Kwanini tunampongeza na kumsifia hata sisi wafuasi wa Vyama pinzani?

Kwa muktadha huu sisi Watanzania kwa pamoja bila kujali chama tulipata mateso sawa kwa miaka mitano iliyopita,na Sasa mama anatuletea faraja Watanzania wote wanaCCM na ambao sio Wana CCM.
Hahaaa, wapinzani wanapoongoza kuunga mkono juhudi, hapo ndo unajua kondoo kwa kihindi inaitwaje !
 
Uko sahihi sana.
Lini saccos itashika dola mkuu?. Jengeni saccos yenu, ccm ni ileile awe Samia awe nani kinachotekelezwa ni ilani ya chama dume basi. Ninyi vyama mitetea,jiandaeni kukaa 2025 kama mlivyokaa Oct 2020.
 
Ni punguani peke yake ndiye anaweza kumsifia Mama kwa sababu bado anaongoza nchi kwa kutumia zile sheria kandamizi za Magufuli.Nchi huwa inaongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa maneno matamu na ahadi za matumaini.Kuongoza nchi kwa maneno matamu na ahadi za matumaini wakati sheria ni mbovu na kandamizi hilo huwa ni changa la macho!
Siyo rahisi kugeuza mwelekeo wa meli kubwa. Tunampongeza kwa hayo machache aliyoanza nayo. Mambo si rahisi, hata yeye ana maadui. Tunamhimiza aendelee kuleta mabadiliko
 
Mtu akiwa Rais hata kwa kupindua nchi Ni Rais huyo,

Akiwa Rais kwa kuchaguliwa kidemokrasia Ni Rais huyo,
Akiwa Rais kwa kuiba kura ni Rais huyo.

Mtu aliyekalia kiti Cha Urais Ana Upanga wenye ncha Kali,Ana Maamuzi .

Hivyo akifanya mambo mazuri yanawafikia wote wasio wapinzani na wapinzani,
Akifanya mambo mabaya yanawapata watu wote wapinzani na wasio wapinzani.

Kwa muktadha huu sisi Watanzania kwa pamoja bila kujali chama tulipata mateso sawa kwa miaka mitano iliyopita,na Sasa mama anatuletea faraja Watanzania wote wanaCCM na ambao sio Wana CCM.

Hivyo nafuu ya mateso tunayoipata tuna Haki ya kumpongeza,Kwa sababu anafanya vizuri kuliko yule Bingwa.
Akikosea tutamkosoa,sisi wapinzani sio wanafiki.

Tukipinga mnasema kila kitu tunapinga,
Tukisifu au kupongeza mnasema tumekwisha.

Hata hivyo Leo hii ukija uchaguzi Mkuu Mimi Lee nitaikataa CCM na mambo yake yote,
Na fahari zake zote,
Na hila zake zote.

Tunaomba katiba nzuri na mpya,
Tuanomba tume huru ya uchaguzi,
Tunaomba Uhuru wa shughuli za kisiasa.
Na huo ndio uungwana, sifa ya mtu mzigo yakhee
 
Siyo rahisi kugeuza mwelekeo wa meli kubwa. Tunampongeza kwa hayo machache aliyoanza nayo. Mambo si rahisi, hata yeye ana maadui. Tunamhimiza aendelee kuleta mabadiliko
Mimi namlaumu sana Mama na sikubaliani nae kwa maneno yake matamu kwa sababu Taifa huwa linaongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa mujibu wa maneno matamu.Yeye leo alipaswa atoe ahadi kuwa atafuta sheria zote kandamizi ambazo alitunga yeye pamoja na magufuli ila hakufanya hivyo.Hilo ndilo ambalo lingetupa matumaini.Maneno yake matamu hayana faida yoyote kwetu kwa sababu siku zote maneno matamu huwa ni mtaji wa wanasiasa katika kuhadaa watu ili watimize malengo yao mabaya.Hata Hitler aliwapa maneno matamu wananchi wa Ujerumani hadi wakamuamini na kumpa uwaziri mkuu kisha akaanza kuwaua kama Kuku.
 
Kusema kweli hi pointi yako ya kutangaza kufuta sheria kandamizi Ni nzuri Sana,naomba uiandikie thread yenye nyama na facts za kutosha ili wahusika waione na ijadiliwe kusudi iwe Kama moja ya matakwa ya wananchi wanaotaka ukandamizaji uondolewe.
 
Mkuu tayari nimeianzishia uzi comprehensive kule kwenye jukwaa la siasa.
 
Wasukuma mnaumia sana Mama akipata uungaji mkono toka kwa Wapinzani,tunajua kabisa mnayo movement yenu ya kumhujumu Mama lakini kamwe hamtafanikiwa mashetani wakubwa nyie.

Ningependa usituhusishe sisi Wasukuma na agenda za kisiasa. Tuheshimiane mkuu
 
Back
Top Bottom