Kwanini tunapenda kutuma pesa (kwa njia ya simu) kuliko benki ambazo huwa na gharama nafuu?

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
669
Hii sio hypothesis, imeshakuwa proven kwa tafiti zilizofanywa na wengine wanaotafiti kuhusu poor economics.

Iko hivi ni rahisi kujua kuwa gharama za kutuma na kutoa fedha kwa kutumia simu, iwe M-pesa, Tigo pesa nk ni gharama zaidi kuliko kutumia benki i.e ATM ambazo zimetapakaa nchini.

Kwa maeneo kama Dar, ATM zimetapakaa maeneo mbalimbali na zaidi benki nyingi zinatumia mitandao mikubwa kama VISA, MASTARCARD, MAESTRO nk ambayo haikupi ulazima wa wewe kutafuta benki yako ili kutoa fehda.

Mbali na hayo bado watu wamekuwa wakitumia zaidi mitandao ya simu ambayo ina gharama kubwa za huduma zao kuliko benki, Je shida iko wapi.

Wewe kama mdau unayetumia simu kufanya miamala, Je unadhani ni kipi kinakufanya ukae humo ukizingatia gharama ni kubwa?

Nadhani watu wa benki wanaotengeneza mifumo ya masoko wanaweza kuwa na njia nzuri ya kuweza kujua namna gani ya kuwanasa watu ambao wanatumia simu badala ya benki ambazo zina gharama nafuu.

Hypothesis: Watu hawatumii benki kwa kuwa benki zinaonekana kama ni za watu fulani wenye hadhi na fedha nyingi (It can be tested)

Au ni kuwa watu huwa hawana muda wa kujua kuhusu gharama za masuala ya kifedha.

Signed

Oedipus
 
Mkuu,

Tatizo wewe unaangalia gharama za miamala tu!

"Time" na "uconviniency" wa mobile services ndio kila kitu.

Yaani kama kutuma kutumia benk nakatwa 2000 na kutuma kupitia simu nakatwa 3500 consider sasa time ya kwenda benk, usumbufu, pia ile availability ya service ni changamoto
 
Umetumwa kuja kupeleka taarifa ili watuongezee makato na kodi...
Au ikoje hii?? Samahani mkuu!

Maana tukijilipua humu kukujibu kesho, inakuja sera wenye account benki marufuku kutumia mobile banking.

Hii nchi inatutia hasira na machungu kila uchwao.

Everyday is Saturday............................. 😎
 
Ki kweli mitandao ya simu inanufaika sana na pesa zetu ni kama kwamba lile wazo waliokuja nalo la kutoa huduma ya mawasiliano halilipi tena wamekuja kufumania sehemu yenye kulipa zaidi kamari na huduma za kifedha kuna siku nilivuta pesa kutoka benk kuja halopesa walikata mpaka nikaogopa sijarudia tena
 
Cost ipo katika sehemu tatu..
1. Money
2. Time
3. Convenience.
Wewe umefucos katika pesa tu.

NB: Mitandao inapiga hela kwenye hizi transactions
Kiongozi, weka Time, kwa ulimwengu wa sasa kuna ATMs ambazo unaweza kutoa fedha, pia hata kwenye simu kuna wakati unaweza kusimama tu kusubria muamala urudishe meseji ya kuthibitisha

Convinience ni ipi ambayo haipo kwenye huduma za kibenk
 
We una hela nyingi Sisi miamala yeti mingi iko chininya laki 2 nyie wenye mamilioni muendage huko tusibanane
Benk nyingi unafungua account kwa Tsh 20,000 kwa hiyo kama uko chini ya laki mbili pia unaweza kufuwa na account na ukatoa muda unataka

Je na hili nalo ni shida au ni some complexities tu?
 
Cost ipo katika sehemu tatu..
1. Money
2. Time
3. Convenience.
Wewe umefucos katika pesa tu.

