RRONDO
JF-Expert Member
- Jan 3, 2010
- 51,719
- 107,817
Mara nyingi tumekuwa tukilaumu au kuwashangaa watu wenye simu za gharama hadi 3m huku hawana kazi au wanalalamika hawawezi kujiajiri kwa kukosa mitaji. Tunawashangaa kwasababu hela hio alionunulia simu au alionunuliwa simu ingeweza kumpa mtaji mdogo ambao akiwa makini anaweza kuukuza ukawa mkubwa zaidi hadi kuajiri wengine.
Mfano kuna biashara ya bodaboda, kwa gharama hio ya 2-3m unaweza kupata pikipiki mpya kabisa ukaitumia kama bodaboda wewe mwenyewe. Ukimpa mtu mwingine itakupasua kichwa, ukiwa nazo mbili au zaidi unaweza kumuachia moja mtu mwingine si mbaya sana kuliko ukiwa na ya ngama halafu umuachie mtu. Kwenye bodaboda nina mfano hai. Kwenye kijiwe changu kuna bodaboda maalum huwa namtumia kwa delivery, amini usiamini huyu kijana kwa siku nampa safari zinazomuingizia si chini ya 20,000/-.Na wakati mwingine namtafuta simpati inabidi nimsubiri arudi kwenye trip za watu wengine. Sasa fikiria kwangu anaingiza 20,000/- je akiongeza na kwa wengine anaingiza ngapi kwa siku?
Unatakiwa uwe smart na muhimu zaidi mwaminifu. Huyu kijana nilipata contact zake kwa jirani yangu ambae ndio alianza kumtumia akaniambia ni mwaminifu sana. Sasa hivi hata wateja wangu wanamtumia kwa trip zao nyingine, wapo wateja wa mikoani wanamtuma Kariakoo na sehemu nyingine akawachukulie bidhaa na kuwatumia kwenye bus kwasababu washajua ni mwaminifu. Siri kubwa ya mafanikio ni uaminifu. Huu ni mfano mmoja tu ipo mingi sana.