Kwanini tunapenda sana njia za mkato? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini tunapenda sana njia za mkato?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Invarbrass, Mar 23, 2011.

 1. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimejaribu kufuatilia utaratibu wetu wa maisha sisi watanzania nakubaini kuwa njia za mkato zinapendwa sana katika kutafuta majibu. Kwa harakaharaka inaweza kuonekana sio tatizo maana kama majibu hayachelewi kutoka yanini kujisumbua na njia ndefu. Ila katika uhalisia (kwa mujibu wa kanuni za sili) majibu ya njia za mkato huwa ni ya muda tu na si ya kudumu. Hebu tujaribu kuona hali ilivyo katika nyanja mbalimbali;
  1. mpira wa miguu timu zetu hufanya maandalizi ya zima moto kabla ya kushiriki michuano ya kimataifa then kamati za maandalizi huwa haidi wachezaji pesa endapo watashinda. kichekesho nim kwamba wakati wa maandalizi wachezaji wanakuwa hawana huduma nzuri lakini watu wanahasika wanasubiri ushindi bila was was.
  2. mashuleni, baadhi ya wazazi hawanunui vitabu kwa watoto wao ila wako tayali kununua mitihani ya mwisho ili mtoto ashinde, serikali nayo hailipi walimu, hainunui vitabu wala madarasa lakini inataka watoto wote wafaulu kwa kushauri mitihani itungwe myepes(uhauri wa president), wakati mwingine makanisa mbalimbali huendesha maombi maalumu kwa watahiniwa wakati wa mitihani na kuwaamisha wanafunzi kuwa watafaulu mitihani yao, kwanini wanafunzi wasiimizwe kusoma kwa bidii wakati ili hata mwaisho wakiombewa kuwe na mantiki maaana ukishamwambia mwanafunzi hakuna kisichowezekana anaweza hata kudharau kujisomea si ataombewa.
  3. mipango ya maendeleo, mara nyingi mipango mingi inakuwa ile ya kuleta majibu ya haraka (impression) hata kama majibu ni ya muda tu. Mfano, kupeleka wtoto wote/wengi sekondari hata kama hawakufaulu inavotakiwa, kujenga shule nyingi kila kata hata kama hazina walimu, kupandisha watumishi mishahara wakati hera hakuna hivo kupelekea mishara mipya kulipwa baada ya miezi sita,
  4. kijamii, kuamini uzushi kuliko ukweli, kupenda kusikia tu habari zinazopendeza na kutokuwa wavumilivu wa kusikia hata tusichokipenda li tuweze kukikataa kwa kanuni ya mantiki, kukubali mawazo ya watu kwa mkumbo bila kutafakari ilimradi tu aloyatoa ahaheshimika, au wengi wanayakubali.
  5.Dini, kupendelea madhehebu yanayo hubiri neema, yaani kupata mafaniko kwa maombi tu kama vile kupata magari, kupanda vyeo, kwenda uraya, kupata mchumba, kuondokana na tatizo la madeni, kuboresha ndoa, kupendwa na watu nk.
  Nadhani wanao tumia njia hizi wanashuhudia umuhimu wake, wasiwasi wangu nim kuwa tukitoa kipaumbele kwa njia hizi tu kuna hatari ya mambo yafuatayo 1. kuharibu ubunifu, kujituma na bidii ya kufanya kazi ambayo ndo msingi wa maendeleo kokote kule,2. tunatengeneza uwezekano wa kutapeliwa kama atatokea msanii akatusoma vizuri (mifano ni mingi duniani hata hapa mfano DECI ambapo mtu alitakiwa KUPANDA HELA NA KUVUNA MARA DUFU tukiaminishwa kuwa difference anajazia Yesu), 3. watu hawatafanya kazi.4. maendeleo yetu hayatakuwa endelevu tutabaki kudili na dharura 5. hatutakuwa na rasilimali ya kuwaachia vizazi vyetu maana si tuliishi kwa ujanja ujanja. sayansi itakufa maaana tunajenga utaratibu wa kuikataa na kuibeza (nilimsikia kiongozi wa Simba akijigamba kuwa walicheza mpira mpaka TP mazembe wakawaogopa , yaani mazembe iifunge simba tatu moja afu iiogope na watu kwa kauri ya kiongozi huyo wajenge matumaini ya kuitoa timu hiyo lakini hiyo ndo bongo.

  Ndugu zangu kanuni za asili ziko wazi ili kufanikiwa inatakiwa kujitoa, kpigana kujituma, kujinyima na kufanya kazi kwa maarifa na juhududi tukitumia ujuzi tunao pata kwa mfano ukisoma na kufanya kazi kwa bidii utapandishwa cheo. ukisoma na kuwekeza katika elimu watoto watafaulu, madege, viwanda, barabara , mabenki, maarifa na vyote tuvionavo kwa wenzetu nimatokeo ya kazi za wanadamu kanuni zao ziko wazi tuzifuate vinginevyo elimu tuipatayo haina maaana na ndio maana haishangazi kuona mtu anaamini kuwa ukiwa na kiungo cha arubino unatajika na ndio maana huwezi shangaa ukikuta watu wamefunga mizigo wako airport wanaenda uraya kuhubiri tena kwa swahili na wana kwambia hawana nauli, wala viza lakini Mungu amewahakikishia wanaenda. Wote hawa tusiwacheka nimatokeo ya mfumo. NI MTIZAMO TU
   
 2. k

  kimini Member

  #2
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nimeipenda sana makala yako ndugu,ila me naona kwa maneno ya haraka haraka ni uvivu wa kufikiri na kutenda ndio chanzo cha sisi kufanya mambo haya......
   
Loading...