Kwanini tunalaumu Mtu mwenye simu ya Gharama halafu analia hana kazi/mtaji?

Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
64,114
2,000
Ubaya wahenga hawaja sema ni nywele za wapi ko unaruhusiwa ku comment

Babu nimekumiso
Hahahhaa wahenga hawana maana kumbe... looo

Mekumisi pia. Twenzetu basi inbobo

Tukirudi hapa tunakuta wazo la biashara lishapatikana... tunauza simu, kazi inaendelea
 

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
13,808
2,000
Wengi wao wamekata tamaa,watasema maisha ni haya haya, na vyote vilivyopo madukani natakiwa nivitumie n.k Ila kwa 'mind set' ya kitajiri ni kuwekeza kwenye vitu vinavyozalisha,umelala usingizi pesa inaingia. Pia kama una 'asset' ambazo hazitengenezi pesa, ni sawa na kazi bure.
clo.jpg
 

Hardbody

JF-Expert Member
Jan 25, 2017
2,504
2,000
Mara nyingi tumekuwa tukilaumu au kuwashangaa watu wenye simu za gharama hadi 3m huku hawana kazi au wanalalamika hawawezi kujiajiri kwa kukosa mitaji. Tunawashangaa kwasababu hela hio alionunulia simu au alionunuliwa simu ingeweza kumpa mtaji mdogo ambao akiwa makini anaweza kuukuza ukawa mkubwa zaidi hadi kuajiri wengine.

Mfano kuna biashara ya bodaboda, kwa gharama hio ya 2-3m unaweza kupata pikipiki mpya kabisa ukaitumia kama bodaboda wewe mwenyewe. Ukimpa mtu mwingine itakupasua kichwa, ukiwa nazo mbili au zaidi unaweza kumuachia moja mtu mwingine si mbaya sana kuliko ukiwa na ya ngama halafu umuachie mtu. Kwenye bodaboda nina mfano hai. Kwenye kijiwe changu kuna bodaboda maalum huwa namtumia kwa delivery, amini usiamini huyu kijana kwa siku nampa safari zinazomuingizia si chini ya 20,000/-.Na wakati mwingine namtafuta simpati inabidi nimsubiri arudi kwenye trip za watu wengine. Sasa fikiria kwangu anaingiza 20,000/- je akiongeza na kwa wengine anaingiza ngapi kwa siku?

Unatakiwa uwe smart na muhimu zaidi mwaminifu. Huyu kijana nilipata contact zake kwa jirani yangu ambae ndio alianza kumtumia akaniambia ni mwaminifu sana. Sasa hivi hata wateja wangu wanamtumia kwa trip zao nyingine, wapo wateja wa mikoani wanamtuma Kariakoo na sehemu nyingine akawachukulie bidhaa na kuwatumia kwenye bus kwasababu washajua ni mwaminifu. Siri kubwa ya mafanikio ni uaminifu. Huu ni mfano mmoja tu ipo mingi sana.
Huwa inaleta confusion sana Mkuu usimlaumu tu mtu wa aina hiyo kwasababu ni moja ya vitu ambavyo vinahitaji uwe focused kweli kweli kuignore simu kali zinazotoka siku hizi utumie kisimu cha kawaida tu ili uwekeze kwenye mambo ya msingi.
Huhitaji uwe na nguvu ya ndani sana kushinda vishawishi vya simu km iPhone na Samsung mkuu mfano S21 unaiachaje?
 

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
45,581
2,000
Huwa inaleta confusion sana Mkuu usimlaumu tu mtu wa aina hiyo kwasababu ni moja ya vitu ambavyo vinahitaji uwe focused kweli kweli kuignore simu kali zinazotoka siku hizi utumie kisimu cha kawaida tu ili uwekeze kwenye mambo ya msingi.
Huhitaji uwe na nguvu ya ndani sana kushinda vishawishi vya simu km iPhone na Samsung mkuu mfano S21 unaiachaje?
Nguvu Ya ndani kushinda vishawishi. Muhimu sana.
 

OllaChuga Oc

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
16,918
2,000
Maboss kama akina @PRONDO, Asprin, na wengineo hapa munakuwa wabahili hivi sisi kajamba nani tufanyeje? Kama pesa ipo nunua simu Kali tu ..usione ubahili kutumia 3M kununua simu. Sisi wenye Vodafone zetu tupambane na hali zetu.

NB: kama pesa ipo, kama hakuna pesa za kutosha acha hayo mawazo ya simu za M3 wewe nunua zako Techno Y4 kisha pambana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom