Kwanini tukio liwe karibu na Ubalozi wa Ufaransa?

Ninachoelewa mimi, hata mtu awe mlenga shabaha vipi, kulenga mtu anayetembea ni kazi kubwa na hasa unapolenga na kujibanza kwa kuibia.
Hamna kazi yoyote mkuu..
Kila kitu kina mafunzo hata wadunguaji wanafundishwa kupiga target inayotembea...we kimbia hata speed ya filbet bayo ila uta kutana tu na risasi. Sembuse huyo anae tembea tembea kwa kunyata.
 
Askari wa Africa hawa heshimu wahai wa watu, kwaza kulikua hamna haja ya kumumiminia lisasi nyingi mtu tayari kasha pingwa chini, askri wetu wanakosa uledi na professionalism.
Yah kabisa mkuuu, japo nadhani walikuwa wanazuia secondary threat ndiyo maana wakawa wanamuongeza risasi.

Secondary threat hutokea iwapo mnadhani mtu amekufa ilhali kumbe anawalia timing msogee ili achomoe bastola awamalize.
 
Mkuu yule jamaa alikuwa na AK mbili na alishaua watu kadhaa, unawezaje kuwaza unayowaza? Taarifa zitapatikana tu
Mimi na wewe tunawaza kitu kimoja, lakini alipopigwa risasi alikuwa amebaki na bunduki moja na inawezekana alikuwa na ile bastola yake bado.

Baada ya kumpiga na kudondoka, cha kwanza kabisa ni kuchukua silaha yake kama yule askari alivyofanya, lakini pia ilitakiwa kumgeuza na kumsearch kama ana bastola au vitu vingine vya kudhuru na kuvichukua.

Baada ya kujiridhisha jamaa hana threat tena, unatakiwa kucheck kama yupo hai, na kama yupo hai, polisi wanatakiwa wafanye wafanyavyo jamaa aishi ili atoe taarifa kamili.
 
Wewe unafikiri mtu mweneye tatizo la akili hawezi kutembea, kukaa, ama kuzungumza. Kubambikia watu kesi, kutesa wengine, kutumia madaraka vibaya kwa kuwatuma watu kwenye kuua wapinzani wako, kupoteza watu, hayo yote ni matatizo ya akili. Kama akili yako haina matatizo hauwezi kufanya hayo mambo.
Mimi naamini nigaidi. Na kama alikuwa hana akili nzuri, sidhani kama ile timing ya kuwauwa askari kwa pistol na kuchukua silaha zao ingefanikiwa.

Kuna tetesi askari mmoja wapo alikuwa anakimbia kuelekea baharini na jamaa akampiga risasi.

Jamaa ana akili timamu kabisa, kwa sababu hakutaka kuwauwa raia kabisa, yeye ilikuwa ni polisi.
 
Hii ni mental case. Psychoanalyst akiwekeza muda akafanya tracing ya maisha yake atapata majibu sahihi.

Tatizo letu sisi wabongo tunachukulia mambo simpo simpo sana. Mbele huko wapo tayari ku-uncover kila detail za mhalifu ili kupata ujuzi wa kudhibiti mambo yanayofanana yanayoweza kutokea siku zijazo.

Asilimia 90 ya matukio ya kihalifu na hata ugaidi yangeweza kuzuilika kama binadamu tungekuwa na umakini wa kujiuliza maswali ya ziada.
Kwa kweli hata mimi nakubaliana na wewe yule yuko mentally disturbed. Nimeangalia picha yake kuna mtu amepost sehemu amevaa viatu tafauti kwenye miguu yake. Hiyo peke yake ni ishara ya kuchanganyikiwa.
 
Mimi na wewe tunawaza kitu kimoja, lakini alipopigwa risasi alikuwa amebaki na bunduki moja na inawezekana alikuwa na ile bastola yake bado.

Baada ya kumpiga na kudondoka, cha kwanza kabisa ni kuchukua silaha yake kama yule askari alivyofanya, lakini pia ilitakiwa kumgeuza na kumsearch kama ana bastola au vitu vingine vya kudhuru na kuvichukua.

Baada ya kujiridhisha jamaa hana threat tena, unatakiwa kucheck kama yupo hai, na kama yupo hai, polisi wanatakiwa wafanye wafanyavyo jamaa aishi ili atoe taarifa kamili.
Angalia ile clip baada ya kuanguka, kuna askari alienda kumgusa shingoni, then rudi tuendelee
 
Hii inatakiwa iwe kazi kubwa kwa raia asie kuwa na mafunzo ya silaha,haitakiwa kuwa kazi kwa polisi waliokua trained
Mimi ninaomba siku moja uende range halafu upande gari inayotembea na upewe target. Kaka ni ngumu.

Ndiyo maana hawa jamaa wanatakiwa kufanya mazoezi kila mara.
 
Ukiangalia video ile vizuri inaishiria kwamba jamaa alikua na tatizo la akili, yule sii gaidi hamna gaidi wa namna hiyo, angekua gaidi zaidi ya police 10 wangekufa pale kwanza hawana shabaha mtu iko kati kati ya barabara peke yake bila kizuizi chochote wanapiga lisasi zaidi ya 20 na mnamkosa askari zaidi ya 30.
Mbona picha zinasambaa jamaa wa kishua sana ndo maana anamiliki piston.
NB: alikuwa na hasira za Tozo.
 
Kama Taifa bado tuna safari ndefu sana kuhusu tahadhari na utayari kwa suala zima la usalama. Mara nyingi nimekuwa najaribu kudadisi madhaifu ya polisi wetu ila nimegundua kitu kimoja kuwa WAMEBWETEKA sana.

Kuna vijana wengi humu mtandaoni huwa wanajitokeza kuomba nafasi za kazi kwenye vyombo vyetu vya usalama ila kwa sababu ya mifumo mibaya ya ajira tumejikuta tunabeba kila mtu hata ambaye hana sifa sababu kubwa tukiita CONNECTION. Vijana hawa ambao huwa wanajitokeza kuomba nafasi hizo wengi huulizwa unataka nini huko jeshini au Polisi?

Ni wazi kuwa kila mtu aliumbwa tofauti na mwingine yule, hivyo kila mmoja huwa anapenda kufanya kazi ambayo anaamini akiipata atakuwa bora sana katika kazi yake. Bahati mbaya vijana hao hukosa sapoti ya kufikia ndoto zao na tunaamua kuwa na vijana walioenda jeshini kwa sababu wamekosa ajira na ugumu wa maisha.

Hivyo umaridadi wa jeshi letu kuanzia kwenye utayari wa askari mmoja mmoja unakuwa mdogo sana maana kuna wengine wameenda kwa sababu hakuna ajira na wengine wameenda kwa sababu ndoto zao ni kuwa walinzi wa amani wa wenzao.

Hivyo basi Polisi na vyombo vyote vya usalama vijitahidi kubaini vijana ambao jeshi lipo mioyoni mwao, kama wanavyofanya tathimini pale wanapowataka vijana wa kazi maalumu au majeshi maalumu basi hata huku polisi wawatafute kwa gharama na weledi mkubwa siyo kuchukua kila mtu kwa sababu tu ni mrefu au anajua kusoma na kuandika.

Tengenezeni vijana wenye umakini popote pale walipo hata nje ya majukumu yao. Polisi wengi wamejisahau sana na hili liko wazi. Tunakaa nao tunawaona hata nguvu tu za kukimbia hawana na mwisho wa siku tunakuja kutegemea hao walinda raia na mali zao.

Mwaka fulani nilimwambia mtu mmoja kuhusu ndoto zangu za kutamani kuwa mlinda amani wa nchi yangu na kweli akapambana sana kutafuta nafasi ila ilipofika miaka mitatu bila majibu nilimwambia acha maana wakati ule ajira nilikuwa sina na nilikuwa vibaya sana kimaisha. Lengo la kumzuia niliona sitoenda kufanya kazi ile ambayo niliitaka kabla bali nitaenda kwa sababu ya njaa zangu na shida zangu.

IGP, tengeneza jeshi imara mkuu huyu jamaa wa leo katembea mtaani na tumetumia zaidi ya saa moja kumdhibiti, vipi kama angekuwa ndani ya Mall au jengo lolote lile lenye kusheheni idadi kubwa ya raia?
Well said mbao za mawe imagine hao jamaa wangekuwa watano ingekuwa ni gharika aisee
 
1. Angekuwa Hana akili timamu asingeweza kupiga risasi yule jamaaa aliyemfuata kwenye kibanda
2. Angekuwa Hana akili timamu angeua raia hovyo kwenye daladala, magari binafsi na bajaji..lakini yeye shida yake ilikua ni Askari tu
Yale ya Kibiti yanaanza kutokea mjini kati.. wapanda treni na daladala mu/tuwe makini.
 
Back
Top Bottom