCHUMI IMARA na akaijenga Libya yenye Uchumi Imara kiasi kwamba kwa ustawi na hali ya Libya ilivokuwa ikienda West walianza kuhisi ipo siku Libya itakuja kuwa Nchi yenye nguvu sana kiuchumi na hata kiteknolojia(silaha) kiasi kwamba itakuwa threat kubwa kwa Ulaya(kwa sababu kutoka Libya hadi ulaya sio mbali sana).

West walimuona Ghadafi ni threat kwao na walishindwa kabisa kupigana nae kiuchumi kwa sbabu alivokuwa kiongozi imara kimaono hasa katika kuijenga nchi yake kiuchumi, ikabidi wamtoe kupitia mtutu au mass riot ambayo wachambuzi wengi duniani wameshaanza kuisi kuwa Arab spring ilikuwa idea ya maanalyist wa intellegensia zenye akili za West ili kuondoa viburi wote katika Arab world.(Nitalielezea hili wakati muafaka ukifika).

Wa pili ni Comredi Robert Mugabe, huyu ni mfano mwingine wa viongozi wa Afrika aliyejua janja ya nchi kubwa duniani ila huyu tatizo lake ni kuwa hana maono mazuri katika kuijenga nchi yake kuwa imara kiuchumi ili aweze kupambana na wale jamaa wakubwa. Mugabe ni kiongozi mwenye msimamo, anayejiamini na asiyejua kumficha mtu kwa sababu kwake nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi. Ila tatizo lake kubwa ni kuwa West wamemuweza kwenye kitu kidogo tu nacho ni Uchumi na ndo mana leo hii Zimbambwe aisogei wala haiendi.

Kwa nini nimetolea mfano viongozi hawa wakati huu Tanzania tukiwa tunafikiri nani anayetufaa kwa mustakabali wan chi yetu na vizazi vyetu huko mbeleni? Ni kwa sababu kwenye uchaguzi huu wanaojitokeza kujipambanua kutaka nafasi ya uraisi wengi wapo kwenye kundi la Mugabe yani wale waliojionesha kuwa wako imara,wana misimamo, wanawasema vibaya wala rushwa na kusema hata watawafunga jela na kuwafukuza na kutumia nguvu nyingi kujionesha ni kwa jinsi gani wanachukia rushwa,ufisadi (ila wanashindwa kujipambambanua kwa namna gani kuijenga Tanzania imara kiuchumi ili kesho tuweze kuwa huru kweli na wananchi wetu wafaidike kweli) ili tu wapendwe na waungwe mkono na watanzania wengi ambao wengi wao hawana uelewa mpana na mambo ya dunia hii.

Lakini ni wachache sana walio kwenye kundi la Ghadafi wenye maono mazuri juu ya Tanzania na mikakati mizuri ya kufikia hayo maono, kwenye kuijenga Tanzania nzuri,yenye kutumia rasilimali lake vizuri kujenga uchumi imara unaolinufaisha taifa na wananchi wake kwa ujumla.

Napenda kumalizia mada hii kwa kusema, Tanzania tatizo letu sio tu Rushwa na hata tukifanikiwa kuiondoa Rushwa bado tutazidi kuwa ombaomba na maskini kwa sababu tu bila UCHUMI IMARA nchi itaendelea kuwa tegemezi na kuendeshwa na jamaa wawili ambao ni MAGHARIBI NA MASHARIKI, au kuwa nchi maskini ambayo raia wake bado wapo kwenye umaskini wa kutupwa pamoja na kuwa hakuna kiwango kikubwa cha Rushwa kama ilivo Bolivia na hata Cuba.

Tanzania tunaitaji kiongozi mwenye maono anayeweza kujua jinsi ya kucheza na hawa wakubwa wote wanaoiendesha dunia na siku ya mwisho akajenga Uchumi imara utakaolinyanyua taifa na kuliweka juu taifa letu na wananchi wa taifa letu kwa pamoja wakashukuru kwa Mungu kwa kuwaweka duniani.

Ni wakati muafaka huu wa kuwapima wagombea wote kuona wana mikakati gani na maono gani juu ya Tanzania tuitakayo na inayotakiwa kuwepo huko mbeleni na kusema tumchague huyu ili atufikishe huko.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom