Inawezekana hukuelewa tu,uliambiwa Obama ana asili ya Kenya na sio Kenyan ktk maelezo yako umekiri kwamba baba yake Barack ni mkenya,then sioni ulipodanganywa. Kwa wakati ule dunia ndivyo ilivyokuwa,ama uende east-communism(CHINA,USSR) ama west-capitalism(USA,WESTERN EUROPE) au usifungamane na upande wowote na katika mifumo hiyo yote miwili mikubwa hakuna wenye uzuri kwetu Afrika pengine afadhali magharibi. Kumbuka mmoja katika hiyo ulishakufa!KWANINI TULIDANGANYWA OBAMA NI MKENYA.
#DUNIAYAKO No.2
Muandishi wa habari ambaye ni mchanguzi na mtafiti bwana Wayne Madsen kwa kupitia vyanzo mbalimbali vya CIA ameweza kugundua uhusiano baina ya CIA na watu muhimu katika maisha ya Barack Obama na mama yake, baba yake, bibi yake na baba wake wa kambo.
Tukianza na 'baba' yake na Obama ni kwamba alikuwa ni mmoja wa watu kadhaa waliotumiwa na CIA kwa ajili ya kusimamia mpango ambao utazuia siasa za ukomunisti kutoka China na muungano wa Sovieti usiingie Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla. Kennedy Foundation ilikuwa ikitoa pesa walizo ziita za ‘msaada’ kwa ajili ya kuwasomesha wanafunzi kutoka nchi za Afrika. September 12, mwaka 1960 Shirika la habari la Reuters kutoka London liliripoti kuwa mango unao itwa airlift ambapo fedha za Kennedy Foundation kwa ajili ya kuwasomesha watoto wa kiafrika Ulaya na Amerika si chochote bali ni mpango wa CIA kwa ajili ya kutoa mafunzo na kuwaanda vijana wa baadae wa kiafrika watakao tumika kwenye mapambano ya kisiasa dhidi ya China na Umoja wa Kisovieti kuzuia ushawishi wa kikomunisti kulimeza bara la Afrika.
Kinara na kibaraka wa Marekani hapa Afrika Mashariki katika mpango huu wa Airlift alikuwa ni bwana Tom Mboya ambaye alikuwa ni kiongozi wa chama cha KANU. Mboya alimchagua Baba yake na Obama kuwa kwa ajili ya kupata scholarship katika chuo cha Hawaii nchini Marekani ambapo huko ndiko alipokutana na mzazi mwenzake kwa Obama Dunham.
Jina kubwa ndani ya Kenya mpaka Marekani. Tom Mboya.
Tom Mboya alipokea dola za Marekani 100,000 kama msaada kwa ajili ya Airlift kutoka kwenye Kennedy Foundation na hii ni baada ya kukataa kiasi kama hicho kutoka US State Department na hii ni kwasababu fedha hizo ambazo zingeonekana zinatoka moja kwa moja kwenye serikali ya Marekani zingewaamsha walio lala kuwa Mboya ni kabaraka na ajenti wa CIA nchini Kenya lakini hizi za Kennedy Foundation ni wachache wangejua kuwa ni fedha kutoka kwenye mfuko mwingine wa suruali moja.[9]
Mboya akiwa na Kennedy, alitumiwa vizuri wakati wa utawala huo kuhakikisha viongozi wa Afrika hawajiungi na ukomonisti, divide and rule kama kawaida.
Airlift iliyoandaliwa na kupangiliwa na Mboya mnamo mwaka 1959 ilijumuisha wanafunzi kutoka Kenya, Uganda,Tanganyika, Zanzibar, Northern Rhodesia, Southern Rhodesia na Nyasaland. Baba yake na Obama hakuwa ni miongoni mwa wanafunzi wa mwanzo kudhaminiwa na Kennedy Foundation kupitia mpango wa Airlift ila ni miongoni mwa waliofuata baada ya hapo.
Kazi ya Mboya na wenzake ni kuhakikisha kuwa wanafunzi, vijana na viongozi wengine wa kiserikali ni vyama vya siasa hawajiungi na siasa za mrengo wa kushoto, siasa za ukomunisti. Hivyo Mboya alikuwa ni mtu mhimu sana kwa CIA. Katika mkutano wa mara ya pili uliofahamika kama All-African People’s Conference (AAPC) uliofanyika Tunisia Mboya alitumika kama tochi ya kuwamulika viongozi wote waliohudhuria kuona misimamo yao ya kisiasa na ikiwa kama ni wafuasi wa siasa za mrengo wa kushoto.
Tom Mboya ndiye aliyemuonganisha mtu ambaye anatajwa kama baba yake Obama kwenye mtandao wa kuwaandaa vijana wa Afrika kufuata maono ya Magharibi.
Katika mkutano huo kwenye ripoti ya CIA inaeleza kuwa palitokea msuguano na kutokuelewana kukali baina ya waziri mkuu wa Ghana Kwame Nkurumah na Tom Mboya. Mkutano wa mwanzo pia wa AAPC inadai ripoti hiyo kuwa Tom Mboya aliifanya kazi yake vyema ya kuwamulika viongozi hao na kupeleka ripoti kwa wakubwa zake.
Ni katika mkutano wa kwanza Mboya ndipo alimchagua baba yake na Obama kwenda kupata scholarship kupitia Kennedy foundation kwenye kivuli cha Airlift. Hivyo baba yake na Obama alikuwa akiaandaliwa kuwa ajenti wa CIA kwa ajili ya kufanya kazi sawa na ya Mboya.
Nkurumah alikuja kupinduliwa mwaka 1966 kwa msaada wa CIA na vijana wake iliyo waandaa kupitia mpango wa Airlift hapana shaka vijana wa Tom Mboya nikimaanisha Obama Sr. walikuwa na mkono kwenye kazi hii. Mwaka mmoja baadae mapinduzi mengine yalifanyika Indonesia ya kumpindua Sukarno kwa msaada wa CIA. Je unamjua mmoja wa waliohusishwa na mapinduzi hayo? Ni Ann Dunham, mama yake na rais Obama.
Inasemekana Mboya aliuwawa mwaka 1969 na maajenti wa kichina ambao walikuwa wakishirikiana na serikali ya Kenya kuondoa ushawishi wa Marekani nchini humo. Baada ya kifo cha Mboya kila ubalozi jijini Nairobi ulipeperusha bendera yake nusu mlingoti ispokuwa ubalozi wa China. Ushawishi wa Mboya kwenye serikali ya Kenya uliendelea muda mrefu hata baada ya kifo chake na hasa muda ambao Obama Sr. akiwa hai.
Dunham mama yake na Obama aliacha masomo katika chuo kikuu cha Huwaii mnamo mwaka 1960 wakati akiwa ni mjamzito wa mimba ya Barack Obama. Baba yake an Obama aliondoka Huwaii mwaka 1962 na kwenda kusoma Havard. Dunaham na Baba wa Obama walitalikiana mwaka 1964. Mwishoni mwa mwaka 1961 Dunham alirejea masomoni katika Chuo cha Washington akiwa na mtoto mchanga aliyeitwa Barack Obama.
Mwaka 1963 mpaka mwaka 1966 Dunham alirudi tena katika chuo cha Hawaii. Mwaka 1965 Dunhama aliolewa na Lolo Soetoro ambaye akawa ni baba wa kambo kwa Obama. Soetoro aliondoka na kuelekea Indonesia mnamo July 20, mwaka 1965 kama miezi mitatu hivi kabla ya uasi uliosimamiwa na CIA dhidi ya Surkano kufanyika. Ni wazi kuwa Soetoro aliitwa Indonesia na CIA kwa ajili ya kusaidia uwasi huo dhidi ya Sukarno ambao uligharimu maisha ya watu milioni moja wa Indonosia.
(Kennedy, Ton mbuya, Barack Wote watatu vifo vyao vinasemwa kuwa na mkono wa mtu nyuma yake)
Fuatilia post hii ya Oboma utajua mengi uliyofichwa katika histoiria yake. Tutajitahidi kila Siku kutoa post moja.
Tukutane post ijayo
Maoni yako ni muhimu.
Na wewe rekebisha SALASINI!Uzi una makosa "salasini na sita". Rekebisha.
Suala la dini siyo la kiasili, ni imani. Originally, baba wa Barack Obama alikuwa ni Muislam (kama sikosei ni "Hussein Obama" na mama wa Barack Obama ni mkiristo(u). Suala la dini yake halifuati dini ya baba wala mama. Anaweza Mkristo, Muislam au Idolator, au dini nyingine yoyote.wengine walidanganywa kua obama ni muislamu.
Kwahiyo mkenya kama kawaida yake aliiba? View attachment 966857
Aliyesema mtoto ni wanani alikuwa mama mwenyewe akiwa na sababu maalum..
huyu mama lazima aliangalia CV za wanaume akaona ya MJALUO wa kenya iko poa zaidi
teh teh teh Jokate naye ni mmarekani?1. Kwa sera za uraia wa Marekani: ukizaliwa Marekani ni Mmarekani; kwahiyo Barack Obama ni Mmarekani mwenye asili ya Kenya.
2.Sera za Uraia wa Kenya zinasemaje? Mkenya akizaliwa nje ya Kenya, let say azaliwe Tanzania, atakuwa Mkenya au Mtanzania.
NB: Huenda Marekani wanamtambua Obama kama Mmarekani kwa sera zao na Wakenya wanamtambua Obama kama Mkenya kwa sera zao.