Kwanini tunaendelea kusisitiza diplomasia kwenye kushughulikia matatizo ya kisiasa

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
Kwa muda sasa tumekuwa tukisisitiza kuwa matatizo ya kisiasa ni vyema kuyashungulikia kidiplomasia bila kujali yana ukakasi kiasi gani kwa sababu njia hiyo ndio yenye uwezekano mkubwa zaidi wa kuleta mafaniko kuliko zingine na faida yake ni kubwa kuliko hasara.

Wanaopinga mtizamo huo wana hoja kuu mbili;
 
Kwanza wanadai kuwa, kwa mazingira ya siasa za Tanzania diplomasia haiwezi kufanikiwa kutatua changamoto za kisiasa kwa uzoefu uliopo. na,

Pili wanadai kwamba kusisitiza diplomasia katika mazingira yaliyopo ni woga, kwa mantiki hiyo, sisi tunaosisitiza diplomasia mara kwa mara hatusukumwi na jambo lolote ispokuwa woga.
 
Kuhusu hoja ya kwanza hapo juu ya 'diplomasia kutofanya kazi'; sio kwa sababu utumiaji wa diplomasia ni tatizo bali ni kutokana na kukosekana kwa approach nzuri. Kwa hiyo zikitumika approach nzuri na kukiwa na u serious wa kutosha, changamoto nyingi zitatatulika kidiplomasia huku mafanikio makubwa yakipatikana na majanga yanayoepukika yakiepukwa.

Nitoe mfano ninaposema approach zinazotumia ndizo zinachangia diplomasia kukwama kwenye mambo mengi namaanisha nini?

kwa mfano unataka maridhiano na mtu au chama kwenye jambo la msingi sana na kila mtu anaona wazi ni jambo la msingi, lakini kabla au baada ya kumuita kwenye mazungumzo unayefikiri mnatakiwa kufanya maridhiano yapamoja kwenye mambo hayo ya msingi;unamuhakikishia kwamba lengo lako ni kummaliza/kumng’oa madarakani n.k, yaani unamuwekea mazingira toka mwanzo kabisa aone hayo mazungumzo/maridhiano kwake yana hasara 100% na kwako yana faida hapo unakuwa ushaharibu. Hilo si kosa la diplomasia bali ni kosa la mtu na mtu.

Msingi mkuu wa maridhiano ni kuuhakikishia upande wa pili kwamba maridhiano yatakuwa na faida kwa pande zote “Win win”. Vinginevyo, kuitisha maridhiano huku ukipuuza msingi huo, ni kujiandaa kufeli kabla ya kuanza. Kama ni wewe mtu akikuita mzungumze halafu kabla ya mazungumzo anakuhakikishia kuwa lengo la mazungumzo ni kukumaliza kwa namna moja au nyingine, bila kujali uzuri wa ajenda, wewe unaenda? kama ni mimi siendi, sio kwa sababu ya ubaya wa ajenda bali wasi wasi wa dhamira. Hilo linakuwa si tatizo la mazungumzo bali 'Approach'
 
CORONA TIMES!

AU UFIPA HAMPO NA WATANZANIA?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu korona sio suala la kujadili, ni suala la kutekeleza. Ushaambiwa korona ipo, umeambiwa uchukue tahadhari, umeelekezwa ni tahadhari gani za kuchukua na unachukuaje? hapo unataka tena mjadala gani zaidi ya utekelezaji?au ukiambiwa mara moja huelewi unataka uambiwe mara nyingi nyingi?

Au unatafuta wa kumlaumu?
 
Kuhusu hoja ya woga; dunia ya sasa inahitaji kutumia akili kuliko nguvu. Kwa hiyo ishu sio kuwa na woga au kutokuwa na woga, ishu unafanya nini ili iwe nini, na kwa nini unachagua kufanya unavyofanya na si vinginevyo.

Kujiepusha kutumia nguvu hakumaanishi mtu ni mwoga. Kabla ya kuamua kutumia njia fulani kutatua matatizo yaliyoko mbele yako, tathmini kwanza faida na hasara na % za uwezekano wa kufanikiwa kwa njia unayotumia; huo si woga bali akili.Si kila tatizo linaweza kutatuliwa kwa kutumia msuli na kwa kadiri siku zinavyoenda, utumiaji wa nguvu unazidi kupoteza ufanisi kwenye karibia kila kitu, umuhimu wa kutumia maarifa unaongezeka.
 
Ndio maana hata wamarekani walivyoshambuliwa na iran huko Iraq walikimbia, na hawakulipiza kisasi; sio kwa sababu hawawezi au ni woga bali wanatumia akili. Hata kurudi nyuma wakati mwingine sio woga ni akili, wakati mwingine kukimbia si woga ni akili, wakati mwingine kujishusha si woga ni akili, wakati mwingine kuwa mpoleee si woga ni akili wakati mwingine kutulia si woga.
 
Mada zako uwa ni nzito na uwa ni vigumu watu kukuelewa ila nataka kuchangia kwamba njia za diplomasia Tanzania kwa tulipofikia haziwezi kufanikiwa kwa msukumo wa ndani ya nchi, labda msukumo wa nje itawezekana. ndani kinachoweza kuleta tija ni resistance pekee.
 
Hoja ya ziada;

Haijalishi upande wa pili unakukwaza kwa kiasi gani, kama huna mpango wa kupiga ngumi usikunje ngumi eti ili uonekana huna woga kwa sababu ukikunja ngumi, upande wa pili unaweza kudhani unataka kupigana na ukakushambulia kumbe wewe wala hata hukuwa na nia hiyo.Kwa hiyo usiwe unakunja ngumi eti tu kuonesha watu wewe si mwoga, hiyo fikira si sawa.

Kutokukunja ngumi hakuashirii kwamba hukereki na jambo fulani, au wewe ni mdhaifu, bali huonesha unatumia akili.Jaribu kutulia fikiri kwa kina ni njia gani inaweza kuleta matunda bora Zaidi kwa gharama kidogo. Kuna muda huwa tunaona watu wakielezana jinsi ambavyo hawaogopani, nadhani hiyo inaweza isiwe na faida sana.

Kwa hiyo kutatua changamoto zinazotukabili kuna njia nyingi lakini njia bora ni ile inayoleta matokea bora kwa madhara kibao.Kila mmoja kutaka kumuonesha mwenzake kwamba yeye si mwoga wakati hatusongi mbele na matatizo ya msingi yanabaki hayajatatuliwa, sioni kama ni uamuzi wa busara.
 
Kwa hiyo, tunaamini diplomasia haifeli, watu ndio hufeli.Tunaamini kutumia diplomasia kushughulikia masuala ya siasa kwa mazingira ya Tanzania inawezekana sana na kufanya hivyo si woga wala udhaifu bali ni kutumia akili na busara na huo ndio uongozi.

Viongozi wenye uwezo mzuri hushindana kuja na fikra na ubunifu bora zaidi kutatua matatizo yanayowakabili au kuikabili yamii waliyopo na sio kuoneshana nani ni nani, nani anaweza kutumia nguvu zaidi au nani hamuogopi nani.

Tukiweza kuyazingatia haya, tutaweza kufanikiwa kwenye mambo mengi ya msingi kwa namna bora zaidi.
 
Hii mada ni 'conceptual' Zaidi. Tukipata muda tutakuja na mada mahususi 'substantial' tutaeleza kwa kina ishu ya madai ya tume huru ya uchaguzi, madai ya katiba mpya, tutachambua kwa nini kuna mkwamo, kwa nini mkwamo unaendelea kuwepo, kwa nini kwa approach zinazotumika hazitaondoa mkwamo bali kutengeneza tatizo jipya, ni nini kinaweza kufanyika na kwa nini.n.k
 
Mada zako uwa ni nzito na uwa ni vigumu watu kukuelewa ila nataka kuchangia kwamba njia za diplomasia Tanzania kwa tulipofikia haziwezi kufanikiwa kwa msukumo wa ndani ya nchi, labda msukumo wa nje itawezekana. ndani kinachoweza kuleta tija ni resistance pekee.
Mkuu kuna shida zinajitokeza, ukijaribu kuziangalia unagundua kuwa, pamoja na kuwa na tatizo la msingi mahali,lakini 'immediate course' ya tatizo ni kila mtu kutaka kumuonesha mwenzake kwamba yeye si mwoga bila kutathimini kwamba kwa kufanya hivyo faida ni nini na hasara ni nini?na lengo ni ili iwe nini. Mwishowe unakuta mara nyingi badala ya kutatua linaloonekana ni tatizo la msingi; approach zinazotumika zinaibua mfululizo wa matatizo mapya.

Nadhani kama tungeweza kuuona ushauri unaotolewa humu na kuufanyia kazi, tungefanikiwa kwenye mambo mengi, tungepiga hatua kubwa na hakuna ambaye angejuta . Kila mtu angeishia kwenye 'win win'

Kwa bahati mbaya ni kwamba bado wengi hawajauona ushauri huu kama ni wakufaa na bahati mbaya zaidi huwa hakuna anayeeleza shida yake ni nini au huwa wanakwama wapi hasa. Ni kama vile watu wanakumbwa na kitu kinachowafanya washindwe kufikiri katika utaratibu wa kawaida.
 
Maridhiano ni jambo muhimu la kitaifa, lina maslahi kwa taifa kwa ujumla wetu, hivyo yeyote anayejaribu kuweka maslahi binafsi mbele kwa kuogopa kwenda kwenye meza ya mazungumzo kwasababu mwenzake kamwambia ataondolewa madarakani huo kwangu ni ubinafsi, analinda maslahi yake na chama chake zaidi ya maslahi ya taifa.

Tuzungumze ukweli kabisa; nia ya chama chochote cha upinzani ni kuingia madarakani, sasa kama utaogopa akikwambia anataka madaraka utakuwa unajidanganya, hakuna chama cha siasa kinachotaka kuishia kuwa cha upinzani miaka yote, ndoto za vyama pinzani siku zote ni wao nao wawe chama tawala.

Hivyo, nikaingalia njia ulizoorodhesha kuhusu kukimbia vitani ukasema sio uoga ni akili, mimi kwangu huo ni uoga na ubinafsi uliopitiliza. Wanaogopa kwenda kwenye meza ya mazungumzo sio kwasababu wataondolewa madarakani wakikanyaga chumba cha mkutano, bali ukweli ni kwamba, hawana cha kwenda kuongea kwenye hiyo meza, wataongea nini wakati Tume iliyopo inawalinda wao? inawafanya waendelee kutawala? ndio maana nasema hao watu ni wabinafsi wa madaraka, kwao kuendelea kutawala ni muhimu zaidi ya kuliunganisha taifa, maridhiano kwao hayana maana.

Juzi nimemsikia Polepole akizungumza kuhusu Corona, akasema atapambana na Corona kama anavyopambana na wapinzani, hivi akili ya mtu kama huyu unaweza kweli kuipeleka kwenye meza ya mazungumzo? kwasababu ili uende kwenye meza ya mazungumzo atleast uwe umejiandaa kiakili ujue nini utakwenda kuzungumza, but kwa huo mtazamo wa jamaa hapo juu leo umwambie twende kwenye mazungumzo unadhani ataongea nini? hana chakuongea, yeye anachowaza kwa sasa ni kuendelea kuwapiga wapinzani tu, ndio maana nasisitiza hao watu ni wabinafsi, wanataka Tume hii hii iendelee kuwepo milele ili waendelee kututawala.

Rais nae aliwahi kuulizwa kuhusu Tume Huru, akajibu hiyo haikuwepo kwenye ilani yake 2010, huyu nae anaonesha hayupo tayari kwa mazungumzo, hawana cha kwenda kuongea huko, hii Tume iliyopo kwao inawatosha, wameridhika nayo.

Mwisho nimalizie kwa kusema, kuwa na Tume Huru sio lazima mpaka Katiba Mpya ipatikane; nimewasikia baadhi ya watu wakisema kuwa na Tume Huru kwasasa haiwezekani, kwamba muda uliobaki mpaka kufanyika uchaguzi mkuu ni mfupi mno, huu nao kwangu ni mfano mwingine kuthibitisha hawapo tayari kuwa na Tume Huru, kama wanaweza kupitisha miswada ya dharura bungeni kwa maslahi yao binafsi kila wakitaka, kwanini washindwe hili la Tume Huru, jibu ni kwamba hawapo tayari, ni wabinafsi, Tume iliyopo inawatosha, vingine vyote ni visingizio tu.

Hivyo basi, ili pawepo na maridhiano lazima pande zote mbili ziwe tayari kwa mazungumzo, lakini kama upande mmoja upo tayari na upande mwingine haupo tayari, hayo maridhiano hayawezi kufikiwa, hivyo ustaadh Azizi ni vyema ukafahamu hilo, na hata mbinu yako ya diplomasia naona itachukua muda mrefu sana kutekelezeka.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom