Kwanini tukienda hospitali zile fomu za NHIF hawafungi hesabu pale chini?

ommytk

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
482
1,053
Habari za leo wadau kuna jambo mara nyingi nakutana nalo sijui kama wenzangu hili mmewahi kukutana nalo, kuna hizi form za matibabu NHIF unaenda hospitali unapata huduma kila gharama zinaandikwa kwenye form ukimaliza matibabu unaenda mapokezi kwa ajili ya kuchukua kadi yako ukifika pale inakupasa kusaini ile form ya gharama ulizotumia.

Ila sijawahi kuona ile form hesabu zimefungwa mara nyingi hesabu zinakuwa wazi, hii ni kwanini maana kuna uwezekano ikatokea hospital ambazo sio waaaminifu wakaongeza gharama ambazo hukutumia wewe, sasa sijui shida inakuwa wapi maana tunasaini hesabu ambayo haijakamilika kwanini hii NHIF waingalie kama ndio Sheria wabadili lazima mtu inasaini kitu halisi ulichotumia.
 
Ni kweli kabisa. Hili tatizo lipo. Kabla ya kusaini inabidi mstari wa kufunga uwekwe halafu nisaini. Kama NHIF mnashirikiana katika Hili, naomba Serikali iingilie kati si kubaki mnalalamika tu kwamba matumizi yamekuwa mkubwa wakati mnaacha mianya ya wizi ikiendelea.

Nssf zamani walikuwa wanafunga, baadaye wakaacha. Kama wanachama tunaomba Hili litazamwe upya.
 
Sio kila daktari anayekuona anajua bei ya dawa/huduma aliyokupa zilizoko kwenye mfumo wa NHIF
Hospital nyingine tayari wameunganishwa online ukisaini maana yake na gharama zimepigwa papo hapo automatic

Sasa ukija kwenye hizi hospital zetu za Serikali bado changamoto ni kubwa ya watendaji kwa upande wa bima, mtu anayeingiza madai kwenye mfumo unakuta ni mmoja anazikusanya anaingiza mara moja moja sana.

Ila yote kwa yote NHIF hawajui majukumu yao ukija kwa ngazi ya vituo vya kutolea huduma wako ofisini kusubiri waletewe madai mwisho wa mwezi wakati watendaji huku chini wa bima hakuna na hata ku-organize mambo na kituo ili hizi changamoto zitatulike.
 
Bora hata hao wasiofunga hesabu lakini wameandika kiasi. Kuna hospitali ya meno nilienda Magomeni wao hawajaandika chochote zaidi ya kutaka nisaini tu.

Nilipokataa akaja daktari mkuu (mwenye hospitali) akajifanya kumuwakia aliyekuwa reception lakini wazi inaonekana ndio mchezo wao.

Kuna TMJ polyclinic iliyopo chang'ombe, wao wana kawaida ya kutuma msg baada ya siku 2 ya kwenda hospitali kuonyesha matibabu yako yaligharimu kiasi gani. Nilikwenda nikacheki malaria tu na kuonekana sina na sikupewa hata paracetamol, baada ya siku 2 msg imekuja matibabu yaligharimu 170,000.

NHIF ni wapigaji lakini wamiliki wa hospital wapigaji zaidi.
 
Bora hata hao wasiofunga hesabu lakini wameandika kiasi. Kuna hospitali ya meno nilienda Magomeni wao hawajaandika chochote zaidi ya kutaka nisaini tu.
Ulitakiwa uwapigie NHIF kwa namba uliyoelekezwa na huo ujumbe kwamba gharama hizo huzitambui.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom