Kwanini tunalazimishwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa tupo Awamu ya Sita wakati Kiuhalisia bado tupo Muhula wa Pili wa Awamu ya Tano?

Krav Maga

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,625
2,000
Rais Mama Samia Suluhu Hassan nitakuwa wa mwisho Kukuamini kuwa tupo Awamu ya Sita kama unavyotulazimisha.

Ninachojua tu Generalist na naamini hata wale Waliobarikiwa vyema Akili ni kwamba tupo bado Awamu ya Tano ya Muhula wake wa Pili ( wa mwisho), ila Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Sita.

Rais Mama Samia Suluhu Hassan nitakubaliana nawe kuwa tupo Awamu ya Sita pale tu ukichukua Fomu na Kugombea Urais na ukashinda kuanzia mwaka 2025.

Rais wa Awamu ya Tano alikuwa ni Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na Wewe kuwa Makamu wake na alipofariki Kikatiba ukaapishwa Wewe kuendelea ndani ya Awamu hii kstika Muhula wake wa mwisho.

Nasikitika tu kuona kuna waliomuamini.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,813
2,000
Kawaida imekuwa kwamba huko CCM lazima Rais mmoja aongoze vipindi viwili, naona hapo ndipo tatizo linapoanzia, kama akitokea Rais akaongoza muhula mmoja then amuachie mwingine naamini hii story ya awamu itabadilika.

Samia angekuwa Rais wa awamu ya sita kama angeanzia mwanzo baada ya kufanyika uchaguzi mkuu agombee na ashinde, lakini kama amekuja kumalizia kazi iliyoanzishwa na mwenzake yeye akiwa makamu basi yeye bado ni Rais wa awamu ya tano anaemalizia awamu waliyoianza na mwendazake.
 

Akili 7

JF-Expert Member
Apr 22, 2019
487
1,000
We ni kilaza,hivi aufahamu kuwa kuna uchaguzi kila miaka mitano je kama magufuli angeshindwa na lisu tungesema lisu anaendeza awamu ya tano.

Hapo nafikiri aujaelewa,hebu fikiria kama membe angechukua fomu na magufuli kutokupitishwa alafu membe awe rais ingekuwa ni hawamu ya tano tena?.

Kwa ufupi hawamu ni vichwa vya marais ndio maana kila hawamu kunakuwa na rais bila kujali muda alioudumu kwa taarifa yako Samia ni rais wa sita wa tanzania .
 

masare

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
445
1,000
Rais wa Zanzibar wa sasa Dkt. Hussein Mwinyi ni Rais wa awamu ya nane kule Zanzibar. Sasa jiulize hao marais nane wa awamu zote nane walifanya uchaguzi ndio ikaanza kuhesabiwa upya au.....!!.

Simple logic ni kuwa anapoingia madarakani Rais mwengine unaanza kuhesabiwa awamu mpya rejea mfano wa Zanzibar
 

masare

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
445
1,000

Biggs

JF-Expert Member
May 3, 2014
544
500
Rais Mama Samia Suluhu Hassan nitakuwa wa mwisho Kukuamini kuwa tupo Awamu ya Sita kama unavyotulazimisha.

Ninachojua tu Generalist na naamini hata wale Waliobarikiwa vyema Akili ni kwamba tupo bado Awamu ya Tano ya Muhula wake wa Pili ( wa mwisho )

Rais Mama Samia Suluhu Hassan nitakubaliana nawe kuwa tupo Awamu ya Sita pale tu ukichukua Fomu na Kugombea Urais na ukashinda kuanzia mwaka 2025.

Rais wa Awamu ya Tano alikuwa ni Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na Wewe kuwa Makamu wake na alipofariki Kikatiba ukaapishwa Wewe kuendelea ndani ya Awamu hii kstika Muhula wake wa mwisho.

Nasikitika tu kuona kuna waliomuamini.
Kama hili linakukera endelea kuamini unachokiona ni sahihi kwa upande wako.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom