Kwanini tunalaumu Mtu mwenye simu ya Gharama halafu analia hana kazi/mtaji?

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
45,581
2,000
Mara nyingi tumekuwa tukilaumu au kuwashangaa watu wenye simu za gharama hadi 3m huku hawana kazi au wanalalamika hawawezi kujiajiri kwa kukosa mitaji. Tunawashangaa kwasababu hela hio alionunulia simu au alionunuliwa simu ingeweza kumpa mtaji mdogo ambao akiwa makini anaweza kuukuza ukawa mkubwa zaidi hadi kuajiri wengine.

Mfano kuna biashara ya bodaboda, kwa gharama hio ya 2-3m unaweza kupata pikipiki mpya kabisa ukaitumia kama bodaboda wewe mwenyewe. Ukimpa mtu mwingine itakupasua kichwa, ukiwa nazo mbili au zaidi unaweza kumuachia moja mtu mwingine si mbaya sana kuliko ukiwa na ya ngama halafu umuachie mtu. Kwenye bodaboda nina mfano hai. Kwenye kijiwe changu kuna bodaboda maalum huwa namtumia kwa delivery, amini usiamini huyu kijana kwa siku nampa safari zinazomuingizia si chini ya 20,000/-.Na wakati mwingine namtafuta simpati inabidi nimsubiri arudi kwenye trip za watu wengine. Sasa fikiria kwangu anaingiza 20,000/- je akiongeza na kwa wengine anaingiza ngapi kwa siku?

Unatakiwa uwe smart na muhimu zaidi mwaminifu. Huyu kijana nilipata contact zake kwa jirani yangu ambae ndio alianza kumtumia akaniambia ni mwaminifu sana. Sasa hivi hata wateja wangu wanamtumia kwa trip zao nyingine, wapo wateja wa mikoani wanamtuma Kariakoo na sehemu nyingine akawachukulie bidhaa na kuwatumia kwenye bus kwasababu washajua ni mwaminifu. Siri kubwa ya mafanikio ni uaminifu. Huu ni mfano mmoja tu ipo mingi sana.
 
nileo

JF-Expert Member
Sep 14, 2021
455
500
Unakuta jumla ya mavazi aliyovaa gharama yake ni kuanzia laki na simu Kali vyote toleo jipya kabsa na kuhonga yumo tena sana ila bado anakuambia life humu mtaji hana huwa nawashangaa sana
 
andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
2,289
2,000
Kuna tofauti ya kuitokuwa na Pesa/Kipato na kutokuwa na kazi.Kuna watu wengi sana ambao wanaishi maisha ya kuunga unga kwa ndugu,wazazi na marafiki na wanatoka katika familia zinazojiweza kikipato.Wanachokosa na kazi itakayowawezesha kuwa PRODUCTIVE hasa kwa kuzingatia SKILLS,EXPERIENCE na ASPIRATIONS/NDOTO zao.Kwa mafano wapo wengi ambao wanao mtaji wa kuuza GENGE au KARANGA lakini je,NDOTO ZAO na EXPERIENCE yao na SKILLS zao zinawatuma kuuza KARANGA?Jibu ni hapana.

SO tusiwalaumu wanaomiliki IPHONE latest kwa sababu wengine wanahongwa tu.TUJIULIZE JE tuna fanyeje ILI NCHI YETU iwe TAIFA la WATU kutimiza NDOTO zao badala ya kuishi maisha ya kuokoteza?
 
Kupanga ni kuchagua. Unaweza ukachagua ukae kusubiri kazi ya ndoto zako hata miaka kumi au ufanye kitu kingine uingize kipato wakati unasubiri hio kazi ya ndoto zako.
 
Nuzulati

JF-Expert Member
Nov 25, 2020
2,793
2,000
Sasa wenye vipara wanaruhusiwa ku-comment?

Kuna kabaamedi hapa Bunju kana simu ya laki 7. Lakini kanaomba vocha ya 500. Mshahara wake elfu 80. ... ila kuna wanaume wanajua kuhonga wallah...
Ubaya wahenga hawaja sema ni nywele za wapi ko unaruhusiwa ku comment

Babu nimekumiso
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom