Kwanini tumechagua umaskini?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Mtanzania hana nchi nyingine ya kwenda zaidi ya Tanzania ila raia wa kigeni wao wanaweza kuwa na pakwenda wakati wowote wanapochoka kuishi katika eneo flani.

Tulikaribisha wageni kwa miaka kumi mfululizo na tukawawekea Kinga ya kutokuguswa na vyombo vyombo vya Dolla Wala vyombo vya sheria, tukawamilikisha Mali kwa mikataba minono na ya muda mrefu. Watanzania wakanyonywa kwa mishahara midogo na kufanywa vibarua bila kujali elimu zao na kila aliyepinga rasilimali kuuzwa akaitwa si mzalendo.

Miaka mitatu Sasa tumeendelea kuwafukuza wale tuliowakingia kifua miaka ya nyuma Tena kwa kuwahita mafisadi na wezi wa Mali ya umma bila KUKUMBUKA kuwa hatukuwakabidhi hizo Mali za umma majukwaani au mbele ya vyombo vya habari bali tulijifungia nao ndani kwa kusaini mikataba ambayo si TU kwamba hatuna nguvu za kuitengua bali tukitaka kuitengua yatubidi tukakae kwenye mahakama zao huko nje ndipo tuzungumze.

Baada ya wageni hao kufungasha virago na kuacha uzalishaji hatujaacha kuwalindia Mali zao Hadi pale watakapoamua kuja kuendelea na uvunaji kwa mujibu wa mikataba Yao.

Thanks ageni wakaondoka tukaamini kuwa mawazo ya kimaskini yametutoka kumbe wapi, tumeanza kuwakamata hata wale wazawa waliokuwa waliopata nafasi za kuondoka serikalini na wakatumia akili zao kuomba na kupata ajira kwa mishahara mikubwa kwenye makampuni ya kigeni yaliyokuwa hapa nchini.Tunakimbizana kuwafilisi Watanzania wenzetu kwa sababu ya kuwaza kimaskini na kuwaaminisha watu kuwa tutakapomalizana na matajiri Basi MASKINI watakuwa matajiri,, kichekesho.

Tumekwenda mbali zaidi Sasa badala ya kuwazuia au kuwachuja wageni wanaokuja nchini tumeelekeza nguvu kubwa kuwadhibiti vijana na baadhi ya watu wenye maono na fikra wakiwemo hata wabunge kusafiri nje ya nchi hadi watoe notice kwa wakubwa flani au wapewe idhini na watu flani....biashara zitakwenda?

Kwanini tulichagua kupigia makofi kauli ya kwamba tutaishi Kama mashetani? Mashetani ni waasi, wauaji, wenye Roho za chuki, tamaa, wivu nk na ndiyo maisha yaliyopo mtaani kwa sasa. Je ndo kusema tupo kwenye njia sahihi?
 
Kwa sababu tumechagua kuwa na katiba inayomruhusu mkuu wa nchi kusema "hapangiwi". Akiamua tuwe maskini tunabaki vivo hivyo.

Tunapaswa kuwa na katiba ambayo wananchi kupitia bunge wanaweza kumpangia rais vipaumbele vya nchi kwa maana ya mgao wa fedha na kupitia teuzi za raisi kabla hawajaapishwa.

Bashite anaichafua serikali kabisa kabisa kabisa.

John Magufuli is fostering a climate of fear in Tanzania
 
Back
Top Bottom