Kwanini tunakufa?

Habari wana jamvi, natumai wote mu wazima na mimi kwa upande wangu ni mzima na bukheri wa afya.

Kama heading inavyosema hapo, nataka kujua ki undani zaidi kwanini tunakufa? Na kwanini binadamu akifa anashindwa kufufuliwa, kama tatizo lilikuwa ni figo kufeli kwanini baada ya kufa marehemu akiwekewa figo nyingine hafufuki?

Maana katika maisha ya kawaida kitu kikiharibika kabisa kama vile gari kikiwekewa kitu kipya kinapona na kinarudia hali yake ya mwanzoni.
katika hali ya kawaida kabisa binadamu tuna kua kwa kisayaynsi wanaita aging na kila kitu katika mwili wa binadamu kinakua kuanzia moyo na organ zote zinakua na tunavozidi kuishi ndivyo zinapozeeka na kukosa ufanisi wa kufanya kazi sasa mtu anapofikia hatua ya kufariki maana yake kuna mfumo mmoja wa kwenye mwili wake umeshindwa kuafanya kazi na unaingilia mfumo mwingine na mwisho system zote zina zima na hiko ndio kifo.....mtu kwa mfano akiiugua figo kinacho muua sio figo ila ni madhara ya figo kutofanya kazi vizuri na kuingilia mifumo mingine nayo inaharibika na inakosa ufanisi wa kufanya kazi na ikifika system ikashandwa kuafanya kazi kabisa hiko ndio kifo
 
Hatufi bali miili yetu Ndio inakufa.

Sisi ni Uhai ulio Hai daima.
Hatuonekani kwa macho ya mwili.

Habari wana jamvi, natumai wote mu wazima na mimi kwa upande wangu ni mzima na bukheri wa afya.

Kama heading inavyosema hapo, nataka kujua ki undani zaidi kwanini tunakufa? Na kwanini binadamu akifa anashindwa kufufuliwa, kama tatizo lilikuwa ni figo kufeli kwanini baada ya kufa marehemu akiwekewa figo nyingine hafufuki?

Maana katika maisha ya kawaida kitu kikiharibika kabisa kama vile gari kikiwekewa kitu kipya kinapona na kinarudia hali yake ya mwanzoni.
 
Unauhakika gani Kuwa Biblia Ndio jibu? Sio Quran, Bhavagad Gita au vitabu vingine vya dini?

nje ya bibilia Hakuna Jibu la kweli mkuu.
Yote haya yalianza miaka zaidi ya 6000 hapo mashariki ya kati maeneo ya Iraq. Karibu na mto tigris ilipokaa bustani nzuri
ya Eden. Kwingine kote utadanganywa. Na summary yake ipo kitabu cha mwanzo 1,2,3.

Ukielewa vizuri ndio utauliza maswali mapya.
1:Kwa nini Kiyama?
2:Kwa nini kondoo/ndama alichinjwa mtu akimkosea Mungu?
3:Kwa nini Yesu Afe?
4:Ni nini Dawa ya kifo?
5:Kuna kufa mara ngapi? Kwa nini hupaswi kuogopa kifo hiki tunachokiona sasa (Temporal death)?
 
1. Biodiversity
Mimea/majani yataliwa na mbuzi na mbuzi tutamla sisi binadamu na sisi inabidi tufe tuliwe na mchwa halafu mchwa waliwe na kuku etc "kufa kufaana"

2. Siri ya uhai anayo Mungu mwenyewe. Hakuna mwanasayansi alieweza kumpatia uhai na kumfanya binadamu kupumua hata maroboti hayatumii roho "roho ni siri ya muumba"

3. Hukumu kwa makosa tuliyofanya ili tukaishi maisha ya milele baada ya kufa. Kuna watu wamechinjwa, wamebakwa, wamekatwa viungo km albino, wamedhulumiwa lazima wapate hukumu ya makosa waliowayo wafanyia wenzao, Haki inabidi ipatikane na sifa ya Mungu ni mtenda haki hana dhulma.

Gari likiharibika tairi tunalibadilishia tairi na mtu akiharibika figo tunabadilisha figo. Binadamu atakapokufa inabidi tumrudishe alipotokea asili ya baba yetu Adam ni udongo.
:eek::eek::eek:
 
Kwanza tuanze na tafsiri yenyewe ya kifo. Kifo hutokea pale uhai unapotoweka, uhai ni nadharia ngumu kuielezea. UHAI ni nini? Formation ya UHAI ikoje? Maana mtoto anaanza kuwa hai anapoanza kujengeka tumboni. Sasa huo uhai unatoka wapi?

Na kwa kuwa binadamu tunapokosa majibu ya maswali yetu au suluhisho la matatizo yetu huwa tunamrudia Mungu na kusema ndiye anayo majibu ya maswali yetu na suluhusho la matatizo yote. Naamini ipo siri ya UHAI ambayo bado haijajulikana.

Binafsi naamini kuwa MUNGU yupo. Na ndiye anayetoa uhai kwa viumbe hai. Ila kifo ni pale uhai unapokosekana.Hivyo ili kukwepa kifo ni kujua namna ya kuutengeneza au kuurudisha uhai. Japo baadhi ya vifo hupelekea mwili kuharibiwa na hivyo hata kama formula ya uhai ikipatikana sio rahisi kwa baadhi ya vifo kuviepuka.

Mfano mtu akiungua moto, au akilipuliwa na bomu akapasuka vipande vipande, huyo sidhani kama anaweza kurudishwa hata kwa maombi. Lakini pale uhai unapokosekana na mwili upo na viungo vyake vyote ni MUNGU pekee anao uwezo wa kurudisha uhai.

Hata kwenye Biblia tunaona Yesu alimfufua Lazaro siku kadhaa baada ya kuzikwa ijapokuwa mwili wake ulianza kunuka. Pia mifano ya wote alio wafufua walikuwa na miili iliyo kamili. Sijaona sehemu kwenye agano jipya mtu ameungua kisha majivu yakafufuliwa na kufanya mwili na kisha uhai ukarudi.

Hata Yesu mwenyewe alifufuka akiwa na mwili wake uleule uliopigiliwa misumari.

Nawasilisha
 
Unapozaliwa unakua umepewa siku zako za kukaa huku duniani kwa maana hiyo unakua na miezi yako kipindi na nyakati za kuepo juu ya uso wa dunia kipindi Chako kiisha hakuna namna lazima uondoke (ufe)

Na ndo kwa maana ukienda makaburini utaona kabisa mwenye kaburi inaandikwa siku ya kuzaliwa na siku ya kufa kuonyesha kwamba ulikua na kipindi Fulani juu ya uso wa dunia

Wakiti tukiwa hai (tunaushi kwa kusudi maalum)

Ile kwamba tunaishi Kuna kusudi kabisa la sisi kuishi na kusudi la kuishi kwako likitimia hakuna sababu ya wewe kuendelea kua hai

Na kwa wakati mwingine kwa kua tunaushi kana kwamba hakuna kusudi la sisi kuishi Basi hapo kifo kinakua karibu Sana
 
Habari wana jamvi, natumai wote mu wazima na mimi kwa upande wangu ni mzima na bukheri wa afya.

Kama heading inavyosema hapo, nataka kujua ki undani zaidi kwanini tunakufa? Na kwanini binadamu akifa anashindwa kufufuliwa, kama tatizo lilikuwa ni figo kufeli kwanini baada ya kufa marehemu akiwekewa figo nyingine hafufuki?

Maana katika maisha ya kawaida kitu kikiharibika kabisa kama vile gari kikiwekewa kitu kipya kinapona na kinarudia hali yake ya mwanzoni.
Mtu akiwa anakufa ...ubongo na cell zake ndio znazoanza kuharibika..tatizo lipo hapo.
 
Habari wana jamvi, natumai wote mu wazima na mimi kwa upande wangu ni mzima na bukheri wa afya.

Kama heading inavyosema hapo, nataka kujua ki undani zaidi kwanini tunakufa? Na kwanini binadamu akifa anashindwa kufufuliwa, kama tatizo lilikuwa ni figo kufeli kwanini baada ya kufa marehemu akiwekewa figo nyingine hafufuki?

Maana katika maisha ya kawaida kitu kikiharibika kabisa kama vile gari kikiwekewa kitu kipya kinapona na kinarudia hali yake ya mwanzoni.
Daaah!
 
Ukifa na chanzo kilikua figo haina maana figo pekee ndo ilikuua. Figo itafeli, kibofu kitapata shida, utapata maambukizi chungu mzima, na mwisho ubongo na moyo navyo vitakufa. Kwahio kwa mtiririko huo utahitaji kubadilisha vitu vingi sana sio figo pekee. Na pia gari halina uhai
 
soma vifungu ktk maandiko matakatifu na si theories za wanasayansi
Habari wana jamvi, natumai wote mu wazima na mimi kwa upande wangu ni mzima na bukheri wa afya.

Kama heading inavyosema hapo, nataka kujua ki undani zaidi kwanini tunakufa? Na kwanini binadamu akifa anashindwa kufufuliwa, kama tatizo lilikuwa ni figo kufeli kwanini baada ya kufa marehemu akiwekewa figo nyingine hafufuki?

Maana katika maisha ya kawaida kitu kikiharibika kabisa kama vile gari kikiwekewa kitu kipya kinapona na kinarudia hali yake ya mwanzoni.
 
Hapo ndipo ukomo wa ufikiri wa mwanadamu - Hakuna sayansi hadi leo imegundua namna ya ku huisha cell zilizochoka za mwilini na kuwa mpya....au kuzuia zisizeeke..

Tukigundua ku-huisha cell hizo za mwili zisichoke milele basi tutakuwa tunakaribia kuunda mwanadamu wetu wenyewe...
 
kifo ni kitu cha kawaida na muhimu na kipo kwa kila kiumbe hai ili kuweka balance kati ya viumbe hai. Ni asili ya kila kiumbe kuepuka kifo kadri iwezekanavyo lakini kifo pia ni kitu cha asili ambacho kipo kuhakikisha Maisha yanaendelea kuwa mapya na yapo katika usawa. Vitu vinavyosababisha tunakufa na wanayama wengine wanakufa vipo vingi tu.

Kwanini hatuwezi kufufua? ni kwa sababu bado hatujafikia kuwa na technolojia ya kutosha ya kuwa na uwezo huo. Mimi naona uwezekano wa sayansi na teknolojia kukua kiasi cha kuweza kurudisha uhai. wapo watu wanaoamini sana katika uwezekano huu. Hao watu huitunza miili yao vizuri baada ya kifo bila kuharibika wakisubiri teknolojia ikue vya kutosha wafufuliwe. ukitaka kufahamu zaidi soma kuhusu "Cryonics"
 
Hakuna uhakika kwamba binadamu watashindwa kufufua milele au watashindwa kutengeneza uhai milele. kunayo mafanikio mengi katika research zinazohusiana na kujaribu kutengeneza uhai. watu wengi hawajui hizo success kwa kua hawapendi kuamini kwamba inawezekana na wapo too obsessed na dini zao kiasi kwamba hawataki kuamini kwamba binadamu anaweza kufikia uwezo wa kufufua au kutengeneza uhai.
 
kifo ni kitu cha kawaida na muhimu na kipo kwa kila kiumbe hai ili kuweka balance kati ya viumbe hai. Ni asili ya kila kiumbe kuepuka kifo kadri iwezekanavyo lakini kifo pia ni kitu cha asili ambacho kipo kuhakikisha Maisha yanaendelea kuwa mapya na yapo katika usawa. Vitu vinavyosababisha tunakufa na wanayama wengine wanakufa vipo vingi tu.

Kwanini hatuwezi kufufua? ni kwa sababu bado hatujafikia kuwa na technolojia ya kutosha ya kuwa na uwezo huo. Mimi naona uwezekano wa sayansi na teknolojia kukua kiasi cha kuweza kurudisha uhai. wapo watu wanaoamini sana katika uwezekano huu. Hao watu huitunza miili yao vizuri baada ya kifo bila kuharibika wakisubiri teknolojia ikue vya kutosha wafufuliwe. ukitaka kufahamu zaidi soma kuhusu "Cryonics"
kaka unaongelea kufufua maiti wakati magonjwa yanayopelelekea watu kufa ndiyo yanaongezeka regardless hiyo sayansi unayosema inapanda kwa kasi sana.

Magonjwa kama Kansa, Kisukari, Pressure nk yote haya hayana dawa hadi muda huu na yanapukutisha watu ni balaa duniani kote sasa unategemea ni lini utapata hiyo technology ya kufufua maiti? Labda uniambie ufufue maiti iwe robot.....
 
