Kwanini tuna wapinzani wengi mitandaoni ila uraiani hawaonekani?

Ukiingia mitandaoni unaweza kudhani kila kona ya tanzania utakutana na ofisi na bendera za wapinzani, maajabu ni kwamba tofauti na miaka kadhaa iliyopita bendera na ofisi za CCM pamoja na makada wanaovaa hizo sare utawapata kila kona ya nchi.

Naomba wapinzani watoke mitandaoni na kuendesha shughuli mitaani ili kuwafikia watanzania wa kawaida wasio na access ya mitandao.
Si mruhusu mikutano tatizo mnazuia mikutano ma vikao vya ndani alafu mnataka kupima numbers??

Dah, umepiga kwenye mshono. Wapinzani waanzie chini kujenga chama.
Always hata mtoto huanza kwa kutambaa kusimamia ukuta hatimaye anaanza hatua moja moja siyo lazima aliye mwenyekiti sasa ndiyo atarajie kuingia madarakani hebutujaribu kutengeneza plan za muda mrefu tukianza na huku chini kwenye raia wanashinda maeneo ya majumbani taratibu tukawajenga kisaikolojia wakatuelewa huku ndiyokwenye kundi kubwa la wapiga kura yaani kama kina mama wanaoshinda nyumbani ndiyo hao wanaendaga kupiga kura achasna na wanao shinda mijini na kuwa busy kwenye keyboard mitandaoni hata kura hawapigi hawa tujielekeze kwa hawa wa chini tukiwaweza hawa ni rahisi sana kuibadiri hii nchi ikaeewa upinzani unataka nini sasa hivi tuna lazimisha katiba ambayo hao wa chini hata hawajui umuhimu wake matokeo wanakuja kuona upinzani unaleta fujo kumbe ni kwamaslahi yao pia ila hawajui

nawasilisha
 
Mtandaoni ni sawa na katiba mpya kuna uwanja mpana wa ku explain mambo ila uraia ukiongea kidogo tu watu wana anza ki deal na ww
 
Ukifuatilia kwa umakini kabisa utabaini kuwa kundi lililopo mtandaoni linatofautiana kwa mbali sana na kundi ambalo kwa sehemu kubwa halingii mtandaoni ambalo ndilo kundi kubwa zaid
tena mkuu kundi kubwa liko vijijini na hata mijini wanaoshinda majumbani na maeneo ya makazi ambao hawaingii mitandaoni hebu tujenge upinzani kwanza huku chini tusi deal na watu wa mitandaoni tuimarishe mashinani kwanza wataelewa tu upinzani ukishakuwa na nguvu ya uma hata iweje watakubali tu bila hivyo yaani bila kuwa na nguvu ya umma upinzani utaonekana ni ukolofi tu sasa hivi hakuna nguvu ya ummma
 
Hilo ni wazo Baya Sana hivi ujui wanapo chart kwa wingi Kodi pia inalipwa? wanapo rumbana ndipo tozo inapatikana waache walipe Kodi kwa manufaa ya nchi
 
Hahahaha, lakini una hoja maridhawa kabisaaa...
Kwa hiyo Green Guard wanavyowahi kufagia nje ya ofisi za CHADEMA na mabarabani wapinzani wanapotaka kukuonyeshi kuwa tupo,.?! umeshasahu, au ndio mnajiongerasha tu kama kuku aliekatwa kichwa.

MaCCM akilizenu hazinaga akili.
 
Ukiingia mitandaoni unaweza kudhani kila kona ya tanzania utakutana na ofisi na bendera za wapinzani, maajabu ni kwamba tofauti na miaka kadhaa iliyopita bendera na ofisi za CCM pamoja na makada wanaovaa hizo sare utawapata kila kona ya nchi.

Naomba wapinzani watoke mitandaoni na kuendesha shughuli mitaani ili kuwafikia watanzania wa kawaida wasio na access ya mitandao.

kwa sababu wengi ni disapora japokua wengine hata sio raia wa tanzania
 
Ukiingia mitandaoni unaweza kudhani kila kona ya tanzania utakutana na ofisi na bendera za wapinzani, maajabu ni kwamba tofauti na miaka kadhaa iliyopita bendera na ofisi za CCM pamoja na makada wanaovaa hizo sare utawapata kila kona ya nchi.

Naomba wapinzani watoke mitandaoni na kuendesha shughuli mitaani ili kuwafikia watanzania wa kawaida wasio na access ya mitandao.
MaCCM mmeua watu, mmetesa watu, mmeteka watu, mmefunga watu, mmeshusha bendera za CHADEMA nchi nzima. Uchaguzi mnaomba msaada wa majeshi mpaka ya Burundi yawaibie kura./ maamuzi ya wananchi.
CCM Magufuli kawafutia ushawishi kwa watu, na hamtakaa mpate wafuasi’ nyie tumieni tu kodi na TOZO kuonga wakuongezea VICHWA.
 
Demokrasia ndio inapanuka hivyo zamani hata hao wa mtandaoni walikuwa hawapo. Mtandao umerahisisha mambo mengi kuwa bayana, kule kujificha na kuzuia taarifa zisifike kumepungua sana. Ndani ya masaa 2 issue ya Hamza bin Laden ilitapakaa dunia nzima.
 
Ukiingia mitandaoni unaweza kudhani kila kona ya tanzania utakutana na ofisi na bendera za wapinzani, maajabu ni kwamba tofauti na miaka kadhaa iliyopita bendera na ofisi za CCM pamoja na makada wanaovaa hizo sare utawapata kila kona ya nchi.

Naomba wapinzani watoke mitandaoni na kuendesha shughuli mitaani ili kuwafikia watanzania wa kawaida wasio na access ya mitandao.
Nikitaka kutukana lakini basi

Hivi unafikiri upinzani ni kama mawe kwamba lazima yaonekane?

Upinzani uko moyoni mwa wengi zaidi hata na hawa unaowaona mitandaoni.

Sitaki kueleza sababu za kwa nini hawaonekani nadhani unazifahamu kuliko nadhani hata nazozifahamu.
Kama unazifahamu sababu za kwa nini hawaonekani mtaani amini wewe ni mpinzani kindaki ndaki na umekosa nafasi tuu ya kuoonyesha.
 
Kwa hiyo Green Guard wanavyowahi kufagia nje ya ofisi za CHADEMA na mabarabani wapinzani wanapotaka kukuonyeshi kuwa tupo,.?! umeshasahu, au ndio mnajiongerasha tu kama kuku aliekatwa kichwa.

MaCCM akilizenu hazinaga akili.
Hahahh Yani hata hueleweki unaongelea kitu gani rafiki...
 
Hawa wapinzani unaowaona mtandaoni wengi ni wanaccm ambao hawawezi kijionesha mtaani kwa kuhofia bughuza kutoka kwa viongozi wao ambao wengi wana mawazo ya kisungusungu
 
Kwahiyo unawaza mapinduzi ili chadema mchukue nchi? Hilo gaidi lenu halina huo uwezo Kama wa aliyempindua Conde na hata jeshi likichukua nchi Haina maana kwamba Chadema ndo watakuwa wamechukua nchi.
Nyumbu hovyo kabisa.
Kitu hujui ni kwamba hawa wapinzani kupitua vyama vya siasa huwa ni asilimia chache saaaana kulinganisha na idadi ya wapinzani walio ndani selikari.

Jifunze kwa waliokuwa wanamsifu Alfa ndio hao hao waliomtunza sehemu salama
 
Ukiingia mitandaoni unaweza kudhani kila kona ya tanzania utakutana na ofisi na bendera za wapinzani, maajabu ni kwamba tofauti na miaka kadhaa iliyopita bendera na ofisi za CCM pamoja na makada wanaovaa hizo sare utawapata kila kona ya nchi.

Naomba wapinzani watoke mitandaoni na kuendesha shughuli mitaani ili kuwafikia watanzania wa kawaida wasio na access ya mitandao.
Mkuu, kwa nini hukupeleka hoja yako mtaani?
 
Ukiingia mitandaoni unaweza kudhani kila kona ya tanzania utakutana na ofisi na bendera za wapinzani, maajabu ni kwamba tofauti na miaka kadhaa iliyopita bendera na ofisi za CCM pamoja na makada wanaovaa hizo sare utawapata kila kona ya nchi.

Naomba wapinzani watoke mitandaoni na kuendesha shughuli mitaani ili kuwafikia watanzania wa kawaida wasio na access ya mitandao.
Mi mwenyewe sasahivi natafuta mademu mitandaoni maana huko mtaani siwaoni. Mwisho wa kunukuu
 
Ukiingia mitandaoni unaweza kudhani kila kona ya tanzania utakutana na ofisi na bendera za wapinzani, maajabu ni kwamba tofauti na miaka kadhaa iliyopita bendera na ofisi za CCM pamoja na makada wanaovaa hizo sare utawapata kila kona ya nchi.

Naomba wapinzani watoke mitandaoni na kuendesha shughuli mitaani ili kuwafikia watanzania wa kawaida wasio na access ya mitandao.
Waulize polisiccm
 
tokea jeshi la police na jeshi la ulinzi walipoacha majukumu yao kisheria na kuanza kuilinda ccm kwa gharama yoyote imekuwa ngumu sana kwa chadema kujitokeza mitaani wakihofia kuuwawa, kubambikiwa case za ugaidi, uhujumu uchumi na mauwaji.
 
Ukiingia mitandaoni unaweza kudhani kila kona ya tanzania utakutana na ofisi na bendera za wapinzani, maajabu ni kwamba tofauti na miaka kadhaa iliyopita bendera na ofisi za CCM pamoja na makada wanaovaa hizo sare utawapata kila kona ya nchi.

Naomba wapinzani watoke mitandaoni na kuendesha shughuli mitaani ili kuwafikia watanzania wa kawaida wasio na access ya mitandao.
Dunia sasa hivi ni ya kidigitali hivyo hao wapinzani wako mbele ya wakati. Hata katika nchi zilizoendelea kampeni kubwa hupigwa mitandaoni.

Na hii ilidhihirishwa na Donald Trump alipotumia Tweet vizuri na kumshinda Bi klinton. Toka hapo viongozi wote wakuu wa serikali wakaanza kutumia Tweet. Mama Samia alipokuwa anatweet, kijani wengi hawakumuelewa lakini wapinzani ilikuwa ni kawaida kwani huko ndiko Taifa linakokwenda.
 
Back
Top Bottom