Kiongozi, weka Time, kwa ulimwengu wa sasa kuna ATMs ambazo unaweza kutoa fedha, pia hata kwenye simu kuna wakati unaweza kusimama tu kusubria muamala urudishe meseji ya kuthibitisha

Convinience ni ipi ambayo haipo kwenye huduma za kibenk
Sio wote tunaishi Dar es Salaam
 
Hii sio hypothesis, imeshakuwa proven kwa tafiti zilizofanywa na wengine wanaotafiti kuhusu poor economics.

Iko hivi ni rahisi kujua kuwa gharama za kutuma na kutoa fedha kwa kutumia simu, iwe mpesa, tigo pesa nk ni gharama zaidi kuliko kutumia benki i.e ATM ambazo zimetapakaa nchini.

Kwa maeneo kama Dar, ATM zimetapakaa maeneo mbalimbali na zaidi benki nyingi zinatumia mitandao mikubwa kama VISA, MASTARCARD, MAESTRO nk ambayo haikupi ulazima wa wewe kutafuta benki yako ili kutoa fehda.

Mbali na hayo bado watu wamekuwa wakitumia zaidi mitandao ya simu ambayo ina gharama kubwa za huduma zao kuliko benki, Je shida iko wapi.

Wewe kama mdau unayetumia simu kufanya miamala, Je unadhani ni kipi kinakufanya ukae humo ukizingatia gharama ni kubwa?

Nadhani watu wa benki wanaotengeneza mifumo ya masoko wanaweza kuwa na njia nzuri ya kuweza kujua namna gani ya kuwanasa watu ambao wanatumia simu badala ya benki ambazo zina gharama nafuu

Hypothesis: Watu hawatumii benki kwa kuwa benki zinaonekana kama ni za watu fulani wenye hadhi na fedha nyingi (It can be tested)

Au ni kuwa watu huwa hawana muda wa kujua kuhusu gharama za masuala ya kifedha.

Signed

Oedipus
Nikuulize kwa nn utoe kwa ATM?

Wakati ndani bank teller anakusubiri?
 
Hili la kusema watu wengi hudhani kuwa benki ni kwa ajili ya watu fulani ni sahihi kabisa. Ndio maana watu wengi hawana account za bank. Lakini watu hao wengi wasio na bank accounts wana miliki simu na wanapokea na kutuma fedha kupitia accounts za simu.

Iko hivi, watu wengi hawana taarifa sahihi juu ya matumizi ya accounts za bank. Kuna rafiki zangu siku moja walikua wanang'ang'ania kuwa wataendelea kutumia CRDB kwa sababu ipo kila mahali...mimi nikawaambia sitaitumia sababu muda mwingi naishi Dar es Salaam. Je, ukienda mkoani? Nikawajibu, ni mara ngapi kwa mwaka naenda mikoani? Na nikienda hata robo mwaka haifiki narudi hapa hapa. Zaidi ntakaa week 2 tena za likizo. Kuna bank kuhamisha pesa toka bank kupeleka Tigo/voda ni bure ila kila mwisho wa mwezi unakatwa sh 250/- hata kama wamepandisha siku hizi, basi tuseme 500/- bado ni nafuu sana.

Lakini kwa nini utumie simu? Wakati kuna visa?
Kuna bank kutoa kwa visa unakatwa sh 3,000 bila kujali kiasi unachotoa. Wakati tigo kutoa laki 2 ni elfu 5. Kuna kipindi mzee alikua anaumwa kalazwa hospitali, na mimi ndio nilikua caretaker. Kuna gharama kule hospitali haziko kwenye bima, sasa ndugu na jamaa wakawa wanataka wanitumie pesa kwa simu, haki nakwambia niliwapa account yangu ya bank. Mtu akihoji niende kwa bank muda huu sijui bla bla namwambia nenda kwa wakala niwekee juat like unavyoenda kuweka tigopesa.
Ilisave sana gharama za kutolea pesa. Maana nikienda ATM navuta laki 2 mpaka 4 kwa buku wakati tigopesa ningetakiwa niwaachie elfu 10 hapo.

Cha msingi ni taarifa.
 
Kitu kizuri umeweka na kiasi,

Imagine unatoa elfu kumi wanakata 1000, ambayo ni 10% Hii si ni balaa kabisa na bado wadau wanakomaa huko huko
 
Back
Top Bottom