Unapozaliwa unakua umepewa siku zako za kukaa huku duniani kwa maana hiyo unakua na miezi yako kipindi na nyakati za kuepo juu ya uso wa dunia kipindi Chako kiisha hakuna namna lazima uondoke (ufe)

Na ndo kwa maana ukienda makaburini utaona kabisa mwenye kaburi inaandikwa siku ya kuzaliwa na siku ya kufa kuonyesha kwamba ulikua na kipindi Fulani juu ya uso wa dunia

Wakiti tukiwa hai (tunaushi kwa kusudi maalum)

Ile kwamba tunaishi Kuna kusudi kabisa la sisi kuishi na kusudi la kuishi kwako likitimia hakuna sababu ya wewe kuendelea kua hai

Na kwa wakati mwingine kwa kua tunaushi kana kwamba hakuna kusudi la sisi kuishi Basi hapo kifo kinakua karibu Sana
wewe umejuaje kwamba kila mtu ana kusudi maalumu?
Hilo kusudi maalumu unapewa na nani?
na kila mtu kusudi lake anaelekezwa vipi na huyo mgawa kusudi?
kwa mfano wewe kusudi lako ni nini?
 
nje ya bibilia Hakuna Jibu la kweli mkuu.
Yote haya yalianza miaka zaidi ya 6000 hapo mashariki ya kati maeneo ya Iraq. Karibu na mto tigris ilipokaa bustani nzuri
ya Eden. Kwingine kote utadanganywa. Na summary yake ipo kitabu cha mwanzo 1,2,3.

Ukielewa vizuri ndio utauliza maswali mapya.
1:Kwa nini Kiyama?
2:Kwa nini kondoo/ndama alichinjwa mtu akimkosea Mungu?
3:Kwa nini Yesu Afe?
4:Ni nini Dawa ya kifo?
5:Kuna kufa mara ngapi? Kwa nini hupaswi kuogopa kifo hiki tunachokiona sasa (Temporal death)?
kwanini unasema kitabu cha mwanzo hakidanganyi wakati kitabu cha mwanzo kina makosa yafuatayo:
1. Mwanzo 2:2,3
Inasema Mungu alipumzika siku ya saba baada ya kumaliza uumbaji. inakuaje asiyechoka, mwenyeuweza wote akahitaji kupumzika au usingizi?
2. Mwanzo 2:17
Mungu alimuambia Adam asile tunda la mti wa kujua mema na mabaya. Mwanzo 3:5 inasema utapata kujua mema na mabaya endapo utakula tunda kutoka mti huo. Kwa maana hiyo wakati eva anakula tunda hakuwa na ufahamu wa mema na mabaya. Kwahiyo wakati anakula alikua nafanya kama vitendo vingine anavyofanya, manake hauwa na uwezo wa kuelewa maana hauwahi kula tunda hilo kabla.
3. Mwanzo 3:14
Inasema kwamba nyoka hula vumbi. hili halipo sawa kisayansi, hata watu ambao ni layman wanajua kwamba nyoka wanakula vitu ambavyo ni orgainic kama vile Wanyama wengine, mayai na vinginevyo lakini sio vumbi.
4.Mwanzo 3:14
Inasema nyoka kutembea kwa kutambaa kwa tumbo ni adhabu yake. Yaani kana kwamba hapo awali nyoka alikua anatembea kwa miguu alafu akanyang'anywa miguu ili atembee kwa shida. ila mimi nnavyomuona nyoka sioni kama anatembea kwa shida na kwanaza nashindwa kuelewa mtu mzima anawezaje kuamini kitu kama hichi.
5.Mwanzo 3:16
Inaonyesha kwamba kuzaa kwa uchungu ni adhabu. Adhabu kwa binadamu?? Lakini inajulikana kwamba Wanyama wengi tu wanapata maumivu wakati wa kuzaa. Fisi anazaa kwa shida sana na anapata maumivu makali sana wakati wa kuzaa (asilimia 18 ya kuzaa kwa fisi husababisha kufa kwa mama fisi) je hao Wanyama wengine walifanya amakosa gani mapaka wapate adhabu hiyo?

6.Kuna hadithi nyingi sana kwenye biblia ambazo hazina mantiki na hazipaswi kutiliwa maanani na mtu mzima. hadithi kama kuna lugha mbali mbali kwa kua hapo zamani binadamu walitaka kujenga mnara mrefu kumfikia mungu. hadithi kama mwanamke akizaa mtoto anakua najisi na akizaa mtoto wa kike anakua najisi Zaidi na hatakiwi kuhudhuria ibada kwa siku 66 ( walawi 12:5).

Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vya kale na katika kitabu hicho kuna vingi ambavyo haviendani na hali ya maendeleo ya binadamu kwa sasa. Yaani kwa kifupi kuna vitu vingi vimepitwa na wakati na havina uhalisia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom