Kwanini tulipie kodi za nyumba kwa mwaka?

Rio Tinto

JF-Expert Member
Sep 18, 2014
777
450
Wadau naomba nilete kwenu hii mada huru kuhusu hizi kodi za pango tunazowalipa landlords ama kwa lugha za kitaa ' Baba Mwenye Nyuma' nimefanya utafifiti na kugundua kuwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati ni Tanzania pekee ambapo mpangaji analazimika kulipia kodi ya mwaka mzima ama miezi sita wakati hakuna sehemu yoyote duniani ambapo mfanyakazi analipwa mshahara wake kwa mwaka in advance.

Naomba ikiwezekana tuanzishe petition ya kumuomba Raisi Magufuli aingilie suala hili ili tuweze kulipia kodi zetu kwa Mwezi kama tunavyolipwa makazini.

Nakaribisha maoni yenu wadau.
 
Wapangaji wa bongo wanasumbua sana kwenye kulipa, ni wazee wa visingizio lukuki lukuki ndio maana ni bora walipe mwaka mzima au miezi sita.
Ukiona huwezi nenda kapange kwingine maana nyumba sio moja.

Muda wa kuongeza kusumbuana na kufuatiliana unaupata wapi? Maisha yapo resi yanakimbia, no time to waste
 
Sidhani kama katika katiba Ya nchi hii hilo swala lime fafanuliwa Vizuri au la! Ni vema kujua kwanza katiba na sheria za makazi na upangaji zinasema nini ndipo tupate mwanga mzuri, sababu nchi nyingi kodi ya nyumba hulipwa kila bahada Ya mwezi mmoja sasa lazima serekali ifanye sheria ambayo ina wasaidia wananchi walio wengi sababu watu wengi wanashindwa kulipa numba sababu kodi ya miezi 3,6,12 ni ndefu sana. Nakwa hali nyingine Ya maisha hii ina onyesha Tanzania bado ni nchi ambayo nyumba zina bei chini sana kwa upangaji sababu nchi kama south africa hapa ninapo ishi sasa ivi huwezi kulipa kodi ya mwaka mzima au miezi 6 ni pesa nyingi sana ambazo yawekana huwezi shika hiyo Pesa kwa mwaka mzima. Hili ni swala la kutatuliwa kisheria
 
Wadau naomba nilete kwenu hii mada huru kuhusu hizi kodi za pango tunazowalipa landlords ama kwa lugha za kitaa ' Baba Mwenye Nyuma' nimefanya utafifiti na kugundua kuwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati ni Tanzania pekee ambapo mpangaji analazimika kulipia kodi ya mwaka mzima ama miezi sita wakati hakuna sehemu yoyote duniani ambapo mfanyakazi analipwa mshahara wake kwa mwaka in advance.

Naomba ikiwezekana tuanzishe petition ya kumuomba Raisi Magufuli aingilie suala hili ili tuweze kulipia kodi zetu kwa Mwezi kama tunavyolipwa makazini.

Nakaribisha maoni yenu wadau.

Tatizo wewe unachagua sana nyumba.Ziko nyumba za udongo zimeezekwa nyasi au makuti kodi yake unalipa kila mwezi.Kwa nini ung`ang`anie nyumba ya kodi ya mwaka mzima yenye maji,umeme na ving`amuzi wakati ziko nyumba hazina maji umeme wala maji za bei poa na masharti poa ikwemo kujisaidia porini huhitaji usumbufu wa kudeki choo.
 
Mkuu Rio Tinto mambo ya kodi ni maumivu sana kwa wafanyakazi,na serikali haina sauti kabisa kwenye hili,labda kama awamu hii wata amua kulivalia njuga.
 
Tatizo wewe unachagua sana nyumba.Ziko nyumba za udongo zimeezekwa nyasi au makuti kodi yake unalipa kila mwezi.Kwa nini ung`ang`anie nyumba ya kodi ya mwaka mzima yenye maji,umeme na ving`amuzi wakati ziko nyumba hazina maji umeme wala maji za bei poa na masharti poa ikwemo kujisaidia porini huhitaji usumbufu wa kudeki choo.
Ahahahahaaaaaaaaaaa hatari sana
 
Wadau naomba nilete kwenu hii mada huru kuhusu hizi kodi za pango tunazowalipa landlords ama kwa lugha za kitaa ' Baba Mwenye Nyuma' nimefanya utafifiti na kugundua kuwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati ni Tanzania pekee ambapo mpangaji analazimika kulipia kodi ya mwaka mzima ama miezi sita wakati hakuna sehemu yoyote duniani ambapo mfanyakazi analipwa mshahara wake kwa mwaka in advance.

Naomba ikiwezekana tuanzishe petition ya kumuomba Raisi Magufuli aingilie suala hili ili tuweze kulipia kodi zetu kwa Mwezi kama tunavyolipwa makazini.

Nakaribisha maoni yenu wadau.
Itabidi aanze na NHC. Na wenyewe wameanza kuingia mikataba ya miezi mitatu mitatu.
 
Back
Top Bottom