Queen V
JF-Expert Member
- Jan 19, 2012
- 776
- 1,330
Wakuu salamu,
Kumekuwa na wimbi la lawama linaloelekezwa kwa marafiki likisindikizwa na "quotes" ama nukuu zinazokuwa namna hii ili tu kutupa guilt kwa kutonunua bidhaa zenu rafiki zetu.
"Your friends will not support your dreams, but random people will"
Sasa jamani tuje kwenye uhalisia. Hadi unafungua biashara unakuwa umeona hitaji la kile kitu unataka kuuza. Sasa ya nini tukumbushane mara mia tatu na maswali ya "sijapata oda yako" au "nikuwekee kijani au njano?"
Kuna rafiki nimemuepuka tangu Januari alipoanza biashara yake. Kanionesha bidhaa WhatsApp nikasema sawa na kusifia uzuri. Lakini mimi sihitaji hiko kitu atleast kwa sasa. Ni vema nimeona in the future nikiwa na hitaji nitamuambia. Ila sasa nasumbuliwa jamani sihemi.
Kwenye bajeti zetu tuweke na kipengele cha 'kitunza urafiki'? Vyuma jamani vyuma. Harusi tunachangishana sawa japo nayo si kitu poa wala nini ila si haki uninunulishe kiatu/pochi ambayo sihitaji kisa urafiki.
Kama kuna mnaofanya haya tuoneane huruma wajameni. Urafiki unakuwa very expensive. Tangaza biashara yako atakaye atakuja kununua, tusichunane kama mbuzi!