Seif al Islam
JF-Expert Member
- Nov 14, 2011
- 2,156
- 638
Nimesikitika sana kusikia jinsi ambavyo watendaji wa vyombo vya Ulinzi na usalama wakikataa kuhusisha tukio la mauaji ya polisi huko Mkuranga na ugaidi. Nieleweke kuwa sishabikii mauaji au ugaidi. Mshangao wangu unatokana na sababu zifuatazo :
1. Uchunguzi wa tukio zima ndio kwanza umeanza na hakuna majibu kuhusu kilichotokea na hivyo kuanza kusema tukio sio la kigaidi ni ku pre empty Uchunguzi. Wanasema no research no right to speak.
2. Tunayo sheria ya kupambana na ugaidi iliyopitishwa miaka ya 2000 baada ya mashambulizi ya kigaidi huko Marekani. Sheria tu kuwepo ni reflection kuwa kuna possibility matukio ya kigaidi kutokea na tofauti na hapo sheria husika haina maana.
3. Wapo watu waliowahi kushtakiwa kwa makosa ya kigaidi japo kesi nyingine zilifutwa kwa kukosa ushahidi. Wapo wengine huko Arusha walioshtakiwa kwa ugaidi. Kwanini tusiamini hata Mkuranga magaidi wanaweza kuwepo?
4. Tukio jingine kama hili liliwahi kujitokeza huko Mkuranga.
Naamini sababu hizo na nyingine nying zingeweza kutosha kuwazuia wasemaji kutokukanusha kuwa huo ni ugaidi na wangeacha Uchunguzi ukamilike. Hili sio la kitaalamu. Ni jaribio la kuridhisha mamlaka.